Search This Blog

Thursday, September 5, 2013

MJADALA: NINI MAONI YAKO JUU YA SAKATA LA WAZEE WA YANGA NA UONGOZI WAO!

Wazee wa klabu ya Yanga wanapinga mambo mawili yaliyofanywa na uongozi wa klabu yao: 

1. kuleta Mhasibu mwenye asili ya bara la Asia na kumwajiri Katibu mkuu mpya ndugu Patrick Naggi kutoka   nchini Kenya,Naggi amerithi mikoba ya Lawrence Mwalusako aliyemaliza Mkataba wake.

2. Kiongozi yeyote ambaye anapaswa kuiongoza Yanga ni lazima awe mwanachama wa klabu hiyo.

24 comments:

  1. Tatizo la hawaa wazee wameona akija huyo mkenya atafuata taratibu za kuendesha klabu kwahiyo ule umate mate watakosa kwasababu kwa mujibu wa sheria pesa lazima itoke kwa matumizi sahihi

    ReplyDelete
  2. Mbona wakina manji wanapotumia fehda kuleta wachazaji hawagomi , vilabu vya simba na yanga kama vinataka viendele viachane na mambo ya kazamani

    ReplyDelete
  3. Viongozi wanastahili kuachiwa kuiendesha klabu kwa jinsi wanavyoona inafaa na kwa kadri ya malengo yao ya kuinufaisha klabu kwa miaka mingi, kazi zote za kitaalamu zina vigezo vyake sio tu uanachama. Mbona wazee hawapingi kocha wa nje anapoajiliwa au hawasemi vijana wao wanakosa kusajiliwa na wanasajiliwa wachezaji wa nje?

    ReplyDelete
  4. Mfumo ndo unao tugharimu ktk yote haya,kamwe tusitarijie maendeleo ya soka kwa nchi yetu kwa utaratibu wanaotaka hawa wazee.mie naona bado nyie waandishi wa habari mnalo la kufanya ktk hili. NAWASILISHA!

    ReplyDelete
  5. hawa wazee wa yanga nadhani wana tatizo la kwenda na wakati alafu kitu kingine wahandishi wa habari ndo wanao wapa viburi labda kwa kukosa habari ndo maana wanaenda kwenye mikutano yao kwani mimi sidhani kama katiba ya yanga ina kipengele ya wazee kufanya mkutano na waandishi wa habri sina hakika sana ila kuhusu hili wazee wamepepesa masikio au tatizo zile hela zinazo toka bila mpangilio utakuwa ndo mwisho wake kwani huyo Patrick Naggi angekuwa kitendaji zaidi. mimi nawaomba waachane na mambo ya kizamani hii yanga ya sasa inaitaji Cv ya ukweli siyo maneno tena alafu waache mambo ya kifikilia mambo ya simba na azam wafikilie kimataifa zaidi

    ReplyDelete
  6. hawa wazee wanasumbuliwa na njaa tu hakuna linguine lolote

    ReplyDelete
  7. Huyu mzee ni kigeugeu kweli!Mambo ya msingi hayaoni, mfano suala la Uwanja wa Yanga ulioahidiwa na uongozi tangu mwaka jana bado halieleweki,mwelekeo mzima wa timu kwa maana ya maandalizi ya timu kwa michuano ya kimataifa,kuongeza udhamini wenye manufaa kwa klabu,ukuzaji wa vipya kwa vijana wadogo ili timu iondokane na gharama kubwa za usajili kila mwaka,yeye haya haoni anazungumzia suala la Katibu mkuu!
    Hizi timu zetu bila kuondokana na haya makundi tegemezi kwa klabu ambayo yanachukua rasilimali za klabu bila kuchangia chochote cha maana tutasubiri sana kuyaonja mafanikio ya soka letui!

    ReplyDelete
  8. Hawajitambui mbaya zaidi naona umri wao unaenda na kila kitu na nahisi miili yao imechoka kubeba vichwa vya hao wazee na sasa vichwa vinakosa support vitakuaje na uwezo wa kutenda?

    ReplyDelete
  9. duh matatizo haya sasa.!!

    ReplyDelete
  10. So long hivi vilabu vyetu ni tegemezi,vitaendelea kukutwa na mambo kama haya hadi vitakapojitambuwa.Kuna siku mtu ataamuwa kumleta mwanawe awe kocha kama hamtaki anaondoa ufadhili.Vilabu vinatakiwa vibuni njia za kujitegemea waache haya mambo ya kutegemea mtu mmoja na haya ndio matokeo yake.

