Umbali wa kutoka ulipo uwanja wa Emirates mpaka White Hart Lane ni maili 5 tu, lakini umbali wa mafanikio baina ya Arsenal na Tottenham kwa miongo miwili iliyopita ni kama maili 1000.
The Gunners,
wamemaliza mara 16 mfululizo katika top-four ya premir league na mara moja wakifanikiwa kuweka rekodi ya kumaliza msimu bila kufungwa - mechi 49 kuanzia msimu wa
2003-04 mpaka 04-05. Arsenal wamekuwa ndio vidume wa upande wa kusini mwa London. Wakiwa na uhakika wa kucheza Champions League kwa takribani miongo miwili mfululizo sasa. Lakini katika misimu ya hivi karibuni, Spurs wamekuwa wakileta upinzani, wakimaliza katika nafasi ya nne na tano mfululizo. Msimu uliopita ni pointi moja tu iliwapa Arsenal nafasi ya kwenda ulaya mbele ya Spurs, na mashabiki wa Gunners waliendelea kuwatambia wenzao kwa mara nyingine tena. Lakini imagine kama Spurs wasingewakosa wachezaji muhimu kama Gareth Bale kwenye mechi za mwisho, labda sasa ingekuwa wao ndio wanacheza na Fenerbahce katika play off ya kucheza Champions League.
Arsenal wakiwa wamepata bahati ya kuwapita Spurs na kupata nafasi ya kucheza UCL, kwa hakika wengi tuliamini Wenger na wenzake wangefungua kitabu cha check na kufanya usajili mzuri wa kuimarisha timu lakini mpaka sasa patupu.
Huku zikiwa zimebaki wiki tatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa, Arsenal haijafanya lolote la maana katika usajili, Arsenal haijafanya lolote kujiimarisha wakati Spurs ikiwa inajiimarisha vilivyo ikiwa imetumia zaidi ya paundi milioni 55 katika usajili wa Roberto Soldado, Chadli, Paulinho na Etienne Capoue, wakifukia mashimo katika ambacho tayari kimesheheni kwa ubora. Na kikosi cha Spurs ndio kiliweza kutoka na ushindi wa pointi katika mechi ya ufunguzi, wakati Arsenal wakiumizwa 3-1 na Vill - huku balaa la majeruhi likizidi kuwaandama na pia beki wao tegemeo Laurent Koscielny akiwa amepigwa kadi nyekundu hivyo atakosa baadhi ya mechi.
Wiki moja ndani ya msimu, na Arsenal wapo katika hali mbaya, hii inaweza ikawa ndio nafasi pekee ya Spurs kuweza kuwageuzia kibao ukizingati an usajili wanaofanya -- bila kuzingatia uwepo au kutokuwepo kwa Gareth Bale.
Kwenye karatasi mpaka sasa Arsenal ndio timu yenye kikosi dhaifu katika TOP 6 ya EPL - na wana ratiba ngumu mwanzoni mwa ligi ikizingatiwa wanacheza mechi za play off za Champions League.
Jana wameanza kucheza na Fernebahce, the Jumamosi wanaenda kucheza na timu ambayo imekuwa ikiipa upinzani hivi karibuni Fulham, Jumanne ijayo wanarudiana tena na Fernebahce -baada ya hapo September 1, Arsenal inakutana na wapinzani wa Tottenham, siku moja kabla ya dirisha la usajili kufungwa - mechi ambayo itakuwa vita kubwa baina ya timu hizi mbili.
Ikumbukwe Arsenal wataingia kwenye vita hii wakiwa na kikosi ambacho kinawakosa watu muhimu kwenye timu hiyo walio majeruhi (Laurent Koscielny ametoka kwenye mechi ya jana akiwa ameumia) - Wenger atakuwa kwenye hali ngumu kupata ukuta imara wa kuweza kipa mbovu Wojciech Szczesny.
Huku tetesi za usajili nyingi zikionekana kuegemea kwa Arsenal kutaka kufanya usajili wa washambuliaji - walianza na Rooney, Higuain, Suarez na sasa Karim Benzema - mshambuliaji ambaye akinunuliwa atakuja kusaidiana na Giroud katika kuziba pengo la RobinVan Persie waliyemuuza United, lakini ushambuliaji sio tatizo kubwa kwa Arsenal kwa sababu ni moja ya timu ambayo msimu uliopita ilifunga mabao mengi sana na sasa Giroud akiwa kwenye msimu wake wa pili atakuwa na uwezo wa kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita baada ya kuizoea ligi. Tatizo kuu la Arsenal lipo kwenye ulinzi. Ukianza na golikipa (*Asmir Begovic*,angewafaa sana na ingekuwa rahisi kumnunua kuliko huyo Iker Casillas anayetajwa)
.
Wakati Arsenal wanasuasua kusajili, Spurs jana walikuwa wanakaribia kutumia paundi millioni 60 kwa kiungo Willian na winga Lamela na kuzidi kuimarisha timu yao vizuri. Spurs wana kikosi kilicho na ufundi, wachezaji wenye nguvu kitu ambacho Arsenal wanakosa sana. Kiwango chao kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace hakikutisha sana, lakini kadri muda unavyoenda ndivyo wachezaji wapya watakavyozoena na kuunda timu nzuri yenye kuweza kushindana vizuri.
Na ikiwa, tetesi zilizopo kwamba Gareth Bale atauzwa kwenda Madrid kwa paundi millioni 93 pamoja na Spurs kupewa Fabio Coentrao - ukichanganya na ujio wa Willian na Lamela kwa hakika Arsenal wanaweza wakampisha Spurs kwenye TOP 4.
Kwa namna Spurs walivyofanya usajili - wakifanikiwa kuepeukana na majeruhi na kucheza vizuri basi lazima TOP 4 ya mwakani ibadilike. Wakati Manchester City ilipokuja juu Liverpool waliondoka kwenye TOP 4, na sasa kwa hali nadhani kama Arsenal hawatofanya usajili mzuri katika wiki hizi 3 zilizobakia basi - washika bunduki wa London itabidi waweke silaha chini na kumpisha mpinzani wao Tottenham Hotspur katika nafasi nne za juu mwa ligi kuu ya England.
Kila mwaka mnaongea hivi tumekwishazoea.
ReplyDeletehaujawadia na vitu unaviona mwenye macho aambiwi tizama
Delete