Search This Blog

Thursday, September 5, 2013

KUNA KOSA MANCHESTER UTD IKICHEZA KWA MFUMO HUU?

Wadau wa mpira hasa wa Manchester united. Njooni tudiscuss mpira hapa kuhusu team yenu, me nimekua na wazo hapa nataka mnikosoe pale ntakapo kua nimekosea.

Hivi mnaonaje kikosi chenu kikiwa kama hivi nitakavyokitaja, hizi ni technique zangu ambavyo ningechezesha kikosi chenu na nitatumia mfumo wa 4-3-3.

Goalkeeper:
 David De Gea kama kawaida hana mpinzani.

Ningewatumia Ferdinand na Vidic kama mabeki wa Kati, Vidic akiwa kama stopper na Rio akiwa kama sweeper, kwaiyo Vidic awe anakaba alafu Rio awe ana-clear mipira na kuangalia offsides, ila wanakua wanabadilishana kutokana mazingira husika ya Mashambulizi mkiwa mnashambuliwa, na mkiwa mna attack hawa defenders wawe wanasimama pembeni ya nusu duara ya lile duara la katikati ya uwanja kwa hii nusu ya chini upande wa half yenu..

Alafu ningetumia fullback wawe wanatanua uwanja wanatembea wao pembeni ya uwanja wakiwa kama ndio wapiga cross mkiwa mna-attack na mkiwa mna- defend hawa fullbacks wawe wanaingia kwenye penalty box kuzuia, na fullbacks hao ningechagua Evra na Rafael.

Alafu defensive midfielder angecheza Carrick, team ikiwa ina defend huyu defensive midfielder anatakiwa awe anakaba nje kidogo au ndani kidogo ya penalty box, na wakati team inashambulia basi jamaa awe amesimama nje kidogo ya nusu duara ya dimba la juu la upande wa wapinzani, tena akiwa usawa wa katikati kati ya mabeki wawili wa nyuma.

Alafu ningemuweka fellain akiwa kama box to box midfielder huyu kazi yake inakua ni kuendesha team wakati mkiwa mna attack yaani yeye ndio awe wa ku-dribble mpira kwa distance ndefu pale Kati Kati ya uwanja mpira ambao atakua ameanziwa pass fupi na Michael Carrick, na wakati wa kuzuia huyu felain anatakiwa yeye ndio aanze kumkabia mipira defensive midfielder wake, kwakua yeye sio mtu wa mwisho Ana ruhusiwa kujaribu kuwin mpira kutoka kwa attacker.

Alafu kweye role ya number ten ningempanga Shinji Kagawa ambae ni playmaker atakua anacheza nyuma ya striker kazi yake kubwa itakua ni kupasia final balls kwa washambuliaji wote watatu wa juu au awe anafunga mwenyewe akipata chance, na wakati wa kuzuia huyu Kagawa awe anarudi mpaka ndani ya duara la Kati upande wa nusu duara ya goli lake kuja kuongeza watu wa kukaba.

Alafu washambuliaji ningemuweka van persie ashambulie akitokea kushoto na wyne Rooney ashambulie akitokea upande wa kulia na chicharito angekua striker, sasa hapa huyu vanpersie na Rooney hawatakiwi kucheza mbali sana na penalty box wawe wanacheza nje kidogo, ili waweze kufunga magoli na pia huyu chicharito anakua anasumbua ndani ya box akisubiri Pass kutoka kwa Kagawa, vanpersie au Rooney au pia awe ana subiri rebound kutoka kwa goalkeeper wa team pinzani, na wakat wa kuzuia huyu striker atarud had usawa wa katkat ya uwanja, na hawa washambuliaji wa pembeni hapa sasa ndio wata tanua watasimama pembezoni mwa uwanja kwenye maeneo ya fullbacks kwakua wakat huo fullback watakua ndan ya penalty area Yao.

