Search This Blog

Tuesday, September 3, 2013

PAMOJA NA KUMSAJILI FELLAINI, TATIZO LENGINE LA MANCHESTER UNITED NI KUTOKUWA NA MAWINGA MACHACHARI.……


Hapo jana usiku Manchester United ilikamilisha uhamisho wa kiungo Maroune Fellaini, pamoja na kukamilisha usajili huo ambao unaonekana kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo, kwa mtazamo wangu nadhani walikuwa wanahitaji zaidi kumsajili winga kutokana na utamaduni wa timu hiyo kutengeneza mashambulizi mengi kutokea pembeni,

Tangu enzi za kina George Best,David Beckham, Cristiano Ronaldo na Ryan Giggs ambaye mpaka sasa anaendelea kuichezea timu hiyo, Manchester Utd imekuwa ikisifika kwa kuwa na mawinga hodari. nadhani mapungufu makubwa ya Manchester Utd ni kukosekana kwa mawinga hodari katika siku za karibuni,na nadhani lingekuwa jambo la busara kwa David Moyes kama angemsajili winga kabla ya dirisha la usjili kufungwa hapo jana.

Viwango vya mawinga wa Man Utd msimu uliopita vilikuwaje?

Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa mawinga watatu wa klabu hiyo ; Ashley Young, Nani na Antonio Valencia:



Michezo
Magoli
Nafasi zilizotengenezwa
Pasi
Nani
11
1
11
2
Young
19
0
35
3
Valencia
30
1
40
5


Ukiangalia jedwali hapo juu utaona mawinga wote watatu hawakuwa na makali mbele ya lango la timu pinzani,wachezaji wote watatu kwa pamoja walichangia kwa 2.3% ya mabao yaliyofungwa na UNITED msimu uliopita, inasikitisha mchezaji kama Ashley Young alishindwa kufunga walau bao moja huku winga wa Sunderland Adam Johnson akifunga mabao matano.

Siyo tu wachezaji hawa walikuwa na msimu mbaya kwenye sekta ya kupachika mabao,pia hawakuwa na mchango wa kutosha kwenye sekta ya kusaidia wenzao kufunga kwa pamoja wote watatu msimu uliopita walichangia 19.6% ya nafasi za mabao zilizotengenezwa na Manchester United. Kwa upande mwingine wachezaji watatu wa Chelsea Oscar, Eden Hazard na Juan Mata kwa pamoja walitengeneza 47% ya nafasi zilizotengenezwa na Chelsea msimu uliopita.

Kiuhalisia Man Utd ilitegemea mchango mkubwa kutoka kwa hawa mawinga kutokana na utamaduni wa klabu kushambulia mara nyingi kupitia pembeni,kwa mantiki hiyo mawinga hawakuwa na msaada msimu uliopita kutokana na takwimu zilizopo kitu kilichopelekea Sir Alex Ferguson kulazimika wakati mwingine kumchezesha pembeni Danny Welbeck hasa kwenye baadhi ya mechi kubwa,na hicho kilidhihilisha Ferguson kutokuwa na imani kwa hao mawinga wake watatu.

Nini cha Kufanya?

Mazungumzo mengi ya wadau wa soka hasa mashabiki wa Man Utd walikuwa wakisisitiza timu hiyo kumsajili kiungo wa kati lakini sehemu ambayo kweli ilikuwa inahitaji marekebisho ya haraka ni kwenye ni pembeni. Nadhani walishaona hayo mapungufu ndio maana msimu uliopita walipambana kweli kuwasajili Lucas Moura na Eden Hazard lakini mwisho wa siku wachezaji hao walichagua kujiunga na vilabu vingine (labda ni kutokana na wachezaji hao kuhitaji mishahara mikubwa ).

Kwasasa Ashley Young ana umri wa miaka 28 na kusema ukweli hajaonyesha kiwango kukua tangu ajiunge na Man Utd akitokea Aston Villa, pamoja na msimu uliopita kukosa mechi kadhaa kutokana na majeraha lakini bado hajaonyesha cheche zake.

Nani ni mchezaji mwenye kipaji lakini amekuwa na kiwango cha kupanda na kushuka kama homa za vipindi tangia ajiunge na Manchester United.

Valencia ni mchezaji mzuri lakini hana rekodi nzuri ya kufunga mabao na kibaya zaidi ni winga pasee.lakini amekuwa na msaada kwa staili yake ya uchezaji amekuwa akiisaidia sana timu kuwa na balance kwenye upande wa kulia:


Ukiangalia jedwali hapo juu utaona Valencia alivyo na mchango kutokana na aina ya uchezaji wake, amekuwa akiisaidia timu kupanua uwanja hasa kipindi ambacho inahitaji huduma hiyo pamoja na Valencia kuwa na msaada bado kutokana na aina yake ya kiuchezaji timu himuhitaji katika kila mchezo. Uwajibikaji wake unamfanya kuwa na faida kwenye timu kuliko wenzake kina Nani na Young mfano tu msimu uliopita takwimu zinaonyesha alikuwa na msaada mkubwa kwenye ulinzi ambapo79% ya tackles zake alifanikiwa kuipata mipira kutoka kwa wachezaji wa timu pinzani msimu uliopita,huu ulikuwa mchango mkubwa kwa timu kwa jukumu lake akiwa kama winga.


Hitimisho.

