Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga ambaye alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Malawi Tom Saintfiet amejiuzulu kuifundisha timu hiyo ya taifa kufuatia kipigo cha 2-0 dhidi ya Nigeria jana jumamosi.
Kufuatia kipigo hicho matumaini ya nchi hiyo ya Malawi kwenda kucheza katika fainali za kombe la dunia yamefutika kabisa, kitu kilichompelekea Sainfiet kujiuzulu.
Kocha huyo ambaye alikuja kuifundisha klabu ya Yanga na kuipa ubingwa wa CECAFA kabla ya kuondoka baada ya kutofautiana na uongozi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba hana mpango wa kuendelea kuifundisha Malawi kwa sababu aliajiriwa kwa muda mfupi tu na jukumu lake lilikuwa ni kuiwezesha nchi hiyo kuifunga na Nigeria na kusonga mbele kwenda kwenye play off ya kucheza Wolrd Cup.
"Nilikuwa kwa sababu moja tu kushinda mechi hii dhidi ya Nigeria na hilo ndilo lilikuwa jukumu langu namba moja," alisema.

No comments:
Post a Comment