Usajili wake ulikuwa ndio mwanzo mpya wa zama za Galacticos ndani ya Madrid. Florentino Perez alikuwa amerejea kwenye uongozi wa Real Madrid wakati wa kiangazi mwaka 2009 na kaka akawa mchezaji wa kwanza kuwasili Bernabeu katika project ya kuijenga upya Madrid. Lakini miaka minne baadae, mbrazil huyu yupo tayari kuondoka Santiago Bernabeu kupitia mlango wa nyuma - mchezaji ghali zaidi ambaye amefeli kufikia mategemeo.
Akiwa ndio mchezaji wa kwanza katika kuijenga Galacticos mpya chini ya Perez, kuwasili kwake kulitoa matumaini kwa mashabiki kwamba timu yao sasa itarudi kwenye utawala wa soka barani ulaya baada ya kunyanyaswa na mahasimu wao Barcelona katika msimu wa 2008-09. Na kiasi cha €65 million kikalipwa kwa ajili ya kupata saini ya mshindi wa Ballon d'Or 2007 hivyo kumfanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi duniani akitokea AC Milan.
Cristiano Ronaldo akafuatia kutokea Manchester United katika dili la uhamisho ambalo lilisababisha kelele nyingi za wanauchumi ukizingatia matumizi hayo makubwa ya Madrid yalikuwa yakifanyika wakati wa mwanzo wa anguko la uchumi duniani. Lakini miaka minne sasa imepita na hakuna anayezungumzia tena gaharama waliyoingia Madrid kuweza kumsajili kijana kutoka mitaa ya Madeira, ambaye ameshafunga mabao 201 katika mechi zisizozidi 200 - ambayo ni rekodi ambayo haijwahi kuwekwa na mchezaji yoyote aliyewahi kuvaa jezi nyeupe za Madrid. Kaka, kwa kumfananisha na Ronaldo, hajatoa sababu yoyote kuwafanya Madrid kuona thamani ya fedha waliyotumia juu yake. Alinunuliwa kwa €65m na analipwa vizuri kabisa kiasi cha €10m kwa mwaka baada ya kodi, kwa maana hiyo fedha zote hizi ambazo zilitumika kwa ajili ya kiungo wa zamani wa AC Milan zimepotea.
Msimu wa kwanza wa mbrazil huyu chini ya kocha Manuel Pellegrini ulitawaliwa na majeruhi na aliweza kucheza michezo isiyozidi 33, akifunga mabao 9 tu.
Msimu wake wa pili ndio hali ilikuwa mbaya zaidi. Kaka alienda kuitumikia nchi yake ya Brazil katika fainali za 2010 World Cup na kurejea Real Madrid akiwa katika hali isiyoridhisha, akihitaji operesheni ya goti ambayo ilimuweka nje kwa miezi kadhaa. Wakati aliporudi, kocha Jose Mourinho alisema Kaka alikuwa kama "usajili mpya", lakini hakuweza kuvuka michezo 20 ndani ya msimu mmoja na kufanikiwa kufunga mabao 7 katika msimu wa 2009-10.
Kaka baada ya hapo alihusishwa na kuondoka katika wakati wa kiangazi, lakini bado akataka kuendelea kubaki Bernabeu. "Sitoondoka hapa mpka niwe mshindi nikiwa na Real Madrid," aliahidi. Ilionekana na jambo jema.
Msimu wa 2011-12 ulikuwa ndio bora kwake akichukua nafasi ya majeruhi Angel Di Maria na akaenda kuichezea Madrid mechi 40 katika mashindano yote. Madrid wakashinda La Liga na akitoa mchango kiasi fulani Kaka - lakini bado akiwa chini ya kiwango chake alichokuwa nacho San Siro. "Kaka alikuwa bora sana laivyokuwa AC Milan," Mourinho alisema wakati akizungumzia kiwango kizuri alichoonyesha mbrazil huyo dhidi ya CSKA Moscow. "Lakini amekuwa anajituma kuliko hivi sasa. Anajitoa kwa ajili ya manufaa ya timu."
KAKA AT REAL MADRID: 2009-2013 | |
Total games Goals Assists La Liga titlesTotal trophies |
120 29 32 1 3 |
Pia Madrid walikuwa tayari kufanya hivyo. Lakini hakuna klabu iliyokuwa tayari kulipa kiasi cha €20m kucheza kamari ya kumsajili kiungo huyo wa kibrazil, wakati mshahara wake pia ukawa kikwazo kikubwa katika uhamisho wake. Lakini bado Kaka alikuwa radhi kubaki Madrid mpaka mkataba wake utakapoisha 2015.
Mambo yamebadilika, japokuwa Kaka alikuwa na mawazo kwamba atapata nafasi kubwa ya kucheza katika cha sasa cha kocha wake wa zamani wa AC Milan Carlo Ancelotti, lakini amekuwa akitoswa na hilo limeonekana katika michezo miwili ya kwanza ya Madrid ya ligi na sasa mchezaji huyo ameleezea matamanio yake ya kuondokakwenda kwenye klabu ambayo itampa nafsi ya kuonekana aweze kurudishwa katika kikosi cha Brazil kwa ajili ya michuano ya mwakani ya kombe la dunia itakayofanyika nchini kwao.
"Nataka kuondoka," Kaka aliwaambia maripota baada ya kufunga mara mbili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Deportivo La Coruna katika mechi ya hisani ya kumbukumbu ya Teresa Herrera Alhamisi iliyopita. "Nadhani ni wakati sahihi kwangu na klabu kwa mie kuondoka. Nimeongea na Carlo Ancelotti na klabu. Wote wanajua."
Kutoka kuwa mshindi wa Ballon d'Or kwenda kukali benchi la Santiago Bernebeu, Kaka ataandikwa kwenye historia kama mchezaji 'flop' aliyeigharimu Madrid zaidi ya €100m katika kipindi cha miaka minne. Hivyo akiwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na akiwa mbali kabisa na zama za ubora wake ambao alitegemewa kuwa nao, bodi ya wakurugenzi wa Real itakuwa na furaha kuona kiungo mwenye miaka 31 akiondolewa kwenye listi ya wachezaji wanaolipwa mishahara mizito na mchezaji mwenyewe akiwa na furaha kwenda kupata nafasi ya kucheza soka tena ikiwa tu atapata timu kabla ya dirisha la usajili haijafungwa kesho usiku Jumatatu.
No comments:
Post a Comment