Search This Blog

Thursday, August 8, 2013

RAISI WA REAL MADRID: " £100 MILLION KWA AJILI YA KUMSAINI GARETH BALE NI FEDHA NYINGI SANA"

Raisi wa Real Madrid Florentino Perez ameonyesha wazi kutokubaliana na dau wanalolitaka Tottenham kwa ajili ya Gareth Bale, akisema ada ya uhamisho wanayotaka Spurs ni nyingi sana kwa thamani halisi ya Bale.

Mwenyekiti wa Daniel Levy alifanya mazungumzo na Raisi wa Madrid huko Florida wiki hii, huku klabu ya kaskazini mwa London akisemekana  kuihitaji £100 million kwa ajili ya kumuuza mshindi wa tuzo za PFA na FWA Player of the Year.


Lakini Perez amezungumza na kutoa maelezo yanayoonyesha dili la uhamisho wa Bale lipo mbali na kukamilika, na ameshangazwa sana na ada ya uhamisho wanayotaka Tottenham kwa winga huyo mwenye miaka 24.

Katika mahojiano na kituo cha ESPN, Perez alisema : "Tumeongea na watu wengi sana na ngoja tusubiri tuone nini kitatokea katika mazungumzo yetu - na huyu mchezaji [Bale] na wengineo.

"Hatuzungumzii kuhusu wachezaji wengine kwa heshima ya mchezaji, klabu na Raisi wa klabu bwana Levy, ambaye ni rafiki yangu wa dhati, ambaye nimejenga nae mahusiano mazuri tangu msimu uliopita wakati tulipomnunua Luka Modric.

"Kama sitaki kutaja majina, pia siwezi kutaja kuhusu kiasi cha pesa...... ikiwa unasema 100 million, basi hizo ni fedha nyingi sana kwa kitu chochote sio mchezaji husika tu - lakini kwa heshima niliyonayo kwa klabu ya Totenham sitotaka kuendelea kulizungumzia suala hili...."

No comments:

Post a Comment