Search This Blog

Tuesday, August 20, 2013

SIRI ZA MKATABA WA MRISHO NGASSA NA KLABU YA SIMBA SC

WAKATI Mrisho Ngassa amepitishwa kuichezea Yanga msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, imedhihirika kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliupokea mkataba wa Simba tangu Desemba 17, mwaka jana.
Mwanaspoti limeuona mkataba wa Simba na Ngassa, ambao umegongwa muhuri wa TFF kuonyesha kuwa ulipokelewa katika shirikisho hilo tangu Desemba 17 mwaka jana.
Mkataba huo, unaonyesha kuwa Ngassa alisaini kuichezea Simba Agosti 2, mwaka jana na kwamba ulitakiwa uanze kutumika Mei 22 mwaka huu na kumalizika Mei 31 mwakani.
Katika moja ya makubaliano kwenye mkataba huo, Ngassa haruhusiwi kuichezea Yanga katika kipindi hicho au timu nyingine yoyote na mshahara wake ungekuwa Sh2 milioni kwa mwezi.
Hata hivyo katika kikao chake cha mwishoni mwa wiki, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Soka (TFF), chini ya Alex Mgongolowa ilimuidhinisha Ngassa kuchezea Yanga, lakini ikamfungia mechi sita pamoja na kumtaka arejeshe Sh30 milioni ambazo alichukua Simba pamoja na asilimia hamsini ya fidia ambazo ni Sh15 milioni.
Kamati hiyo ilibaini kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) na anatakiwa kurejesha fedha alizopokea Msimbazi Sh30 milioni pamoja na fidia ya asilimia 50 (Sh15 milioni) ya fedha hizo hivyo kufanya awe anadaiwa Sh 45 milioni.
Kamati hiyo pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii Jumamosi iliyopita), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.
Hiyo ina maana kuwa Ngassa amekosa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam na nyingine tano za Ligi Kuu Bara ambazo ni dhidi ya Ashanti, Coastal Union, Mbeya City, Prisons na Azam.
Kwa mara ya kwanza, Ngassa ataonekana katika Ligi Kuu Bara, Yanga itakapocheza dhidi ya Ruvu Shooting Septemba 28 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

SOURCE: MWANASPOTI

4 comments:

  1. Nimesoma mkataba wa ngasa na samba ila nina maswali mengi sana ambayo sijapata majibu. Tarehe ya mkataba n muda ambao kwa sharia za tff timu hairuhusiwi kuongea na mchezaji mambo ya usajili, yaani Mei sasa tff walipokeaje mkataba mwezi wa 12 wa tarehe ya nyuma, vipi walikuwa wameingia makubaliano miaka mitano iliyopita, pili, mkataba unaonyesha analipwa milioni 20, na umi atapewa kabla ya msimu wa 2013/14 kuanza, sasa mboa wanamdai 30? tatu kwenye mkataba inaonyesha ataanza kutumikia mwaka mmoja baada ya mkataba wa mkopo wa azam na kuna kipengele kinasema hatachezea Yanga katika kipindi hicho cha mkataba sasa kama ana mkataba na Simba angechezeaje Yanga na je ndio aina ya mikataba ya tff ikiwa na vipengele hivyo? nne, waliosaini ni ngasa na viongozi wakuu wa Simba sasa kwa nini Ngasa apewe adhabu peke yake, haki iko wapi hapa? Shaffii mambo mengi unayatolea mijadala sana lakini uko kimya sana kwani halikugusi? unajua nyie ni muhimu hamtakiwi kuwa bias

    ReplyDelete
  2. ASANTE NDUGU MCHAMBUZI..NIMUONA MKATABA KWENYE GAZETI LA MWANA SPORT......NILIYOYAONA:
    1. MKATABA ULISAINIWA TAREHE 2 AUGUST 2012 JE MKATABA WA NGASA NA AZAM ULIKUWA UNAISHA LINI...?
    SHERIA INASEMA MCHEZAJI ANAWEZA KUINGIA MKATBA NA TIMU NYINGINE AU KUFANYA MAONGEZI NA TIMU NYINGINE PALE MKATABA WAKE UKIKARIBIA MIEZI 6 KWISHA...?

    2. WAKATI WA KUSAINI NA JINSI INAVYOONEKANA KULIKUWA NA VIONGOZI WA SIMBA PEKEE PAMOJA NA MWANASHERIA WAO JE NGSASA LAIWAKILISHWA NA NANI...? HUYO MWANASHERIA NI WA SIMBA JE HAPO HAKUKUWA NA MAZINGIRA YA KUMSHURUTISHA MCHEZAJI...?

    3. KIPENGELE CHA 11 KAMA SIKOSEI KINA MKATAZA NGASA KUINGIA MKATABA NA TIMU NYINGINE YOYOTE JE SIMBA WALIFANYA HIVYOA KAMA NANI WAKATI MCEZAJI ALIKUWA NI MALI YA AZAMU...?

    4. KAMA SIJAKOSEA MKATBA UNA TAREHE MBILI TOFAUTI SIJAJUA KISHERIA HAPO INAKAAJE.... (THIS CONTRACT IS MADE THIS 2nd DAY OF August 2012 LAKINI SEHEMU YA KUSAINI NGASA IMEANDIKWA TAREHE 8 MWEZI August 2012 IMAKAAJE)

    5. NARUDIA TENA WITNESS WA NGASA ALIKUWA NI NANI...? HAPO NGASA ANAWEZA KUWAKANA SIMBA MCHANA KWEUPE KAMA KWELI ALISAINI MKATABA.....NIONAVYO KUTOKANA NA MAKOSA HAYO MACHACHE

    6. KIUJUMLA MIMI SIYO MWANASHERIA LAKINI NAONA KUNA MAPUNGUFU MENGI YA KISHERIA AMBAYO HAYAMTII NGASA HATIANI..NA KAMA NGASA YUKO HATIANI HAKUNA NJIA SIMBA PIA WAKAWA HATINANI KWA KUINGIA MKATABA NA MCHEZAJI AMBAYE YUKO CHINI YA AZAM....

    7. NAOMBA KUREKEBISHWA KWA HILI MIEZI SITA IKIBAKI MCHEZAJI ANARUHUSIWA KUJISAJILI AU KUFANYA MAONGEZI PEKEE NA TIMU NYINGINE...?

    8. SEHEMU YA 5 NIKIISOMA VIZURI NI KAMA NGASA ALIPOKEA AU ALITAKIWA KUPOKEA MIL. 20 PEKEE NA 10 ILIYOBAKI ANGEPEWA MWEZI MAY AMBAO ALIINGIA MKATABA NA YANGA....

    9. MKATABA WA KUPENANA VEROSA UKJO WAPI....?

    10. JE MKATABA WA KUPEANA HELA INAMAANISHA MCHEZAJI ALIPEWA HELA.....?

    11. MCHEZAJI ALIPEWA HELA KWA NJIA GANI....HUNDI AU TASLIMU...?

    12. WAKATI ANAPOKEA ALIPEWA DOCUMENT YOYOTE KUISAINI...?

    KAMATI YA TFF NAWASHAURI PITIENI UPYA HAYO...NA PIA NGASA NILIYOKUPA HAPO JUU NI BAADHI TU YA MSUKUMO WAKO KUKATA RUFAA HAPO NIONAVYO MIMI HATA WAKIJA FIFA NGASA ATAKUWA WA YANGA....!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeangalia upande wa mchezaji na maslahi yake,lakin makosa aliyofanya mchezaji huyaoni,msipende kutetea watu wajinga waacheni makosa yao yawaangamize

      Delete