Search This Blog
Monday, August 5, 2013
MICHEAL WAMBURA: NAUNGA MKONO HATUA YA MSAJILI KUIKATAA KATIBA YA MAGUMASHI YA TFF
YAH:SABABU ZA KUUNGA MKONO UAMUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO NA VILABU KUKATAA KUSAJILI MAREKEBISHO YA KATIBA YA TFF KUTOKANA UKIUKWAJI WA UTARATIBU NA SHERIA ZA MAREKEBISHO YA KATIBA TFF 2013
Katiba ya TFF ya 2012 ilifutwa na msajIli wa vyama vya michezo na vilabu kwa kuwa ilibadilishwa kinyume cha sheria(BMT) pamoja na Katiba ya TFF ibara ya 30 kwa kutumia njia ya waraka badala ya Mkutano Mkuu, hivyo katiba halali kisheria inayotambulika ni ile ya 2006 na mabadiliko yake . FIFA na Serekali kupitia wizara yenye dhamana na michezo iliiagiza TFF iitishe Mkutano Mkuu ili ifanye mabadiliko ya katiba stahiki kwa mujibu wa katiba na kwa kufuata taratibu zilivyoainishwa kwenye katiba ya TFF. Nimelazimika kuendelea kuiunga mkono Serikali kupitia msajili kwa maamuzi yake ya kukataa kusajili mabadiliko ya katiba ya TFF kwa kuwa TFF kwa makusudi imeendelea kuvunja katiba yake katika kufanya mabadiliko.
Kisheria msajili husajili mabadiliko yoyote ya Chama kilichosajiliwa chini ya Sheria ya BMT kwa kuzingatia Sheria NA 12 ya 1967 na marekebisho yake NA 6 ya 1971 ya Baraza la Taifa la Michezo pamoja na Kanuni za Baraza la Michezo la Taifa na Kanuni za Usajili NA 422 za1999.
Chama chochote kitakacho kwenda kinyume na sheria hizo hikiwezi kupewa usajili au Katiba yake na marekebisho yake hayawezi kupewa usajili,aidha uamuzi wa msajili sio tu utaifanya TFF peke yake itambue sheria bali hata vyama vingine vitawajibika kufuata utaratibu katika kufanya mabadiliko ya katiba zao,
Katiba ni nyaraka ya kisheria hivyo chombo chenye mamlaka kisheria hapa Tanzania ya kutafsiri katiba ni Mahakama pale pande mbili zinapotofautiana juu ya tafssiri ya Katiba, hivyo kwa kufanya hivyo msajili atakuwa ameepusha suala la Katiba ya TFF kuingia katika mikono ya kimahakama kwa kuwa utaratibu uliotumika kubadili katiba ya TFF ni dhahiri haukufuata taratibu zilizoainishwa kwenye katiba ya TFF na sheria na za nchi kama zilivyoaanishwa. Sababu kuu zinazonipelekea mimi kuunga mkono uamuzi huo ni kama zifuatazo:
1. UPIGAJI KURA MAREKEBISHO YA KTIBA
Ibara ya 30(4) ya katiba ya TFF 2006 inaelekeza ya kuwa mapendekezo ya mabadiliko ya katiba ya yatapitishwa ikiwa yataridhiwa na wajumbe theluthi mbili(2/3) ya wajumbe wenye haki ya kupiga kura.
· Ibara ya 28(4) maamuzi yote ya mkutano mkuu yatafanywa kwa kuzingatia uwingi wa kura halali zitakazopigwa na wajumbe halali wa Mkutano Mkuu labda ikiwa katiba ya TFF inaelekeza vinginevyo. “ Unless otherwise stipulated in the statutes the decisions of the general assembly shall be taken by simple majority of the votes validly cast by the official delegates”.
