Klabu ya Everton imeripotiwa kuikataa vikali ofa ya £28million kutoka kwa Manchester United kwa ajili ya kuwasajili Leighton Baines na Marouane Fellaini.
United
walituma ofa ya £16million kwa ajili ya Fellaini - wiki mbili baada ya kumalizika kwa muda wa kutengua kipengele chake cha kumuuza kwa ada ya £23.5million - na pia wakaongeza millioni £12 kwa ajili ya
Baines, taarifa kwa mujibu wa Liverpool Echo.
Lakini Everton kwa haraka waliikataa ofa hiyo kutoka kwa kocha wao wa zamani David Moyes, siku mbili kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England.
Inaaminika Everton watakuwa tayari kuwauza wachezaji hao angalau kwa bei ya kuanzia £38m na sasa inasubiriwa kama United watakuwa tayari kuongeza paundi millioni 10 ili kufanikisha dili hilo kabla ya siku 14 za dirisha la usajili hazijaisha.
No comments:
Post a Comment