    ReplyDelete
  11. Nadhani kuna tatizo la elimu juu ya uelewa wa majukumu na mtu sahihi anayetakiwa kusimamia hayo majukumu katika taasisi. Hawa wazee wanatakiwa wajue ya kuwa sie mashabiki wa Yanga ndio wenye kuumia na maendeleo hafifu ya timu yetu. Wao hawana utofauti na siye tuliopo huku vijijini ambao hadi leo hii hatujawahi iona Yanga live zaidi ya kwenye redio zetu na tv's lakini bado tunatambua lipi zuri na lipi baya kwa timu yetu. Tofauti yetu na wao hasa sie vijana ni wao kuwa na umri mrefu wakiwa washabiki wa Yanga na si vinginevyo. Kama kweli wao ni wazalendo na walikuwa wana uchungu na timu yao katika keleta maendeleo mbona hadi leo tunazidiwa na mtoto wa chekechea ambaye hajafikia umri wa kuanza shule(Azam)na huku wao wapo siku nyingi? Huwa najiuliza ni watu gani wanawapa nguvu hawa wazee hadi kutoa masharti kwa UONGOZI uliochaguliwa na wanachama wote? wao ni sehemu ndogo sana ya hao wanachama. Ingekuwa ni amri yangu hata kuingia kwenye conference room na kuwaita waandishi wa habari wasingepata nafasi kwani kufanya hivyo ni kuondoa haki sawa kwa wanachama wengine. Kwa ufupi"" WASHABIKI AMBAO HATUNA HATA KADI ZA UANACHAMA NDIO WENYE KUUMIA NA MAENDELEO NA TIMU YETU KULIKO HAO WAZEE AMBAO KILA KUKICHA WANAMTAKA FULANI ILI NJAA ZAO ZIPUNGUE"". mtazamo tuu

    ReplyDelete
  12. ndugu shaffih unajua kuna mambo ya kuangalia wazee wanatakiwa kuwa na vitu vya msangi 1.kuangalia jinsi ambavyo katibu mkuu alivyo ajiriwa kwa usaili upi je walitangaza ajira 2 usaili ulifanyika lini? wapi? kisha ndio watengeneze hoja za kujadili.suala la pili ni kuhusu mhasibu ni kuangalia kulitangazwa ajira na vigezo vilivyo tumika ndio walete hoya kuliko kuwa na maneno yasiyo na hoja kusimamia.

    ReplyDelete
  13. Uswahili umetawala sana soka la TZ hasa katika hizi timu zetu kubwa. Soka la sasa lazima liendane na ueledi na sio ubabaishaji au kubahatisha kama ilivyo sasa. Huyo Katibu hajaja mwenyewe inamaanisha ameletwa na watendaji. Na ninachoamini mimi ni kwamba sio kila kinachofanyika katika klabu hao wazee wanajulishwa. Mimi nadhani wanataka kulinda maslahi yao na ndo maana wanataka Katibu wanaomtaka wao. Sioni kwanini wahoji au waseme hawamtaki zaidi ya kama ingekuwa vipi wangehoji sifa zaka. Wazee wangu soka limebadilika, lazima tubadilike. Mtabaki kuwa mahiri katika kupinga na kutimua viongozi wenu mpaka lini??? Mambo hayo yamepitwa na wakati, tuhoji mambo ya msingi yatakayoijenga klabu kulikoni namna hiyo.

    ReplyDelete
  14. Kwani hawa wazee kulingana na katiba ya Yanga wapo juu ya uongozi ? Nguvu hiyo ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari wanaipata wapi ? waachane na mambo ya miaka mingi iliyopita tuu

    ReplyDelete
  15. Bado namuona Francis Kifukwe kama nabii katika soka la bongo.... njia pakee itayosaidia vilabu vya soka ni kama vitaendeshwa kwa mfumo wa Kampuni, vinginevo longo longo hazitoisha!