· Ibara 28(5) ya katiba ya TFF(MAAMUZ)
Inazungumzia Maamuzi yanayohusiana na mabadiliko yoyote ya makao makuu ya TFF, mabadiliko yoyote ya Katiba na Kanuni zake, marekebisho yoyote ya ajenda kwenye mkutano mkuu wa kawaida, maamuz iyoyote yanayohusiana na kusimamishwa au kufukuzwa mjumbe wa vyombo vya TFF au inayohusiana na kuvuliwa hadhi ya Urais wa heshima au mwanachama wa TFF au inayohusiana na kutengwa kwa mwanachama au kuvunjika kwa TFF lazima itahitaji zaidi ya 2/3 ya kura halali zililizopigwa na wajumbe resmi wa Mkutano Mku “ Decision relating to any change of head office of TFF ,any amendments of Statutes and regulations, any modification to the agenda of the ordinary general assembly, any decision relating to suspension or dismissal of member a member of an organ of TFF or relating to bestowing of the title of honorary president or member of the TFF or relating to the exclusion of a member of TFF or dissolution of TFF shall require a majority of 2/3 of the votes validly cast by the official delegates”.
Kwa kuwa hakuna kura zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kuhesabiwa kuamua ama kupitisha au kukataa mabadiliko basi zoezi hilo na marekebisho hayo ni batili kwa mujibu wa Katiba ya TFF.
2. MKUTANO MKUU WA DHARURA
Ibara ya 25(4) katiba ya TFF ya 2006 inaelekeza kuwa Agenda na makabrasha ya Mkutano Mkuu ni lazima yawafikie wajumbe wa mkutano mkuu walau siku 15 kabla ya mkutano Mkuu.
Kwa kuwa wajumbe walipewa agenda na makabrasha siku moja kabla ya Mkutano Mkuu, huo ulikuwa uvunjaji mkubwa wa Katiba ya TFF , wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF hawajiwakilishi wao bali wana wakilisha Mikoa, Vyama shirikishi na Vilabu ambavyo vina wanachama wake na kamati zake za utendaji ambazo zilikuwa na haki ya kujadili na kuwapa wawakilishi wao mawazo yao kwani maamuzi ya ya TFF yanagusa kuanzia ngazi ya Taifa mpaka wilaya.
3. KUINGIZA VIFUNGU KWENYE KATIBA BILA KUJADILIWA NA KUPITISHWA NA MKUTNO MKUU WA TFF
Kwa kuwa marekebisho ya katiba kwa kutumia waraka ya 2012 yaliyowasilishwa kwa msajili, usajili wake ulifutwa hiyo maraekebisho yote yaliyofanyika wakati huo ikiwa ni pamoja ibara Ibara 52 (1(b),2,3,4,5,6(a,b) yanayohusu Kamati ya Uchaguzi na kamati ya Rufaa ya Uchaguzi iliyopelekea Uteuzi wa Mtinginjola na kamati yake , pamoja na Ibara ya 64(1,2) ya leseni za vilabu yanakuwa batili, hivyo kama TFF ilikuwa bado inapenda vifungu hivyo viwemo kwenye marekebesho ya katiba ya 2013, basi njia sahihi ilikuwa ni kuwasilisha maombi kwenye mkutano Mkuu wa TFF 13/7/2013 kwa mujibu wa Katiba ya TFF ibara 30 (2006).
Kwakuwa TFF haikupeleka maombi ya mabadiliko haya na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF 2013 hivyo kuyaingiza kwenye katiba ya sasa ya 2013 na kuyaombea usajili kwa msajili ni kinyume na sheria na Katiba ya TFF, tafsiri rahisi ni kuwa TFF ilitaka kuonyesha kwa Umma wa Watanzania ya kuwa serekali kupita msajili wa vyama vya michezo haikuifuta na haikuwa na mamlaka ya kuifuta katiba ya Tff na mabadiliko yake ya Desemba 2012.
4. UUNDWAJI WA KAMATI KABLA YA MAREKEBISHO YA KATIBA KUSAJILIWA.
TFF iliamua kuunda kamati zake hata kabla katiba haijasajiliwa na Msajili wa vyama vya michezo na vilabu, hii naonyesha jinsi ambavyo mfumo mbovu ulivyozoeleka huko nyuma ambapo msajili alikuwa akisajili katiba bila kuzingatia mapungufu hivyo kufanya vyama vya michezo kuwa kama mali za watu binafsi na hata wakati mwingine kumuona msajili kama sehemu ya vyama vyao jambo ambalo Wizara imeamua kulifuta na kuhakikisha taratibu zinafuatwa.
