Dirisha la usajili la barani ulaya linakaribia kufungwa mnamo September 2 mwaka huu. Timu kadhaa zimeshafanya usajili wa kuiimarisha vikosi vyao. Wachezaji wengi wameshahama kutoka kutoka timu moja mpaka nyingine. Lakini katika siku za hivi karibuni baada ya issue ya Gareth Bale kupoa - Luis Suarez na Wayne Rooney sasa ndio wanaongoza kutokea kwenye vichwa vya habari vya vyombo habari ulimwenguni.
Wayne Rooney anadaiwa kutaka kuondoka Manchester United na kujiunga na Chelsea ambao wameshatuma ofa mbili zilizokataliwa na United, lakini kocha Jose Mourinho amekaririwa akisema kwamba hatokata tamaa ya kumsajili mshambuliaji huyo mpaka siku ya mwisho ya usajili barani ulaya.
Luis Suarez yeye tofauti na Rooney - ameshathibitisha waziwazi kwamba anataka kuondoka Liverpool. Arsenal wameshatuma ofa ya £40m lakini Liverpool wameikataa kabisa huku wakisisitiza kwamba hauzwi. Kocha pamoja na mmiliki wa klabu hiyo wakisema Suarez hatoruhusiwa kuhama wakati huu kwa sababu bado wanamhitaji na hata kama wakimuuza watakosa mbadala wake hivyo kuidhoofisha timu yao. Kwa maana hiyo hawawezi kumuuza kwa bei yoyote.
Mjadala: Je Rooney na Suarez wataendelea kuvichezea vilabu vyao vya sasa au wataenda kujiunga na mahasimu wa vilabu?
Je ni Chelsea ni timu sahihi kwa Rooney? Au Rooney ataifaa Chelsea?
Luis Suarez anafanya uamuzi sahihi wa kutaka kuondoka Liverpool na kujiunga na Arsenal na je atasaidia?
JADILI KWA KUTOA MAONI YAKO
hayo hayatuhu sisi tunawaza azam tv watuletee king'amuz
ReplyDeletemimi nafikiria rooney kwennda chelsea kwasasa si ahihi kwani vain magori kashasema yeye kwenda OT nikumfuata rooney
ReplyDeleteWatabaki na timu zao kwa7bu n wachezaj wanaotegemewa xana...suarez akbk liver nahc watashrk uefa msimu ujao
ReplyDeleteLuis akitaka kuwa mchezaji bora zaidi....aobdoke aende timu yyte yenye kiwango cha juu
ReplyDeleteChelsea ni mahala sahihi kwa Wayne Rooney bt kwa Luis Suarez ni tofauti sana kwa sababu kuhama liverpool fc na kwenda Arsenal fc ni sawa na kuruka mkojo na kukanyaga mavi ucl hawapo next season
ReplyDeletemorinho lengo lake c kwamba rooney n chaguo lake namba moja bali anataka kuichanganya man u coz rooney ameonekana n kipenzi cha wana man u
ReplyDeleteKama suarez atapeleka transfer request and then kuripoti kwa pl, naimani liverpool watakuwa hawana tena haja ya kumng'ang'ania coz atadhihirisha 100% kuwa hana mpango nao tena. Xo arsenal watalamba dume.
ReplyDeleteRooney akijaribu kufikiri future ya UTD anaona kuna tatizo na kiukweli kabisa Wazza akiruhusiwa kujiunga na Chelsea atafanya makubwa maana is a kind of hard worker anayehitajika pale darajani
ReplyDeleteKila mtu aachiwe aende timu anayotaka, kumlazimisha mchezaji abaki cyo uungwana.
ReplyDeleteRooney anataka timu mbadala ili apate namba ya kucheza wakati Suarez anataka timu iayoshiriki CL, so timu zinazowamiliki ziwackie maana wakibaki hawatacheza kwa moyo.
ReplyDeleteMi ni shabiki wa man u lkn kwahili naungana na wewe kwa 100%
ReplyDeletena waende tu kwani wao kina nani? waking'ang'aniwa wataleta pozi
ReplyDeletesuarez kuhama kwenda arsenal ni ngumu,kwa msimu huu na hata kama akihama hataenda kuongeza chochote arsanal
ReplyDeleteMaamuzi ya mwisho yatabaki ktk vilabu wanavyochezea !!!
ReplyDeleteRooney aendi kkote,
ReplyDelete