Baraka Mbolembole
Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba SC watakuwa
uwanjani siku ya jumapili ijayo katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuwakabili mabingwa watetezi na mahasimu wao wa soka nchini Yanga SC, katika
mchezo wa raundi ya tisa. Timu zote zinatumia uwanja wa Taifa kama uwanja wao
wa nyumbani, ila katika mchezo ujao Yanga watakuwa wageni, na Simba watakuwa
timu mwenyeji.
Simba wapo juu ya Yanga kwa tofauiti ya pointi tatu, na
wanaweza kuongeza pengo hadi kufikia tofauti ya pointi sita ebdapo watapata
ushindi. Katika michezo nane iliyopita, Simba imekusanya pointi 18, huku
wapinzani wao wakiwa na pointi 15 katika nafasi ya nne ya msimamo.
ZILIPOTOKA
Simba iliifuinga timu ya Tanzania Prisons wiki iliyopita kwa
bao 1-0, wakati mahasimu wao Yanga walipata ushindi wa ugenini dhidi ya Kagera
Sugar, mjini Bukoba waliposhinda kwa mabao 2-1.
OKTOBA 20
Yanga wanapewa nafasi kubwa ya ushindi katika mchezo huo kwa
kulinganisha aina ya wachezaji wa pande zote mbili na kuwachambua katika
makaratasi. Kwa ubora wa mtazamo Yanga wnaoneka kuwa na pointi katika hili, kwa
kuwa wamekuanya wachezaji ' wa bei mbaya' katika kikosi chao ukilinganisha na
wale wa Simba. Lakini hiko si kigezo sahihi cha kuwapa ' pointi' mbele ya
Simba, ukizingatia tayari walionja radha ya kichapo waluipocheza na Azam FC,
huku Simba wakifanya vizuri na kuwa timu ambayo haijapoteza mchezo wowote hadi
sasa.
MBINU ZA MCHEZO
Mara zote Simba wamekuwa watala wa eneo la katikati ya
uwanja, pindi wakicheza na Yanga. Wana wachezaji ambao wanaweza kucheza katika
mfumo wa 4-4-2, au ule wa 4-3-3 kwa usahihi, mifumo hii imekuwa ni mizuri kwao
katika michezo ya ' DAR- PACHA' kwa kipindi kirefu sasa. Ila kuelekea mchezo wa
jumapili hii inaonekana kuna hatari ya timu hiyo ' kupotea' mchezoni na kutoa
utawala kwa timu ya Yanga ambayo pia inauwezo wa kusoma mifumo ya timu pinzani
na kuivuruga wakitumia wachezaji wao wa ' kazi'
Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni kwa wiki nzima amekuwa
akijinasibu kwa atashinda, wakati yule wa Yanga, Ernest Brandts amekuwa bize
kuhakikisha wachezaji wao wanaongeza kiwango chao cha uchezaji, umakini, na
nidhamu. Kumekuwa na tetesi kuwa makocha Kibadeni na msaidizi wake Jamhuri
Kiwelo, kuingia katika tofauti na baadhi ya wachezaji wa timu yao.
Ila sikupendezwa na namna alivyokuwa bize kuongelea mambo
hayo nje ya timu, makocha hao hawakujali ni sehemu gani nzuri ya kukaa na
kuzungumzia mambo yao ya ndani, ilikuwa ni kazi ya msemaji wao Ezekiel Kamwaga
kukanusha au kukubali kuhusiana na habari za kuwepo kwa ugomvi kati ya kocha na
baadhi ya wachezaji muhimu. Wakati muda umekaribia kufika na kila kitu kuwa
hadharani, makocha hao watakuwa wakikuna vichwa na kutazama ni namna gani
wanaweza kuleta ' heshima'.
Nassoro Masoud, Issa Rashid hawa watakuwa walinzi wa pembeni
wa Simba katika mchezo huo, japo anaweza kuingia Haruna Shamte upande wa
kushoto kama, Kibadeni ataamua kucheza kamari ili kujaribu kuwadhibiti
washambuliaji wa pembeni wa Yanga, Mrisho Ngassa na Saimon Msuva.
Yanga wana kawaida yao ya kuimaliza mechi yoyote ngumu
wakitokea pembeni ya uwanja, Ngassa ni mchezaji mjanja, mnyumbulifu, ana kasi,
chenga, na maarifa ya kufunga ama kutoa pasi, na uwepo wa Msuva upande mwingine
wa uwanja naona kabisa kulikuwepo na fasi ya Henrry Joseph katika eneo la
kiungo la Simba. Jonas Mkude ni kiungo mzuri sikatai ila bado ana mengi ya
kujifunza ili kuingia katika kundi la viungo bora nchini, ana shambulia vizuri,
ndiyo maana tayari ana mabao matatu katika michezo saba aliyocheza, ila si
mzuri katika kucheza mipita ya ' tackling' . Hivyo uwepo wa Joseph ambaye ni
mzuri katika vyote hivyo vingeweza kumfanya Mkude kuwa na nguvu ya kuisukuma
timu mbele na ,kuicheza huku wakiwa na jukumu la kuwasaidia walinzi wao wa
pembeni wakati wakiwa wanashambuliwa.