Kwa mujibu wa katiba ya TFF ibara ya37(3)i (2006) Rais wa TFF anayo mamalaka ya kupendekeza kwa kamati ya Utendaji majina ya wajumbe wa vyombo vya TFF(TFF Organs) zilizoko kwenye katiba ya TFF ibara ya 44(a,b)(kamati ya nidhamu na Rufaa),ibara 48(mahakama ya usuluhishi,49(Kamati ya Uchaguzi), pamoja na kamati ndogo ndogo (standing Committees) zilizoainishwa kwenye Ibara ya 39(1)a-i, isipokuwa hana mamlaka ya kuteua wajumbe wa kamati za vyombo ya TFFambavyo havimo kwenye katiba ya TFF (2006) kama kamati ya Rufaa ya Uchaguzi, kamati ya Maadili na Kamati ya Rufaa ya Maadili.
Uteuzi wa Majaji na Wanasheria waandaamizi kuingia kuongoza kamati ambazo zina utatata wa kisheria kumeidhalilisha sana idara ya Mahakama na wanasheria kwa Ujumla hali ambayo huenda kwa siku za usoni Majaji / Mahakimu na wanasheria waandamizi hawataweza kukubali kushirikiana tena na TFF. Hata hivyo uundwaji wa kamati hizi ni dhahiri ulikuwa ni wa hila kwa kuwateua majaji ili ionekana haki ingetendeka huku TFF ikijua wazi maamuzi yao kwa mujibu wa katiba yanazingatia upigaji wa kura zaidi pale pande mbili zinapopingana kwani ukiachila majaji kwenye kamati hizi wajumbe wanaobaki ni wale wale ambao kwa mtindo wa Kura wanakuwa wengi(wengi wape)
TFF inaelekeza kuwasilisha malalamiko ya uchaguzi kwenye vyombo vyake ambavyo ndio hivyo vilivyo haribu mchakato wa Uchaguzi ambao hadi sas haujafanyika.Katika kuonyesha dhamira isiyo nzuri ya kutaka kuwa na uchaguzi usiokuwa huru na wa haki TFF imewateua na kuwabadilisha wajumbe ambao kwa sehemu kubwa walishiriki kuharibu mchakato wa uchaguzi uliopita kwa kuwapa majukumu ambayo kwa njia moja au nyingine bado watashiriki katika mchakato wa uchaguzi unatarajia kufanyika siku za hivi karibuni, mfano ni wajumbe 3 kati ya 5 waliokuwa kwenye kamati ya Rufaa ya chaguzi ya TFF wamehamishiwa kwenye Kamati ya Maadili ya TFF(Francis KebweMohamed Mpinga,madundo Mtambo na mmoja( Murtaza Mangungu Kamati ya Rufaa ya Maadili,aidha wajumbe 4 wa kamati ya Uchaguzi Kati ya 5 wamebakishwa kwenye kamati ilie ile na wawili kati yao wamepandishwa vyeo na kuwa mwenyekiti na Makamu wa Kamati hizo ambao Hamidu Mbwezeleni (mwenyekiti), Moses Kaluwa (m/mwenyekiti), Hassan Dyamwale na Kitwana Manara. Katika shauri lilifunguliwa mahakama kuu M.A. Ndolanga & others v National Sports Council and Other [HCT, 1996, TLR 325,Bubeshi,J.] lililohusu uchaguzi mkuu wa FAT ambalo maamuzi yake hayajawahi kutenguliwa na mahakama nyingine ya juu nchini mpaka sasa, matatizo kama haya yalijitokeza na ambapo mahakama pamoja na hoja nyingine ilitaka kujua:) (i) Kama Kamati ya Usaili ya uchaguzi ya BMT iliundwa kwa kufuata misingi ya sheria? (ii) Kama kamati ya usaili ya Uchaguzi ya BMT ilifanya kazi kwa kuzingatia haki asili za kimsingi (Natural Justice and Fair Play) UAMUZI WA MAHAKAMA ULIMPA USHINDI M.A. NDOLAGA Mahakama iliamua kuwa Vyombo vya maamuzi vya kiutawala wakati wa kutekeleza majukumu yake ambayo yanahitaji kutambuliwa kisheria, vinawajbu wa kutenda kwa kufuata sheria kwa kuzingatia haki za