Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti
30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni
(exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL).
Mkataba
huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa
kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman
Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam
Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.
Ligi
Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder)
cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo
zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.
Makamu
wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa
pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao
wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.
MMmm Yanga vipi jama!!wataonekana kwenye kioo au msimamo palepale?mtujuze jamani tulioko namtumbo,nanjilinji,kwangulelo, etc.
ReplyDeletehawataonekana watapatikana zuku
ReplyDelete