Search This Blog

Thursday, October 24, 2013

MJADALA KUELEKEA UCHAGUZI WA TFF: NI AINA GANI YA RAISI SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI ( TFF ) LINAMUHITAJI KWA AJILI YA KULINUSURU SOKA LA NCHI YETU.

Uchaguzi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) unataraji kufanyika tarehe 27/10/2013.
Wagombea wawili ndugu Jamal Malinzi na Athumani Nyamlani wamejitokeza kuwania kiti cha Uraisi,sisi kama wadau wakubwa wa mchezo wa soka hapa nchini tumekuwa tuziona changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiukabili mchezo wa soka hapa nchini kwetu,

SASA WADAU MNAOMBWA KUTOA MAONI YENU JUU YA SIFA AMBAZO RAISI ATAKAYECHUKUA MIKOBA YA LEODEGAR TENGA AWE NAZO.

HAYA KAZI KWENU ILA TUSITUMIE LUGHA ZA MATUSI.




3 comments:

  1. Msimu wowote wa uchaguzi uwe wa kisiasa au wa aina nyingine yoyote kama huu wa TFF kwa sasa, ni fursa ya muhimu sana na hivyo ni vizuri ikatumika kwa busara mno ikiwa hasa tunataka mabadiliko ya kweli ya soka letu.

    Pia niseme kuwa sina maslahi yoyote ya moja kwa moja na mgombea yoyote wa nafasi ya rais wa TFF na hivyo ninao uhuru wa kutoa mtazamo wangu bila kupendelea mtu yoyote - kama mpenda michezo hasa soka.

    Kwa mtazamo wangu nashauri huu uwe wakati wa kuleta mabadiliko na kuwapa nafasi watu wengine ambao hawakuwepo ndani ya mfumo unaomaliza muda wake, kwanini? Iko sababu moja ya msingi -

    Kimazoea, ni vigumu sana kuleta mabadiliko ya kweli kama uko katika mfumo huo huo ambao wewe ni sehemu ya watendaji. Tafsiri yake, hasa ni kuwa kama ulikuwa katika mfumo huo huo na labda sasa ukasema ninalo wazo jipya la kuleta mabadiliko na maendeleo ya soka ikuwa mtanichagua, ok; hapa utasababisha swali: "kwanini hayo mawazo yako unayoita ndiyo muarubaini wa matatizo ya soka letu, huku yafanyia kazi ulipokuwa katika mfumo huu unaomaliza muda wake?

    ....pengine jibu litakuwa aaah unajua mie wakati huo sikuwa president wa TFF na hivyo nisingeweza kusukuma ajenda 1, 2, 3....ok; Hii nayo inazaa swali lingine: Je uko ushahidi wowote kama ulishawahi kutoa mawazo kama hayo "unayoita ya kuendeleza soka Tanzania" wakati ukiwa ndani ya mfumo unaoishia?; .....pengine aaah unajua...aaa, eee, iii, na unajua wakati huo nilifanya 1, 2, 3....ila kwa wazo 4, 5, na 6 uongozi uliokuwepo haukunipa ushirikiano etc. Swali: Kwanini hukujiuzulu ikiwa kweli wewe hukuwa sehemu ya tatizo la mfumo unaoishia? Aaah unajua....

    Kwakifupi utaona kuwa tunahitaji kitu kipya, mfumo mpya, mawazo mapya etc ili tujaribu kuota mabadiliko katika soka. Sisemi kuwa hii inatoa guarantee, never I am not saying so! Ila ninachoamini ni hiki: "You can't solve a problem at the same level of thinking" (kama ambavyo imesikika hivi karibuni wanasiasa wetu wanavyo "quote" hii kauli, ambayo kimsingi inaukweli)

    So Let's think for the Change & Actually be the catalyst for the change. Nadhani wakati umefika tuwajaribu wengine ili ifike mahali wao nao tuwaondoe ikiwa kama ahadi zao zitakuwa hazitekelezeki. Hapa naomba nieleweke vizuri, hatukusudii kufanya "trial & error" na hatima ya soka letu hapa ila kama hao ndiyo wagombea walio mbele yetu basi let's facilitate the change kupitia hao na kuondokana na mawazo yaliyoko ndani ya box ambayo kimsingi ili kubadili mtazamo ni lazima kutoka ndani ya box na kuwa nje.

    Upande mwingine sijui ni lini katiba ya TFF itatoa fursa ya viongozi kuwajibishwa kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nao ikiwa performance ya kingozi ndani ya muda wake iko poor.....kuna haja ya kutazama hilo nalo.

    ReplyDelete
  2. Mpira ni science siku hizi na kasumba ya dumba na ngai pamoja na kuing'ang'ania kwa muda mrefu lakini imeshindwa kutupa kilichotegemea. Sasa raisi ajaye atambue mpira ni science na katika ilani yake atupe mwelekeo kama nchi kushiriki World Cup, CHAN na vilabu vyetu kubeba ndoo katika mashindano ya kimataifa.

    Aiweke Tanzania katika ramani ya dunia kwa kutoa wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu na mpira kuwa sector miongoni mwa sector katika uchumi wa nchi hii. Kutambua umuhimu wa Simba na Yanga pamoja na kuona wanachama wao kama ni mtaji badala ya mfumo huu mpya wa kuwaponda na kutaka kuviua vilabu vikongwe kwa kisingizio cha kuua soccer.

