Search This Blog

Tuesday, August 13, 2013

EXCLUSIVE: SAKATA LA YANGA VS DILI LA AZAM TV - SERIKALI YAINGILIA KATI - YAWAITA MEZANI

Masaa takribani 24 tangu Raisi wa TFF kuiandikia barua Yanga akiwaambia ameomba maelezo rasmi kutoka kwa kamati ya ligi juu ya mchakato mzima wa namna Azam Tv ilivyoshinda tenda ya kuonyesha mechi za ligi kuu ya Tanzania bara kuanzia msimu ujao, serikali kupitia wizara ya habari, utamaduni na michezo  imeingilia kati suala hilo.

Habari za kuaminika kutoka chanzo cha habari hii, ni kwamba Serikali kupitia wizara wa Habari, Utamaduni na Michezo imeamua kuingilia kati sakata hilo ambalo limechukua nafasi kubwa katika vyombo hivi karibuni baada ya klabu ya Yanga kushindwa kukabaliana na mchakato mzima wa dili la haki za matangazo ya mechi za ligi kuu msimu ujao kupatiwa Azam TV.

"Serikali imewaita viongozi wa Yanga, Azam Media, TFF na Kamati ya Ligi kwa pamoja siku ya tarehe 14 mwezi huu, saa 5 asubuhi katika ukumbi wa wizara husika ili wafanye mkutano ambao utajaribu kuhakikisha pande zote zinakubaliana kwenye suala hilo kwa munufaa ya mchezo wa soka nchini," kilisema chanzo cha habari hii.

Hatua hii ya serikali inakuja wakati Yanga kupitia mwenyekiti wake Yusuph Manji akiwa ameitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama wa Yanga juu ya suala hili - mkutano ukiwa umepangwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu.

8 comments:

  1. Wengi wapeni jamani, mnambeleza wa kazi gani?? Akisusa wenzie wala!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Young Africans ..Umoja wa Mataifa...!!!!!!

      Delete
    2. Yanga ni timu moja lakini ndo wengi ukilinganisha na vilabu 13 vilivyokubali..kwani we aujui ilo...

      Delete
    3. bro mbona comments zangu huwa hauzipublish kwenye blog yako kama watu wengine?? nimekuwa mfatiliaji mzuri sana wa blog yako na kila mara nimekuwa nikikomet na naambiwa comment yangu itakuwa visible baada ya kuwa approved, je inamaana mawazo yangu ni pumba kiasi hayawezi kuwa published

      Delete
  2. si wawa ache,ubinafsi umewazidi,ili waendendelee kudominate ligi wangine waendelee kutabika




    ReplyDelete
  3. Kweli hii ligi inaendeshwa na yanga yaani yanga wakikomalia kitu kwenye ligi hii mpaka watakipata mfano kwenye swala la uamisho wa wachezaji utakuta kuna marumbano kati ya yanga na timu pinzani kwenye media utaona kelelela,logo za wazamini,mapato mwishoni wana shinda .ndo tuseme hii ligi bila yanga aipo

    ReplyDelete
  4. Kweli hii ligi inaendeshwa na yanga yaani yanga wakikomalia kitu kwenye ligi hii mpaka watakipata mfano kwenye swala la uamisho wa wachezaji utakuta kuna marumbano kati ya yanga na timu pinzani kwenye media utaona kelelela,logo za wazamini,mapato mwishoni wana shinda .ndo tuseme hii ligi bila yanga aipo

    ReplyDelete