Search This Blog

Tuesday, August 13, 2013

PATRICK KAHEMELE - WEWE NDIO KANJANJA NA MNAFIKI MKUBWA.

Mapema leo asubuhi mtandao huu uliandika habari kwamba raisi wa shirikisho la soka nchini Leodegar Tenga ameiomba kamati ya ligi kumpa maelezo ya namna mchakato wa kuipa haki za matangazo ya Televisheni kampuni ya Azam Media ulivyofanyika kupitia barua iliyoandikiwa klabu ya Yanga na katibu mkuu wa TFF bwana Angetileh Oseah.
Baada ya habari hiyo kutoka aliyekuwa meneja wa Azam FC ndugu Patrick Kahemele akiwa anachangia katika moja ya mijadala ya soka katika group la LIGI KUU TANZANIA katika mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kujua au kutokujua aliamua kuuushambulia mtandao huu kwa kuuita wa 'kikanjanja' kwa kutoa habari inayohusu Tenga kuiagiza kamati ya ligi kutoa maelezo ya namna mchakato mzima wa  Azam TV ilivyoweza kupata tenda ya kuonyesha ligi kuu ya Vodacom.

Sasa baada ya tuhuma zake dhidi ya mtandao huu - tumeonelea tumwekee bwana Kahemele chanzo chetu cha 'Kikanjanja' ili aweze kujiridhisha na hiyo taarifa.

HII NDIO BARUA WALIYOANDIKIWA YANGA NA TFF. 
PATRICK KAHEMELE
Ndugu yetu Patrick Kahemele kwa taarifa yako sisi hatupo kwa ajili ya kupigizana makelele na watu kama wewe kwenye mitandao ya kijamii,lengo letu si kumpendelea au kumkandamiza mtu fulani. NA WEWE NDO TATIZO KUBWA LA HII ISHU NA NDIO MAANA KUTWA UNAKESHA UKIWAPIGIA WATU SIMU KUTAFUTA PUBLIC SYMPATHY.Sisi kama vijana wenzako tunakushauri uachane na hizi siasa za mpira.
Kwenye timu ya Azam Fc 'umekichafua' kutokana na tabia zako za kujiona muda wote wewe ndio upo sahihi na unachokiamini ni lazima kiwe matokeo yake wamekuweka pembeni, sasa umeamia kwenye hili la haki za matangazo ya Televisheni.
Sisi hatuna hofu na uwezo wa Azam Media kiutendaji na hatupingi wao kupata hiyo Tender, kilio chetu na wadau wengine ni 
NAMNA MCHAKATO ULIVYOENDESHWA!
wewe ukiwa kijana tena msomi tunakusihi utulizane na uacha kuhangaika sana kutafuta CHEAP POPULARITY.

Mara hii umeshasahau ya kwamba ulikuwa mstari wa mbele kupinga mambo yanayofanyika ndivyo sivyo kwenye tasnia ya mpira wa nchi yetu?Tena ulifika mpaka hatua ya kupigana ngumi na baadhi ya viongozi wa TFF ? nini kimekubadilisha mtazamo wako tena ghafla ndugu yetu.
   '' True Popularity comes from acts of Kindness rather acts of stupidity '' Bob Bennett

TUNAMALIZA HIVI:

 KWA TAARIFA YAKO SISI KAMA shaffihdauda.com AZAM NI WADAU WETU WAKUBWA NA NI MARAFIKI PIA,KWAIYO USIDHANI HIZO CHUKI ZAKO UNAZOZIPANDIKIZA KWAO ZITAKUSAIDIA KWENYE HARAKATI ZAKO. 


12 comments:

  1. Mmh hapa kwel kazi ipo!

    ReplyDelete
  2. KUNA VIJANA WANAPENDA SANA UMAARUFU MJINI.
    YANGA WANA HAKI YA KUDAI WANACHODAI

    ReplyDelete
  3. Yanini marumbano yanini maneno kunapasenti nini daaaaaah

    ReplyDelete
  4. wengine ni bora viongozi kaka Shaffih wasikuumize kichwa.

    ReplyDelete
  5. hapa hela imetembea ila mgao ndio watu wamedhulumiana!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. I always like this blog and you shaffih coz hougopi kusema ukweli. Wachane live hao

    ReplyDelete
  7. msijibizane nao andika mnachokiamini kuwa ni kweli ..si kila mnaloandika linamfurahisha kila mtu...wakati mwingine mnagusa masilahi ya watu..ndo uandishi wa habari huo..songa mbele hata kama mtu akiponda ukweli siku zote utasimama..keep it up!

    ReplyDelete
  8. Huyo Kahemele ni @~>.'<. sana sio mara ya kwanza anaposhambuliwa kwa hoja hukimbilia kumshambulia mtu. Sijui ndo usom wa wapi huu,!!! Anaidhalilisha Club ambayo inakuja na mfumo wa kisasa hasa kwenye uendeshaji lakini yeye bado anaakili za Kijima na Haya ndo matokeo ya kusoma kwa kudesa, ...Wanaenda shule lakini hawaelimiki.Kweli kuna kila haja ya kubadili mfumo wetu wa Elimu.

    ReplyDelete
  9. Ha ha ha ha ha ha ha ha! Mara zote kila biashara ila dalali sasa bwana Kahemele Yanga wamemgeuzia dili kuwa dirisha anahaha. Waitumie hiyohiyo blog ya mfadhiliwa wao anaedai hata kuandika hatujui halafu tunapinga mkataba! Yanga imara, mbele daima nyuma mwiko. Mkumbuke hata mpotoshe vp huu mcmamo wa viongozi wetu, cc bado tunaona mkataba ni wakikanjanja na hata tv yenyewe hamna!

    ReplyDelete
  10. dauda .com unanikumbusha mbali mno, ukisema ukweli lazima uchukiwe,muulize Roma.,jifanye na ww umechinjiwa ng'ombe ukanyweshwa damu uje town utete wanyonge,keep it up!

    ReplyDelete
  11. Hahaahaa... Tanzania bwana mipasho hadi kwenye sports......

    ReplyDelete
  12. kaka Shafii usiumizwe kichwa na watu kama hao huwa wana tabia za kike kila kukicha wao kujipendekeza

    ReplyDelete