Nimeamua kuwaweka pembeni Rooney na vanpersie kwakua ni wachezaji wazuri wanaweza kuperfom vizur kwenye position zaid ya moja alafu hua hawana uchoyo kuwatengenezea wengine nafasi wafunge na pia wanajua kukaba vizuri ili kutokana na wao wanapaswa wafunge basi hawatakiwi wacheze mbali na penalty area.

Nina amini kwa uwezo wa Kagawa visions na passing ability alikua nayo ata tengeneza chance nyingi za kufunga na kutokana na uchu wa magoli wa vanpersie na Rooney wataruhusiwa kushoot ili chicharito aweze kufunga rebound zitakazo zinatokana na mashut hayo kuokolewa na kipa.

Na substitution hapo nitafanya hivi nitamtoa fellain kama amechoka na kuingiza Anderson ikiwa team inahitaji kupush magoli zaidi Anderson hua anajua kutembea na mpira, na nitamtoa felain na kumuingiza cleverly ikiwa team inahitaji kumaintain possession, na kama team ikiwa inahitaji kuzuia basi nitamtoa felain na kumuingiza Phil Jones aje kucheza midfield na Carrick. Au kama Carrick huyo akichoka basi nitamuingiza Phil Jones kucheza iyo nafasi.

Hapo inaonekana substitution nyingi inamuhusu fellain kwakua iyo role ya fellain ni ngumu kuliko zote kwakua anatakiwa acheze kwa 100% wakati wa kushambulia na wakati wa kuzuia, so akicheza hadi dakika ya 70 atakua ameanza kuchoka na hapo matokeo ya mech yataonesha kama nitahitaji kumuingiza cleverly au Anderson.

Na kwenye sub za strikers nitamtoa chicharito na kumuingiza Luis nani aje kucheza upande wa kushoto na vanpersie atasimama striker, au nitamtoa Kagawa nitamuingiza zaha, then Rooney anaingia kucheza number ten na zaha atacheza kulia, alafu dany wilbeck atakua backup ya zaha na luis nani kama mmoja wao hatakuwepo atacheza welbeck.

Wachezaji wa defensive watakua wana piga straight long pass kwa washambuliaji watatu wa juu ikiwa tu washambuliaji hao watakua wamekaa kwenye nafasi nzuri ya kupokea mipira, ikiwa washambuliaji wamekabwa basi defensive midfielder atapiga short pass kwa box to box midfielder ambae huyo box to box atajaribu kusogeza mpira mbele kwa kudrible tayari kwa kumpasia playmaker au kwa forwards.

Kutokana na washambuliaji wa pembeni watakua wanacheza karibu na penalty box basi hawa fullbacks ndio watakao takiwa wawe wanaenda na move hawa ndio watakao kua wapiga Cross.

Hapo soka ni la speed na mchakamchaka kama kawaida yenu mkiwa kwenye ubora wenu.

 Imetayarishwa na Joel Chuku Verminator:

13 comments:

  1. ,kaka mawazo yako ni mazuri sana hasa kwa soka la kisasa linalochezwa na timu nyingi barani ulaya...pia umetoa uchambuzi mzuri kwa kuwaweka nje mawinga wa man maana kwa sasa wameshindwa kuisaidia timu katika upatikanaji magoli...kuhusu chicharito , m naona anastahili kupewa nafasi uliyompa kwani uchezaji wake unamfanya awe hatri anapozurura ndani ya box wakati RVP na Wazza wanaweza kuwa na madhara hata kutokea pembeni...Moyes nahis bado ajajua kumtumia vizuri kagawa...katika mech 3 man ilizocheza nafasi ya kagawa imeonekana wazi,man u inahitaj kagawaacheze zaidi ili kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na pia kutengeneza nafasi nying za kufunga...ni hayo tu

