Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kutimua vumbo kesho (Oktoba 19 mwaka huu) kwa
mechi tano huku Mbeya City ikiikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
nyingine zitakuwa kati ya Oljoro JKT na Azam (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri
Abeid, Arusha), Mtibwa Sugar na Mgambo Shooting (Uwanja wa Manungu, Turiani),
Ashanti United na Ruvu Shooting (Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam) na Kagera
Sugar dhidi ya Coastal Union (Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba).
Wakati
huo huo, Ligiu Daraja la Kwanza (FDL) nayo inaendelea katika viwanja nane kesho
(Oktoba 19 mwaka huu) huku Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ukiwa
mwenyeji wa mchezo kati ya African Lyon na Friends Rangers.
Nayo
Villa Squad itacheza na Green Warriors katika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi,
Polisi Morogoro na Kimondo (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Lipuli na Kurugenzi
(Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa) na Mkamba Rangers dhidi ya
Majimaji (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro).
Toto
Africans na Mwadui (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Polisi Dodoma na Polisi
Tabora (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), wakati Polisi Mara na pamba zitacheza
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
No comments:
Post a Comment