Search This Blog

Tuesday, September 3, 2013

MAONI YA MDAU REVO ALEXANDRIA Jr JUU YA UJIO WA MESUT OZIL PALE EMIRATES STADIUM!

Watu wanasema ozili kasajili Arsenal kwa Kazi gani, wengine wanasema tatizo la arsenal ni kiungo na mabeki mpo mbali sana na kuijua arsenal ilivyo.

Takwimu za msimu uliopita za ligi zinaonesha arsenal ni team ya 2 kwa kutofungwa magoli mengi ikiwa imezidiwa na mancity iliyofungwa magoli 34 huku arsenal ikiwa imefungwa magoli 37. Sasa mniambie hilo tatizo la defense lipo wapi? Ukuta wa arsenal mnaosema mbovu ndio umefungwa magoli machache zaidi kuliko nyie mnajiona mnaukuta imara hapo msimu uliopita huku ukizingatia czscney alikua amedrop kiwango tofauti na sasa amerudi kwenye ubora wake.

 Arsene Wenger ana waamini sana wachezaji wake, so do I. Kuhusu striker atacheza Podolski alishawahi kucheza nafasi iyo before na alifunga magoli 18 akiwa na club ndogo ya fc colgne. Sometime muwe mna dig deep zaid kufikiria kwanini watu wana sajili ivyo, wakati Wenger anaanza kumchezesha Gervinho kama FALSE number nine alisema kua anataka kugeuza mawinga wawe kama strikers kasoro chamberlain tu ambae atakua kama central attacking midfielder.
 Ukiangalia Cazorla, Ozil, Rosick na ramsey hawa wote wanaweza kucheza number zote za kiungoni wakiwa kama ofensive players wanaweza kucheza kutokea kati kati, kutokea kushoto na kulia rotation itakayo fanyika japo kutakua hamna tofayti simu atakayo miss mmoja wao. Usajili wa arsenal ulikua mzuri na kusajili ozil ina maana kua jukumu la kufunga sio la strikers peke yao tutakua tunacheza na offensive players wengi na chance za kufunga zitakua nyingi kwakua hata hao Olivier giroud na podolski wanafunga na kuassist pia kwaiyo chance za kufunga zitakua nyingi sana na kipa mchezaji atakua anafunga.

Arsenal ilikua vizuri kabla hata ya ozil hajaja ila waswahili na wanafki walishindwa kuelewa mlikua mnaishi kwa kukalili, arsenal tangu ipoteze mechi na spurs mwanzoni kwa mwezi March msimu uliopita haikufungwa tena hadi ilipokuja kufungwa na Aston villa mwezi august, na baada ya ile game ya Aston villa tumecheza mechi nne tumeshinda zote tukifunga magoli 9 na kufungwa goli moja tu na Fulham, hiki kikosi kimekomaa Ramsey wa sasa sio Ramsey wa miaka miwili nyuma Ramsey amekua man of the match kwa mech tatu mfululizo na hii mechi ya juzi huyu Olivier giroud asingekua ana block mipira vile Ramsey angekua yeye man of the match kwa mara nyingine, kwakua wao wawili ndio waliongoza kwa perfomance ila Olivier alikua bora zaid kwakua Alishambulia na kuzuia zaid ya Ramsey.

Tulihitaji superstar mmoja wa kuboost hii team morari yake ikae sawa, tulihitaji superstar mmoja wa kurudisha fans wawe karibu na team yao, tulihitaji superstar mmoja ambae ni mtu wa mpira atakae kua anautaka mpira kila saa, na kwa ozil jibu limepatikana, jana shangwe iliyokua pale emirates makelele ya mashabiki wa arsenal mara ya mwisho shangwe zile kutokea ilikua kwenye usajili wa Denis bergkamp mwaka 1996.

3 comments:

  1. mmh,ngoja ifike December tutajua kama yaliyomo yamo,haya maneno tu ukweli tutauona uwanjani

    ReplyDelete
  2. acha wizi wa post za watu

    ReplyDelete
  3. ARESNAL ina defence nzuri? ok let's wait tutaona huko mbele kama uliyoongea hapo yana ukweli.But what i know ni kwamba Arsenal ina kikosi finyu cha kuweza kucheza michuano.Ina maana kelele zote za mashabiki wa Arsenal kumuambia Wenger asajili ilikua ni kwasababu ya kucheza pale mbele?

    ReplyDelete