    ReplyDelete
  2. Sitazungumzia fomesheni hiyo hapo juu,lakini mchango wangu unaweza kuigusa.Kiufundi ni kwamba pamoja na mifumo ya soka, Ferguson alikuwa na kitu cha ziada kilichotokana na personality yake ambacho kilichangia kuifanya Man U iwe vile,kitu hicho Moyes hana na makocha wengi hawana na hivyo kwa sasa Man itabakia kuwa timu ya kawaida sawa na Arsenal,City na Chelsea.Uwepo wa Fergie kwenye bench la ufundi ulikuwa na impact kwa waamuzi,wachezaji wa Man na wapinzani na hata washabiki na hivyo wakati mwingine kusababisha matokeo mazuri kwa Man.Aina ya wachezaji aliosajili walitokana na falsafa yake na hivyo walikuwa wanapigana hadi dakika ya mwisho,ni wapambanaji.kWA FOMESHENI YA HAPO JUU NI DHAHIRI KWAMBA rOONEY NA cHICHARITO MMOJA LAZIMA ASUBIRI BENCH ILI KUWAPISHA aSHLEY yOUNG,wELLBECK AU vALENCIA.

    ReplyDelete
  3. Mm nilikua nawazo tofaut kidog. formation iwe iyo iyo 4-3-3 but wachezaj wawe ivi,
    1. DE GEA
    2. RAFAEL
    3. EVRA
    4. VIDIC
    5. RIO
    Af katkat kunakua na mido wa wili deep na mchezeshaj 1, but hawa deep mmoja anaruhusiwa kuzunguka na kuja kukaba kwa haraka (fellaini anaweza zaid). na mido hao ni.......
    CARRICK
    FELLAINI
    KAGAWA

    Na juu kunakua na CF, SS na FRW na huyu FRW anakuwa anasaidia kukaba kwa haraka pale wanapokua wanadefend(VALENCIA anaweza zaidi) na hawa wa juu ni kama.......

    CF. RVP
    SS. ROONEY
    FRW. VALENCIA/NANI/ZAHA/ANDERSON/LINGARD

    YOUNG asaidie kuokota mipira, tutamtoa kwa mkopo dirisha dogo.

    ReplyDelete
  4. previous comment ya 433
    RAMADHAN MAJID MWANANA
    DAR.

    ReplyDelete
  5. Vituko hivi Felain hawezi kudribble au kucheza mpira wa kisasa labda ule wa kizaman kusukumana sukumana na kukumbana huyu ni mzur na anamfaa Sam Aladiyce.
    ManU wapuuzi wamenunua bonge la kiungo Kagawa lakin anachezeshwa left wing wakati hii ndo namba 10 bora iliyopo Man U.
    Moyes hawezi badili mfumo wa man u coz kaletwa man u coz ni muumin wa 4 4 2 akibadili ni 4 5 1 mifumo aliyokuwa anaitumia Fergie na mafail yote aliyokabidhiwa na SAF ni yamifumo hiyo 2.
    Pia Felain kasajiliwa kucheza no 10 nyuma ya van Persie ili 4 4 2 na 4 5 1 iende vizuri.

    ReplyDelete
  6. namtazama kagawa kama ndo mtu anayestaili kucheza mbele ya carrick na fellain na si giggs ambaye amekuwa very slow nakupoza mipira mechi zote za man kuanzia ile ya swansea nadhan mmeona ni jinsi gan man wamekua wakiangaika ktk pass za mwisho nakumuacha van persie akiwa hana la kufanya namtaka sana kagawa pale ktk na ndiye pekee ambaye anaweza kuziba pengo hilo

    ReplyDelete
  7. Ngoja nikajaribuu kwenye play station nione kama itakuwaa poaaa. Pes

    ReplyDelete
  8. Ngoja nikaujaribu kwenye Play station

    ReplyDelete
  9. KWELI KAKA APO INGEKUWA POUWA KWELI YANI

    ReplyDelete
  10. Mhh unajua hizi timu kubwa nyingi zina traditional "futbol" kwa maana ya mfumo. Ndiyo maana unakuta sio kila timu inaweza kucheza kama barcelona au Arsenal, kwa mfano tu.

