- Mashabiki wa Simba na Yanga wapagawa
Mashabiki wa Simba na Yanga katika sehemu mbalimbali za jiji
la Dar es salaam leo wamepokea kwa kishindo promosheni ya Nani Mtani Jembe inayoendeshwa
na bia ya Kilimanjaro Premium Lager nchi nzima kwa siku 75 ili kuleta mwamko
katika utani wa jadi kati ya mashabiki hao.
Kampeni hiyo ilipokelewa kwa kishindo baada ya wafanyakazi wanaoitangaza
kampeni hiyo wakiwa na msafara wa magari kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji
hususani yale ambayo ni maarufu kwa kuwa na mashabiki au makundi maarufu ya
ushabiki kama vile Wakali wa Terminal, Vuvuzela Tandale, nk pamoja na vijiwe na
matawi ya Simba na Yanga na kutoa burudani na maelezo ya kushiriki pamoja na
kuitambulisha rasmi mtaani kampeni hiyo ya aina yake.
Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Tandika wilaya ya
Temeke walisema kuwa kampeni ya Nani Mtani Jembe imeleta mwamko mkubwa sana
katika utani wa jadi uliopo kati ya mashabiki wa Simba na Yanga na pia wanaamini
itasaidia kuwaleta karibu zaidi mashabiki pamoja na kuibua mashabiki wapya.
“Jonathan Assey
alisema “Nimeanza kushabikia Yanga tangu nikiwa na miaka 14 lakini sijawahi
kuona tukio lolote kubwa la kusisimua namna hii ambalo ni mahususi kwa ajili ya
mashabiki, hivyo nawashukuru Kilimanjaro Premium Lager kwa kutukumbuka sisi
mashabiki na kutuletea hii kampeni”.
Meneja wa Bia ya hiyo, George Kavishe alisema jana kuwa katika
shindano hilo Kilimanjaro inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi
cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu
inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa
kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo
inapata fedha nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka
kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la
Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni
kununua bia ya Kilimanjaro ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.
Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona
namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani
na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha
anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa
amepunguza shilingi 1,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma
ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 1,000 kutoka
kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza
shilingi 1,000 kutoka kwa Simba.
Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha
zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku kuanzia leo Jumatatu
hadi siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.
Kavishe alisema kuwa mashabiki watakaoshiriki kwenye
shindano hilo kila siku pia watanufaika kwa kuchaguliwa watu 400 watakaokuwa
wametuma mara nyingi zaidi ambao pia watazawadiwa shilingi 5000 kila mmoja na
kufanya kiasi cha fedha zinazokwenda kwa mashabiki kuwa shilingi milioni mbili
kila wiki.
Mashabiki wanaweza kufatilia matokeo kila dakika kupitia
tovuti maalum ya Nani Mtani Jembe ambayo ni https://cms.rasello.com/kili.
Mashabiki wa Simba na Yanga wakiwa wanacheza kwa furaha jana wakati wa maandamano maalum yaliyofanywa kuitangaza Nani Mtani Jembe inayoendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa mashabiki wa jiji la Dar es salaam. Msafara huo utatembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kwa siku tatu kuitambulisha kampeni hiyo na kutoa elimu namna ya kushiriki.
Msafara wa magari yakipita katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana kuitangaza kampeni ya Nani Mtani Jembe inayowashindanisha mashabiki wa Simba na Yanga kuzipa shavu timu zao kupitia kampeni hiyo inayoendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager. Msafara huo utatembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kwa siku tatu.
Mbezi Joseph akimvalisha jezi ya Yanga shabiki wa Yanga Anastazia John (80) wa Mabibo nae alijitokeza kupokea msafara huu wa utambulisho wa Nani Mtani Jembe kwa mashabiki wa Dar.
No comments:
Post a Comment