Mawinga wa Manchester United wana udhaifu ukilinganisha na idara zingine ndani ya kikosi kitu kilichopelekea wachezaji kama Shinji Kagawa na Danny Welbeck kulazimishwa kucheza pembeni. Mimi nadhani Ashley Young na Luis Nani wanatakiwa kuongeza viwango vyao ingawa kuna kijana mpya Wilfred Zaha amabaye bado hana uzoefu.

Pamoja na Machester Utd kumsajili kiungo hodari Maroune Fellaini lakini mapungufu makubwa yalikuwa kwenye mawinga.

9 comments:

  1. Kaka, kama Moyes atakuwa amekusikia ataona unamaanisha kwamba Giggs anajaza nafasi. Pia jambo kubwa watu wanatakiwa waelewe kuna mifumo ambayo hulingana na mchezo ama homa ya mchezo kuweza kumfanya winger afunge ama atengeneze goli na Valencia na Nani sinashaka nao ktk hilo. Labda kama hapo ungekuwa unamzungumzia Ryan Giggs na Ashley Young. Kwakuwa Valencia na Luis Nani hawajatumiwa ipasavyo ama ilivyotakiwa.
    Fellaini hajakuja kimakosa sababu licha ya kwamba tuna viungo wa kati kama Tom, Fletcher lakini ujio wa Fellaini utaleta changamoto kwa hawa midfielders wengine ambao wameshindwa kuvivaa viatu vya Paul Scholes.
    Nadhani hapa umemlenga Giggs anajaza nafasi na Ashley Young anatakiwa kutumia kila nafasi aipatayo vizuri ili kujiimarisha klabuni.
    Sababu yalaiti kama mimi ndio ningekuwa team coach nisingekuwa na sababu ya kuendelea kumpanga Giggs na Young kwenye matches za nguvu na kasi kama ya Liverpool na Chelsea.

    Wasalaam.

    ReplyDelete
  2. Hello,

    Hii article umecopy mahali na kujaribu kutafsiri au wewe ndiyo mwandishi ? Ni vizuri kuonyesha kila mara kama wewe ni mwandishi na kama umecopy basi kuonyesha sources.

    Binafsi sikubaliani na baadhi ya statements, na at times inabidi kuchimba ndani zaidi maana tatizo linaweza kuwa mfumo na siyo player. Hivi winger kazi yake kufunga au assists- kupiga cross na ili kuwa effective, unapima kwa winger kufunga tuu, crosses tuu au na kukaba..? Maana kama unajua hii sio enzi ya akina Sunday Juma ya kukimbia na kupiga cross tuu, siku hizi wing-backs (beki mbili na tatu ktkmifumo mingi pia wanatumika kama wings, at times zaidi kuliko hao namba 7 na 11 )

    ReplyDelete
    Replies
    1. taja wapi amecopy siyo unakuja tuu unamshambulia mwandishi,huo ni mtazamo wake nawewe unaweza kuja na mtazamo wako pia,

      Delete
    2. Dah, sasa ndg yangu wewe kweli huelewi maana na hii alama ya kuuliza ?. Kama ungekuwa unaielewa basi husingekurupuka na kuona nimemshambulia bali nimemuuliza swali ?

      Delete
  3. inammana yeye anaijua Manchester UTD kuliko Wenye timu wenyewe!? Ina maanna SAF hayaoni hayo matatizo mpk Shaffih ayaone!? Me nadhani ni hisia tu na Mtazamo wake. Acha wazungu wafanye yao na sisi tubaki kuiga au kushangilia na c kukosoa as if sisi tuna viwangio vya Brazil au Germany and Spain for that Matter!

    ReplyDelete
  4. kaka shafii umechemsha

    ReplyDelete
  5. Jamani michezo ni amani na furaha....tuchangie kama wanamichezo na sio wanasiasa. Kusema ukweli Shaffih hilo ulilolichambua ni mtazamo wako kwa jinsi ulivyoona wewe na tunaliheshimu lakini hatujakubaliananalo. Sababu sometimes mifumo na mechi ndio humfanya kila kocha awatumie vipi wingers. Kunamfumo kama aliyousema kaka hapo juu kwamba winger analazimika kuwa full back anatokea nyuma kwenda kushambulia na kwahili utakuwa shahidi kama Valencia ni hodari na ameishatumika sana ktk mfumo huu.

    Kuna mfumo wa kukaa na mpira na kushambulia kwa kushtukiza hutegemeana na team mnayochezanayo inachezaji na Najua unajua Nani ni hodari wa kukaa na mpira na anamashuti ya mbali ya kushtukiza. Ndio maana wana wa United tumeyapinga maoni yako vikali kama nilivyosema hapo juu labda kama unamlenga Griggs wa sasa anajaza nafasi ktk timu licha ya kwamba pasi zake zinamadhara.

    Wasalaam

    ReplyDelete
  6. Kuna mfumo mfano timu ikacheza na team yenye mashambulizi hatari muda wote kiasi ikamlazimu kocha kutumia wingers kuwa kama mabeki wa kulia na kushoto. Mfano mzuri ukicheza na Barca kama Chelsea walivyowakamata kipindi fulani na Damien Duff alicheza vizuri sana siku hiyo akirudi nyuma kukaba kama fullback akichukua mpira kutokea nyuma na kupandisha mashambulizi kama winger hapo hata asipofunga au kupiga cross lazima ukubali mchango wa winger hiyo ya kushuka na kupanda. Naninakumbuka mechi hiyo ilikuwa ya kwanza ktk hatua ya awali na Chelsea ilipata matokeo vizuri Nou Camp na Duff alitupia na Drogba.

    ReplyDelete