Chelsea imethibitisha kwamba imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo Willian kutoka Anzhi Makhachkala.
The Blues wameshindwa kutoa taarifa rasmi ya ada ya uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri miaka 25, lakini ripoti zinasema watailipa klabu ya Russia kiasi cha £32million.
Tottenham walikuwa wanakaribia kumsajili mbrazil huyo, wakiwa tayari wameshakubaliana bei na Anzhi na hata vipimo vya afya vilishafanyika.
Lakini wakati wakiwa bado wanabishana kuhusu maslahi binafsi ya mchezaji, wawakilishi wa kiungo huyo wa kibrazil wakatoa ofa kwa Chelsea kumsajili kiungo huyo ambaye klabu hiyo ya London imekuwa ikimuwinda kwa muda mrefu.
Taarifa kutoka kwenye mtandao rasmi wa Chelsea inasomeka: "Chelsea Football Club inaweza kuthibitisha kwamba imefikia makubaliano na Willian pamoja na klabu ya Anzhi Makhachkala kwa uhamisho wa mchezaji huyo wa kibrazil.
Kilichobakia sasa ni kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza ambacho kinategemewa kutoka jumatano ijayo."
Willian anakuwa mchezaji tatu kusajiliwa na Chelsea kwenye dirisha hili la usajili, kufuatia kuwasili kwa Andre Schurrle kutoka Bayer Leverkusen na Marco van Ginkel kutoka Vitesse Arnhem, wakati huo Wayne Rooney akiwa bado ni kipaumbele kikuu katika usajili wa upande wa mshambuliaji.
No comments:
Post a Comment