Mtu, mwingine muhimu kwa Simba katika eneo hili la kati ni
Amri Kiemba, alicheza vibaya katika mchezo wa mwisho wa watano hao wa jadi, Mei
18, mwaka huu na katika siku za karibuni amekuwa akionesha kiwango cha chini.
Kiemba amecheza michezo nane ya timu yake na hajafunga bao lolote kitu ambacho
kilimfanya kocha wake kumuweka benchi katika mchezo uliopita. Ila anaweza
kucheza vizuri siku ya jumapili na kuisadia Simba kwa kuwa Simba hadi sasa
haina mbadala wa nafasi yake. Mechi ambazo Kiemba ameshindwa kuongoza eneo la
kiungo Simba ilibaki ikimtegemea Haruna Chanongo, na hapo wakawa wanacheza na
kutegemea upande wao wa kulia ili kupata mabao, bila shaka Chanongo anaweza
kumsumbua mlinzi wa kushoto wa Yanga David Luhende ila na wasiwasi kuwa
anaweza kutumia muda mwingi kumsadia Chollo ili kumzima Ngassa, kama Yanga
wataongoza mchezo.
Kiemba, anauwezo wa kukaa na mpira na kupiga pasi nzuri za
mwisho huku rekodi yake ya ufungaji ikiwa ni nzuri pia Simba inaweza kunufaika
na vitu alivyo navyo na kujaribu kuwazima ' viungo- wahamasishaji' Athuman Idd
' Chiji' na Haruna Niyonzima, ambao waliweza kutawa eneo la katikati. Yanga
hawana safu kali sana ya mashambulizi, ila wana washambuliaji wa ' mechi
kubwa', Hamis Kizza na Didier Kavumbagu wanaweza kuwaumiza kwa mara nyingi
Simba endapo watarusu krosi, na pasi za kunyeza, sina shaka na uwezo wa Joseph
Owino, huyu ni mlinzi kiongozi wa wenzake mchezo, ila uwepo wa washambuliaji
wenye kariba ya Kizza na Kavu, utakuwa mtihani mkubwa kwao. Wanaweza kuibuka
muda wowote mchezo na kuimaliza mechi kama walivyofanya Mei 18
Amis Tambwe, Chanongo kwa pamoja wamefunga mabao 11 katika
michezo nane iliyopita, mabao manne pungufu yaliyofungwa na timu ya Yanga.
Tambwe amekua akinufaika na uwepo wa Bertam Mombeki ambaye amekuwa akiwapa
wakati mgumu walinzi wa timu pinzani, Mombeki hutumia umbo lake kumiliki kila
mpira unaopigwa katika eneo lao, ni mzuri kwa mipira ya chini na ni hatari
zaidi kwa ile ya juu, Tambwe yeye amekuwa ni bingwa wa kukaa katika maeneo ya
hatari na kutumia kila nafasi anayoipata kwa umakini mkubwa, ni mzuri katika
mipira ya ' kuunganisha', ana jua ni wapi goli lilipo, ila mara zote hutegemea
timu yake kucheza na kuongoza mchezo. Endapo Simba watamili mchezo Tambwe
atafunga mara mbili, kwa kuwa sijaona bado ubora wa sasa wa Nadir Haroub na
Kelvin Yondan, bado wapo katika kujiweka sawa na wamekuwa wakipoteana mara kwa
mara, ila Mbuyu Twite anaweza kuwasaidia kwa kuwasogeza Simba nyuma ili
kuwafanya wawe bize na kukaba.
NANI MSHINDI
Abel
Dhaira na Ally Mustapha wote wameonesha udhaifu katika maeneo yao, Dhaira
amefungwa mabao matano na Mustapha amefungwa nane. Kushina au kufungwa kwa timu
zao kutagemea na kikla mmoja kupandisha kiwango chake cha uchezaji wa mipira
iliyokufa, ushapu wa kuzungumza na kuitokea mipira. Atayayekuwa anatematema
sana bila shaka ataimamiha timu yake. Naipenda Simba, Shabiki wa
Yanga.....Dakika tisini za kukumbwa ' Mimi naikumbuka ile ya marehemu Mutesa,
akiaina fulani ya muziki katika moja ya kona za uwanja wa Taifa huku akionesha
ishara ya mkono juu'
0714 08 43 08
0714 08 43 08
Poor analysis,bias,spelling errors etc.
ReplyDelete