    Kuleta mashindano makubwa nchini na kuimarisha usalama na ulinzi mpirani, kuliondoa kabisa jeshi la polisi katika kusimamia ulinzi mpirani hili kuuweka mpira huru na rushwa. Rushwa kutokuwa sehemu ya mpira si kwa waamuzi, vilabu na wachezaji.

    Kuweka mfumo thabiti wa kupima utendaji kazi katika ngazi zoote za uongozi wa mpira, kuhamasisha na kuongeza uwekezaji kuwe katika manifesto zao.

    ReplyDelete
  3. Kwanza kabisa napenda nichukue fursa hii kupongeza blog hii kwa kuamua kuweka mjadala huu uhenda wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wakapata mwanga wa kuanzia kabla ya kufanya maamuzi.
    Ndugu wadau wenzangu wa mpira wa miguu,naamini kila mmoja wetu anaguswa kwa namna moja au nyingine jinsi mpira wa nchi yetu ulivyo nyuma katika dunia hii ya kidigitali.!!Sote tunakumbukumbu nzuri sana ya uongozi wa Bw.Leodgar Tenga wakati anaingia madarakani mwaka 2004,ahadi zilikuwa ni nyingi japo yapo yaliyotekelezwa lakini kubwa la kujivunia ni kuwa Bw.Tenga ameweza kuweka msingi mzuri wa TFF Na kuwa taasisi huru.Sasa ni wakati wa kuleta maendeleo.
    Uchaguzi huu ndio wenye hatima ya soka la Tanzania kwa miaka minne(4) ijayo tayari tumesikia na kuona wagombea hususan wa nafasi ya urais wakijinadi naomba nichangie katika maeneo muhimu machache kwa kuuanza na Bw.Jamal Emil Malinzi:
    kwanza Bw.Malinzi anasema,Atahakikisha kuwa mpira unachezwa kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa,kuwa na ligi bora na yenye ushindani,kuwa na viwanja bora ahishii hapo anaenda mbali kuwa vyama vya mikoa na wilwya watapatiwa ruzuku ili viweze kujiendesha,AIdha anasema kuna haja ya kufufua mashinadano kama vile Taifa cup,na FA.Kwa haya machache kwanza nimuunge mkono na pili awe nadhamira ya dhati maana tayari fursa zipo za kuweza kufanikisha haya,mfano leo hii serikali ni kama dhamana kwa TFF hata wadhamini hawaogopi kudhamini suala nikuweka mambo wazi na uaminifu lakini kuhusu viwanja yeye jamali awashirikishe wamiliki wa viwanja ambavyo vingi vinamilikiwa na chama Tawala naamini ni wasikivu wataonyesha utayari wa kuwa na PPP katika hili.Lakini ambalo mimi binafsi Jamal aminigusa ni kuhusu kuaandaa mashindano ya u-17 Afrika,hili ndgu zangu linawezekana tena litatusaidia sana kama taifa tujifunze kwa Afrika kusini 1994,Bukinafaso na nk,Miundombinu ipo kama vile viwanja,mfano:TAIFA,UHURU,AZAM COMPLEX,CCM KIRUMBA(Ukarabati),GOMBANI PEMBA NA AMANI.Kwanini tushindwe?Inawezekana.Hapa kwa Malinzi nasema mimi sio mpiga kura ila nawasaidia nyinyi wajumbe kuwa huyu ni mtu sahihi ambaye naona anaweza akavaa viatu vya Bw.Tenga.
    ATHUMANI NYAMLANI:
    Bw.Nyamlani yeye kaja na kali ya mwaka kuwa katika kipindi chote alichokuwa msaidizi wa Bw.Tenga ameona kuna rushwa kwa hiyo atajitahidi kuwa mkali eti ,Atasimamia mazuri yote walofanya,yote kwa yote hana jipya sijamuelewa kabisa maana nilitegemea atakuja na jipya mfano Ataisaidiaje taifa kuwa natimu bora ya Taifa lkni hakuna jipya.
    MWISHO:
    Ndugu zangu wajumbe wa mkutano mkuu,mko wachache sana ila mnatumia Demokrasia ya uwakilishi tambueni kuwa mnawakilisha watanzania wapatao milioni 45 kwenye uchaguzi huu,Tafadhali likomboeni Taifa letu,hebu ingieni ukumbini mkimlilia mama yetu TANZANIA tambueni leo hii nchi inaenda kusimama kwa siku moja tu.,tukitafakari maamuzi yenu,basi hamna budi kutumia kalamu zenu vizuri,mkichagua vizuri mtbaki kwenye kumbukumbu nzuri za taifa hili lakini mkichagua vibaya HISTORIA ITAWAHUKUMU.Hebu fanyeni kama mnafanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi enzi hizo mkiamini kuwa kufeli kwako ni kuendelea kubaki nyumbani kulima ama kuchunga n'gombe na wenzako watakao faulu wanapanda treni kwenda mazengo! Naishia hapa kwa leo,
    Ni mimi Adili H.kinyenga
    Mdau.

    ReplyDelete