Athumani Nyamlani-Uraisi
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza orodha ya
mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa TFF na wa Bodi ya Ligi (TPL Board)
utakaofanyika baadaye mwezi huu.
Uchaguzi
wa Bodi ya TPL utafanyika Oktoba 25 mwaka huu wakati ule wa TFF utafanyika
Oktoba 27 mwaka huu. Kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa TPL Board na ule wa TFF
zimeanza leo (Oktoba 18 mwaka huu)
zitamalizika siku moja kabla ya uchaguzi saa 10 kamili alasiri.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni amewataja wagombea kwa upande wa TPL
Board kugombea uenyekiti ni Hamad Yahya Juma (Mtibwa Sugar), Makamu Mwenyekiti
ni Said Muhammad Said Abeid (Azam). Wanaowania ujumbe wa Bodi ya Uendeshaji ni
Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na Omary Khatibu Mwindadi (Mwadui).
Wagombea
kwenye uchaguzi wa TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emily Malinzi
(Rais), Imani Omari Madega, Ramadhan Omar Nassib na Wallace Karia (Makamu wa
Rais).
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita
na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus
Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza), Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Kanda
namba 3- Shinyanga na Simiyu).
Ali
Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali (Kanda namba 4- Arusha na Manyara),
Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo (Kanda namba 5- Kigoma na Tabora), Ayubu
Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo (Kanda namba 6- Katavi na Rukwa), Ayoub
Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve, Lusekelo Elias
Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na Mbeya).
James
Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge (Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma),
Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder (Kanda
namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima,
Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Irick
Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na Twahil Twaha Njoki (Kanda
namba 11- Morogoro na Pwani).
Davis
Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani),
Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said Balhabou na Omary
Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es Salaam).
Mbwezeleni
amewataka wagombea kufanya kampeni bila kukashfu wenzao, kwani Kanuni ya
Uchaguzi za TFF toleo la 2013 inatoa fursa kwa Kamati ya Uchaguzi kuwaondoa
wagombea wa aina hiyo kwenye uchaguzi.
No comments:
Post a Comment