Search This Blog

Wednesday, August 14, 2013

MAOFISA WA MAN UNITED NDANI YA JIJI LA MADRID KUFANYA MAZUNGUMZO YA KUMSAJILI LUKA MODRIC


Maofisa wa Manchester United wapo jijini Madrid kuzungumza na klabu ya Real Madrid kuhusu uwezakano wa kumnunua kiungo Luka Modric kwa mujibu wa mtandao wa ESPN.

Kiungo huyo mwenye miaka The 27 alihamia Spain akitokea Tottenham Hotspur kwa ada ya uhamisho wa £33 million lakini amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha Madrid, hata kufikia kupigiwa kura na mashabiki kuwa mchezaji mbovu zaidi kuwahi kusajiliwa na Madrid kwa msimu uliopita - ilikuwa mwezi January.

Alijitahidi na kucheza vizuri hasa kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya zaidi kwenye mchezo wa mtoano dhidi ya Man United katika uwanja wa Old Trafford lakini hatma yake ndani ya Madrid imezidi kuwa shakani baada ya klabu hiyo ya Spain kuongeza viungo watatu baada ya lile lundo la mwanzo - wamemsajili Isco,  Asier Illarramendi na Casemiro.

Modric kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kujiunga na United lakini mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy hakutaka kumuuza mchezaji huyo kwa wapinzani wa ligi ya nyumbani na hivyo akauzwa kwa klabu ya nje ya nchi. Kwa hali ilivyo sasa ndani ya Madrid inaweze kuwa rahisi kwa United kumpata kiungo huyo wa wa Croatia.

2 comments:

  1. Shaffih sikuelewi unaposema modric hana nafasi kwenye kikosi cha Real , huku kwenye preseason ndio moja ya wachezaji walioonyesha kiwango kizuri na kumfurahisha kocha na sijui kama unajua ni mmoja ya wachezaji ambao kocha amesema haondoki , hapohapo ukumbuke kwa Xabi na Illarramendi wapo majeruhi na season inaanza hivyo Je unafikiri Ancelloti na Zidane wataruhusu auzwe kweli ? Soma habari zenye uhakika ili ujue mambo yana endaje sio ushabiki na kufurahisha watu !

    ReplyDelete
  2. man u mnazingua fanyeni kweli kwa Luca

    ReplyDelete