Kiungo
wa Simba, Jonas Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars
kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia
itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemuongeza mchezaji huyo ili
kuimarisha sehemu ya kiungo. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu kwenye hoteli
ya Accomondia jijini Dar es Salaam.
Timu
hiyo imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
wakati kesho Jumatatu (Septemba 2 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
timu ya kuunga unga c angeamua moja tu achukue vijana wote ili wakapate uzoefu...?
ReplyDelete