Cesc Fabregas amekiri kwamba asingeweza kujiunga na Manchester United wakati huu wa dirisha la usajili hata kama David Moyes
angemuongeza mshahara mara 3 wa anaopata sasa hivi ndani ya FC Barcelona.
United
walikuwa wakimtaka kwa udi na uvumba nahodha huyu wa zamani wa Arsenal kwa kipindi kirefu cha msimu wa usajili huku ofa zao za £30million na £35m zikikataliwa.
Lakini Fabregas anasisitiza kwamba ahkutaka kabisa kuondoka nchini katika klabu yake ya utotoni.
Fabregas aliiambia The Sun: 'Ninsingeweza kuhama kwa fedha mara mbili au tatu ya mshahara wangu wa sasa.
'Nimelipa fedha zangu mwenye kuweza kucheza Barcelona. Nilikuwa nalipwa vizuri nikiwa Arsenal zaidi ya hapa. Kuna ndoto na hii ilikuwa ndio ya kwangu.
'United
hawakuwahi kuongea nami. Klabu inapokutaka kawaida huongea na klabu na sio lazima iongee na mchezaji husika.
No comments:
Post a Comment