Search This Blog

Saturday, August 10, 2013

MAKALA: CESC FABREGAS NA WACHEZAJI WATANO AMBAO WALIIKATAA MANCHESTER UNITED MSIMU HUU


Cesc Fabregas anakuwa mchezaji mwingine kukataa kujiunga na mabingwa wa ligi kuu ya England jana alhamisi wakati kiungo huyo alipothibitisha kwamba atabaki Barcelona msimu ujao.

Kiukweli, harakati za wazi za United kutaka kumsajili Fabregas siku zote lilionekana litashindikana, pamoja na utayari wa United kulipa £35 million ili kumsaini nahodha huyo wa zamani wa Arsena.


Moyes ana shauku wa kufanya usajili wa mchezaji mkubwa hasa kwenye nafasi ya kiungo kwenye dirisha hili la usajili. Hii nafasi imekuwa ni tatizo la muda mrefu hasa katika miaka ya mwisho ya utawala wa Sir Alex Ferguson hasa baada ya Darren Fletcher kuanza kuumwa na Paul Scholes kustaafu mara ya kwanza. 


Ndio, United wasingeweza kuendelea kutoa ofa mfululizo kwa Fabregas kama wasingepewa ishara kwamba mchezaji mwenyewe anaweza akavutiwa na kujiunga na klabu hiyo ya Trafford, lakini licha ya hivyo kauli kutoka Nou Camp tangu mwanzo wa dirisha la usajili ni kwamba kiungo huyo angebaki FC Barca angalau kwa msimu mmoja mwingine. 


Inaaminika United walimgeukia Fabregas mara baada ya kushindwa kumpata Thiago Alcantara, ambaye inasemekana alitakiwa na United japokuwa hakuwahi kufanya nao mazungumzo lakini mwishowe aliamua kumfuata kocha wake wa zaman Pep Guardiola huko Bayern Munich.

Lakini kabla ya wawili hawa, United tayari ilishakumbana na tatizo la kukataliwa na wachezaji wengine wanne waliowataka huko wakati dirisha la usajili lilipofunguliwa.

Kwanza, ofa ya £35m kwa ajili ya kiungo wa Real Madrid Luka Modric ilikataliwa na magwiji hao wa soka la Hispania mwezi uliopita, wakati huo huo pia kwa usiri mkubwa United waliwafuata viungo wa Juventus Claudio Marchisio na Artulo Vidal, na kiungo wa Paris Saint-Germain Marco Verratti, kote huku waligonga mwamba.  


United walipewa ishara kwamba Verratti alikuwa tayari kutoka PSG kwenda Juventus na sio timu yoyote jambo ambalo liliwapelekea United kuangalia upatikanaji wa viungo wa mabingwa wa Italia Vidal na Marchisio. Kwa haraka Juventus  walikawakatisha tamaa United kwa kuwaambia wachezaji hao hawauzwi.

Wakati pia hatma ya Wayne Rooney ndani ya klabu hiyo ikiwa inawasumbua - Moyes sasa hana jinsi zaidi ya kuangalia 'Plan F'.

Marouane Fellaini - ambaye siku zote ndio amekuwa wa mwisho kwwenye listi ya United ya viungo wanaowataka na kwa hali ilivyo inaonekana kwamba mbegijia huyu atamfuata kocha wake wa zamani Old Trafford akitokea Everton. 


Moyes anavutiwa na Fellaini mwenye miaka 25, kiungo mwenye nguvu na ana uzoefu wa premier league, lakini kama Fellaini angekuwa ndio kipaumbele basi wangekuwa wameshamsajili miezi miwili iliyopita.

Fedha inayohitajika kuvunja mkataba wa Fellaini na Everton ni £22m - ni kipengele hicho tayari kimeshakwisha muda wake - hivyo sasa itahitajika United kuanza majadiliano mapya kabisa na Everton katika kuhakikisha wanakubaliana bei ya mchezaji huyo. 


Wakati Fellaini ni mtu ambaye sifa zake zinampa nafasi ya kuweza kufiti kwenye mfumo wa United, lakini sio dizaini ya mchezaji (kijina) ambaye mashabiki wa United wangependa kuona Moyes akifungua utawala akiwa nae.

Zoezi la Moyes kuanza utawala wake mpya limekuwa gumu kwa kutofanikiwa kwa mipango yake ya usajili - lakini pia kukiwa na suala la Wayne Rooney.

Pia imekuwa shida sana kwa mkurugenzi mkuu mpya wa klabu hiyo Ed Woodward kurithi vizuri mikoba ya David Gill - akiwa tangu aingie madarakani United haijasajili. 


United ilishinda vizuri sana kombe la ligi msimu uliopita, lakini wanahitaji kufanya usajili mkubwa na wenye tija kabla ya kufunguliwa kwa pazia la lligi kuu dhidi ya Swanse - August 17.

Mpaka sasa sera ya United katika usajili imeanza kuonyesha kufeli - ingawa huwezi kuwalaumu kwa hamu yao ya kutaka kusajili mchezaji ambaye tayari ni miongoni wa wale waliobora duniani.                                                          

3 comments:

  1. sa mbona ueleweki na kichwa chako cha habari umeandika kuwa cesc na wachezaji wengine watano walikataa kujiunga na mufc alafu ndani ya makala yako umeandika ni vilabu vyao ndio vimekataa kuwauza

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. jenga timu moyes kiungo ni sehem muhimu sana ya timu

    ReplyDelete