Usajili wa kiungo wa kihispania Ander Herrera umeshindikana baada ya ucheleweshwaji wa mambo na taratibu za usajili kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Japokuwa inasemekana kwamba United walikubali kulipa kiasi cha €36 million ili kumsajili kiungo huyo, vyanzo mbalimbali kutoka nchini Spain vinasema kwamba masuala kadhaa ya sheria ya kodi nchini Hispania yalisababisha dili hilo lisifanyike.
Mtandao wa ESPN unaripoti kwamba kutoka na masuala ya kodi gharama nyingine zisizozidi kiasi cha €6m zilisababisha United kushindwa kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ambaye amekuwa kwenye kiwango bora sana katika timu ya Bilbao.
United tayari walishamtaarishia namba ya jezi na maslahi binafsi yalishafanyika, huku Herrera akikubali kukubali kupunguzwa kwa maslahi yake binafsi ili kukamilisha usajili huo.
Lakini pamoja na kushindikana kwa dili katika dirisha hili, inaaminika United watarudi tena kwa kiungo huyo katika dirisha la usajili la mwezi January.
No comments:
Post a Comment