    Mashetani wekundu ni watu wa mpira wa kasi, hasa wakiwa nyumbani na ugenini sifa kubwa ni counter attacks.

    Mfumo huo either 433 au modified 451 (4321) inategemea sana aina za wachezaji. ManU kwa sasa huu mfumo hata wakati wa SAF ulitusumbua sababu ya aina ya midfield players tulionao. barca ni wazuri sana kwa sababu ya mastaa wa dunia ktk dimba, Iniesta na Xavi.

    Manu haiwezi kucheza bila mawinga...na tumeona mara nyingi Wazza, Welbeck sio mawinga.

    Kagawa ni mzuri lakini ni slow na wakati mwingine anapunguza kasi au kuchelewesha counter attacks na hawezi kucheza na timu zilizo physical.

    Mnaolaumu mawinga sasa, ni mapema mno na mnashau Nani hakuwa hata ktk pre season tours kutokana na majeruhi (ingawa huyu ni pasua kichwa na Nani atabaki kuwa Nani- lazima audhi kila mechi..). Young pia amekuwa majeruhi sana lkn akipata mechi zaidi cross zake ni bomba sana. Kinachoudhi (hata goli la juzi ni yeye aliyesababisha) ni ile kurudisha -rudisha mipira nyuma pasipo sababu- alisababisha kona iliyozaa goli...!! Valencia anasaidia sana kukaba kuliko mawinga wote na sijui kwa nini kiwango chake kinapanda na kushuka (sijui tangu avunjike au..). Napenda sana direct attacks zake...anamfuata beki na kujaribu kumpita ila hapigi cross chap chap na hivyo kusababisha beki kujipanga mapema at times..! Winga mzuri anapata mpira, anachungulia strickers wake na anatumbukiza majaro...kukimbia ktk chaki ni pale inapobidi, na if so lazima cross aitoe nje ya boksi kidogo ili wanaokuja mbio-hasa attacking midfielder wakutane nazo. Hapa ndiyo watu hawajui lkn Felaini atasaidia sana..

    So timu kwa nyuma sawa kabisa, ila winger kushoto Zaha, Kulia Valencia au Kushoto Young kwanza na kulia Valencia hasa kwa game kama za Arsenal au Liverpool ambao wana kasi sana..!

    Ili mradi anabaki, mbele anaweza kuanza RVP na Waza au Welbeck.

    ReplyDelete
  11. cyo mbaya ila tatizo linakuja pale 2takapo shambuliwa na wapinzani kwa ku2mia attack/long pass wakati cc tutakapokuwa ndani ya 18 ya lango la mpinzani kwa mchakato wa kutafuta goli nahic itakuwa na madhara na muono wangu mm iwe.......
    nafac ya RIO achezeshwe VIDIC na nafac ya VIDIC awepo JONES... RIO hayupo na kasi tena haswa kwa fomesheni hiyo nahic ataathir tim bora apewe nafac JONES nahic yupo mwepes zaidi...............
    ni mtazamo wangu 2 lkn

    ReplyDelete
  12. hizo comment zinawafikia wahusika??

    ReplyDelete
  13. Mimi nadhani mpango wako hapo juu ni mzuri sana, ni kama vile upo kichwani mwa Mo yes. Lakini uelewe kocha huyu atafanya yale tunayotarajia pale tu atakapo fungwa na kuchangayikiwa na kuacha kuogopa lawama za wachezaji wenye ukubwa wa majina na ukubwa wa man utd. Atakapo fikia hatua hii na naamini si mda mrefu mambo yatakua kama tunavyotarajia.Mda mwingi tuliona SAF maamuzi yake na matokea yalionesha hakuna wa kumhofia kama unamipngo yako na hasa itokea ndivyo c vyo, ni yeye tu wa kutoa majibu na kujua mashabiki tunataka nini.Tuache hayo MO yes c mbaya sote tunajua na anajua analofanya na timu yetu ataipanga vzuri na son tutatisha sana tu.

    ReplyDelete