msingi ikwa na maana ya kufuata utaratibu ambao msingi wake utahitaji Uhuru nje ya maslahi na upendeleo kutoka upande wa chombo cha maamuzi kiutawala na haki ya uwazi ya kusikilizwa kwa wale ambao wataathiriwa moja kwa moja na maamuzi. “it is trite to remark that an administrative body exercising functions that impinge directly on legal recognized interests, owes it as a duty to act judicially in accordance with the rule of natural justice which basically means the adoption of procedure, which fundamentally demand freedom from interest and bias on the part of the administrative body and the right to fair hearing for those who are immediately affected by its decision”(pg 333)
Kwa kuwa uundwaji na malengo ya kamati hizi zina walakini kisheria ni wazi uwezekano wa wadau kutafuta msaada wa kisheria mahakamani unaweza kujitokeza kwa kzingatia ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi (Natural Justice) na Katiba ya TFF inavyoelekeza
5. UKOMO WA MADARAKA WA VIONGOZI WA VYAMA
TFF imehusishwa sana na hila na nia ya kuvuruga uchaguzi ili waandelee kuliongoza shirikisho kinyume na katibaTFF Ibara ya 33 ya katiba ya tff inazungumzia Ukomo wa madaraka ni miaka 4 na uongozi wao ulikoma Desemba 2012 hivyo uongozi huu kuendelea kuwepo madarakani na kufanya marekebisho ya katiba ni kinyume na katiba ya TFF na sheria ya BMT ibara 15(1)a. “chama cha mchezo wowote kilichojishirikisha na BMT kitakuwa na wajibu wa kufanya kazi zote za chama kwa msingi wa katiba yake” kwa mujibu wa Katiba ya na kanuni za usajili wa vyama vya michezo kisheria isinge kuwa halali kw a msajili kusajili marekebisho ya Katiba ya TFF kwa kuwa yanapingana na sheria za BMT na Msajili kifungu7(1,2,3,4&5). Vinavyo someka kama ifuatavyo:
· 7(1). “Kipindi cha Uongozi wa Chama chochote kitamalizika mara kipindi cha kufanya uchaguzi mwingine kitakapokuwa kimefika kwa mujibu wa katiba ya chama “ ambapo TFFilikuwa Dec 2012
· 7(3) “Viongozi wanaomaliza muda wao watatakiwa waitisha mkutano mkuu wa Uchaguzi katika Kipindi ha siku 30 kabla ya siku ya ya mwisho ya kipindi cha Uongozi” Jambo ambalo TFF haikulifanya kwa makusudi kwa kingizio cha kupisha mabadiliko ya katiba kwa njia ya waraka ambayo ni kinuyume cha Katiba Ya TFF.
· 7(4). “Endapo siku 30 zitamalizika baada ya kipindi cha uongozi kumalizika bila ya uchaguzi kufanyika ,na bila ridhaa ya wanachama wa chama husika, viongozi wanaomaliza muda wao watahesabika kuwa wamejivua Uongozi” kwa kuwa Uongozi wa TFF haujapata ridhaa ya kuendelea kuongoza TFF kutoka kwa wanachama wake. kisheria hawakuwa na mamalaka ya kufanya na kusimamia mabadiliko ya katiba hivyo msajili kuyakataa ni utekelezaji wa sheria za nchi.
· 7(5). “ Endapo Viongozi wanaomaliza muda wao wamepata ridhaa ya wanachama kuendelea kuongoza baada ya kipindi cha uongozi kumalizika, wanaweza kukiongoza chama husika kwa kipindi kisicho siku 90 tu baada ya siku ya mwisho ya kipindi cha uongozi. Hata hivyo, ridhaa ya wanachama lazima iwe imepatikana kabla yatarehe ya mwisho ya kipindi cha Uongozi”.