    ReplyDelete
  16. Naona figisufigisu zimeanza

    ReplyDelete
  17. Kina choendelea sasa kwa klabu Yanga ni kitu cha kusikitisha nafikiri hawa wazee wanahitaji kuambiwa ukweli kwamba mpira wa sasa si kama ule wa zamani, sasa hivi mpira ni zaidi ya mapenzi kwa sasa mpira unahitaji mambo mengi ikiwemo utaalamu na si utaalamu wa kuloga ni elimu na ujuzi katika utawala ili kuifanya klabu isonge mbele. Umefika wakati hawa wazee watambue kuwa mawazo yao yangeweza kufanya kazi kwa miaka ya nyuma lakini si kwa sasa, mambo yamebadilika na wauache uongozi ufanye kazi yake, mafanikio ya klabu yataletwa na uongozi bora na sio bora viongozi na watambue kwamba Yanga inawafuasi wengi TZ wao ni kasemu kadogo sana cha mashabiki wa Yanga kwa hiyo hawawezi kuamua hatima ya klabu ya Yanga..

    ReplyDelete
  18. JE NI KWELI KATIBU KUTOKA KENYA NI SULUHUHISHO YANGA???MASHABIKI MSILETE USHABIKI BILA KUFIKIRIA MIPANGO YA KIUFUNDI NDIO ITALETA CHANGAMOTO KTK SOKA ACHENI USWAHILI JAMANI BENCHI LA UFUNDI NDIO LINAHITAJI WATAALAMU TU.....VINGINEVYO MAGUMASHI TU

    ReplyDelete
  19. Suala la kuajiri katibu mkuu kutoka kenya ni la kitalaamu sio la kishabiki hivyo wazee wa yanga wanapaswa kujua hilo kama wanadhani kila kiongozi ni lazima awe mwanachama hapo hawako sahihi maana FIFA na CAF wanataka viongozi wa vilabu vinavyoshiriki michuano inayoandaliwa na wao wawe na taaluma ya michezo sio kigezo cha kuwa mwanachama kama tutataka wanachama ndo wawe viongozi tuu bac itatubidi tuwe tunashiriki kwenye kombe la kuku, mbuzi na ngombe maana huku taaluma ya michezo haiangaliwi!!

    ReplyDelete
  20. Tafadhali Bwana SHAFFIH DAUDA TUOMBE RADHI sema wazee wa yanga wa dar es salaam sio wazee tuu maana wazee wa yanga wako tanzania nzima mpaka zanzibar asa ukiwasemea wote utakuwa umewakosea wazee waliopo maeneo mengine!!!

    ReplyDelete
  21. Hili ni jambo la kikatiba na kulijadili tunapaswa kujua katiba ya yanga inasemaje juu ya mchakato wa kuajiri katibu pamoja na vigezo vinavyo takiwa.

    ReplyDelete
  22. kwani hawa si ndio walio muweka manji madarakani sasa imekuwaje tena au ndio umatemate.hawa wazee wajanja sana wanatumia hii falsafa"be good to the people on your way up the ladder you may need them on your way down'.tatizo njaa na uongozi wenyewe uliwaendekeza.mambo mangapi huyo manji kafanyiwa na hao wazee ili kuteka hisia za wana yanga sasa alipe fadhila.uwanja vip

    ReplyDelete
  23. Huu ni upuzi mwingine wa soka la bongo. Katiba inataka katibu wa kuajiliwa na kuajili ni kazi ya management ya Yanga, Viongozi ndiyo wanapaswa kutafuta mtu wanayeona anaweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Huyo mtu haijalishi anatoka Tanzania, Kenya au Uholanzi. Kung'ang'ania awe mwanachama wa Yanga utakuwa ni wendawazimu. Tumeajili kocha kutoka Uholanzi, wachezaji kutoka nchi tofauti tofauti, vipi kwa katibu iwe nongwa? Eti hawataki mhindi awe mhasibu!!! Mbona hawakumkataa mwenyekiti? Vijana chukueni hatua dhidi ya hawa wazee vinginevyo hatuta fika. Katika vitu vinavyo niuma ni kuona Yanga inafanya mazoezi kwenye uwanja ambao ni sawa na ninaofanyia mimi na timu yangu ya MTAANI.
    ACHENI HIZO WAZEE.

    ReplyDelete
  24. shaffih hivi hawa wazeee kuna kitu akijakaa sawa kwao, sizani kama suala la muasia kuwa muhasibu ni jambo baya, tatizo ni kwamba shule inawasumbua

    ReplyDelete