kutoka kushoto: Silas Mwakibinga,Shaffih Dauda,Rahim Zamuda na Said Mohammed.
Jukwaa lilioandaliwa na SOCCEREX kwa ajili ya kuzungumzia mambo kadhaa wa kadhaa yanayolihusu soka la Afrika pamoja na mianya ya kibiashara iliyopo limemalizika leo hii jijini Durban nchini Afrika Kusini.
Washiriki walitoka kila kona ya bara la Afrika na wengine walitoka nje ya bara la Afrika lengo likiwa ni kusikiliza mada mbali zilizokuwa zikitolewa na wazungumzaji mbali mbali kuanzia wafanyabiashara,viongozi mbali mbali wa mpira wa miguu,Wadau wa mchezo huo bila kuwasahau Mawaziri na viongozi mbali mbali wa Serikali.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizotoa wawakilishi kwenye hilo jukwaa,Mheshimiwa naibu waziri wa Habari,kazi vijana na Michezo ndugu Amos Makalla aliwaongoza watanzania wachache walioshiriki kwenye semina hiyo.
Watanzania wengine walioshiriki kwenye semina hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Azam FC ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa kamati ya ligi ndugu Said Mohammed,C.E.O wa kamati ya ligi ndugu Silas Mwakibinga bila kumsahau mmiliki na meneja mkuu wa African Lyon ndugu Rahim Kangezi.
Mara baada ya semina hiyo kumalizika washiriki hao walikuwa na haya ya kusema.
Silas Mwakibinga- C.E.O wa kamati ya ligi:
''kwanza nimegundua bado tuna safari ndefu,tuna mambo mengi ambayo tunapaswa tuyafanyie kazi kutokana na maada nyingi zilizozungumzwa na wazungumzaji mbalimbali,Binafsi nimevutiwa sana na mipango ya raisi mpya wa SAFA Dr Danny Jordaan alivyokuwa akizungumzia takwimu za kiufundi kuhusu nchi yake,nimevutiwa sana kusema ukweli takwimu zile alikuwa anazitoa kichwani bila kutumia karatasi na zilikuwa zinaonekana kabisa ni za na mtu ambaye ni mtendaji,akizungumzia
idadi na uwiano wa makocha wanaowalenga,uwiano kati ya makocha na wachezaji,wanatakiwa kuwafundisha makocha wa kila madaraja wangapi kwa mwaka na kutaka kuuendeleza mpira kuanzia ngazi za chini mpaka juu hiyo inaonyesha baada ya uwekezaji huo kufanyika nchi hii itabadilika sana kimpira,amezungumzia mpango wa nchi nzima wa kuzalisha idadi ya wachezaji pia mfumo wa kuchezwa kwa ligi za watoto nchi nzima,kwakweli nadhani haya mawazo yanafaa kuigwa na sisi viongozi wa mpira katika nchi yetu,lakini pia nimevutiwa na raisi wa chama cha soka cha Ghana Kwesi Nyantakyi alivyokuwa akielezea namna ambavyo vilabu vyenye madeni haviruhusiwi kucheza ligi nchini mwake''
SAID MOHAMMED-MWENYEKITI AZAM/MAKAMU MWENYEKITI KAMATI YA LIGI:
'Semina hii imetusaidia kutufungua macho hasa katika mipango ya kibiashara inayotokana na mchezo wa soka,kuna vitu tulikuwa tunavifahamu lakini hatukujua namna ya utekelezaji wake,semina hii pia imetusaidia kutupatia mawasiliano na wenzetu toka nchi mbali mbali kama vile Nigeria,Ghana na Kenya ikiwa ni pamoja na kutupa mbinu za namna hawa wenzetu wanavyoendesha ligi zao''
RAHIM KANGEZI- MMILIKI AFRICAN LYON:
''Vitu vingi sana vizuri vimezungumzwa lakini bila kuheshimu proffesionalism ichukue mkondo wake kamwe hatutapiga hatua,nimefurahishwa na mpango wa miaka 10 wa maendeleoya soka nchini Afrika Kusini,mpango unaonyesha namna ya kuwatafuta vijana wenye vipaji,lakini pia unavyozungumzia mfumo wa mashindano ya nchi nzima,namna ambavyo wataboresha miundo mbinu pamoja na teknolojia watakayoitumia ili kuhakikisha mipango yao inafikiwa,hilo kwa kweli limenipa matumaini makubwa''.
Hao viongozi wa timu kubwa hapa nchi mbona hawapo au ndio" magumashi united team"
ReplyDelete