Kwa mantiki hii Kamati ya Utendaji ilimalizi muda wake 14/12/2012 na haijaahi kupatiwa ridhaa na wanachama wake na hata kama ingepata ridhaa, ridhaa hiyo ilikuwa na ukomo mwezi wa March 2013 , hivyo kamati hii haikuwapo kihalali wakati wa mchakato wa kubadilisha katiba na hivyo kwenda kinyume kanuni za Usajili wa vyama vya michezo 11(1)d “ mabadiliko hayo hayafai kwa kuwa hayakuzingatia Sera ya Michezo ,Sera ya Utamaduni na sheria ya Baraza la Michezo”
6. HILA ZA KUVURUGA MCHAKATO WA UCHAGUZI
TFF imejiongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya Miezi 7 sio kwa sababu yoyote ya msingi zaidi ya mikakati yenye hila ya kuwaondoa wagombea wasiowahitaji tangu wakati wa kurekebisha katiba kwa njia za hila za waraka ili kuunda kamati zitakazo tekeleza malengo yao na hadi sasa wanaendelea na mkakati huo ili kuidhalilisha serekali kwa kuwa ilionyesha msimomo wake wa kutaka wagombea watendewe haki, swali ni vipi watu walioharibu mchakato wa uchaguzi uliolalamikiwa na Wadau na serekeli wapandishwe vyeo tena washiriki katika mchakato huo huo wa uchaguzi na ni vipi watu ambao hawakuwatendea haki wagombea kwa kuwakata na kuwaondoa kwenye mchakato kwa hila mara ya kwanza watatenda haki tena. Hii ni kinyume na sheria za BMT na kanuni za msajili Kifugu 11(3)b.kwa kuwa nia ya TFF ni kuwanufaisha wachache
Kwa kuwa Marekebisho ya Katiba ya Tff hayakuzingatia katiba ya TFF na sheria za BMT na Kanuni za Msajili wa Vyama ninaunga mkono uamuzi wa Msajili kukataa kusajili mabadiliko haya kwa kuzingatia kanuni za msajili kama ifuatavyo:
· 11(3)a, Mabadiliko hayo yanaweza kuhatarisha usalama na kuvuruga amani miongoni mwa wanachama na jamii kwa ujumla na hivyo kuathiri maeneleo ya chama”.
· 11(1)b, Mabadiliko hayo yanalenga kuwanufaisha wachache”.
· 11(1)d, mabadiliko hayo hayafai kwa kuwa hayakuzingatia Sera ya Michezo ,Sera ya Utamaduni na sheria ya Baraza la Michezo.
USHAURI: 1. Kwa Kamati ya Utendaji chini ya L.C Tenga imemaliza muda wake kisheria na imeshindwa kwa mara nyingine kuandaa katiba ili kuipeleka TFF katiak Uchaguzi ambao utakuwa wa haki na huri ni vizuri na busara inaelekeza kwa Bwn Tenga na kamati yake kawajibika kwa kujiuzulu ili kupisha uundwaji wa kamati ya mpito (normalization Committee) kama ilivyofanyika nchi za Sieraleon, Gambia, Cameroon na Tanzania(2001)ili kuandaa njia huru kuelekea uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya. 2. Kwa kuwa Uongozi uliopa madarakani kwa makusudi umekiuka katiba ya TFF kwa mara ya pili, Msajili atumie kifungu 10(1)a,b (kukiuka katiba ya Chama) za kanuni ya Usajili kuwawajibisha viongozi hawa wa TFF waliomaliza muda wao. Kifungu “10(1).b endapo itabainika kuwa kiongozi au viongozi wnaendesha shughuli za chama bila kufuata katiba iliopo au kukiuka kwa makusudi vifungu vya katiba ya chama,msajili anaweza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja kufutwa uongozi kwa kipindi cha uongozi kilichobaki”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
...kati ya taasisi zinazofanya mambo yake kwa mazoea na hila mojawapo ni TFF...hawawezi kuaminika hata kidogo..
ReplyDelete