UONGOZI wa Boom FC umelishukuru Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kuipatia msaada wa Sh 5,125,000 kwa ajili ya uendeshaji wa timu hiyo katika Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa Boom FC, Duni Mibavu amesema fedha hizo zitasaidia timu kufanya vizuri katika ligi na kuwapa morali wachezaji ili kuhakikisha timu hiyo inacheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
“Tunawashukuru wenzetu wa NSSF chini ya Mkurugenzi wake Dk. Ramadhan Dau kwa msaada mkubwa walioutupatia, hii inaonyesha ni jinsi gani walivyoguswa na na kilio chetu na kuamua kutusaidia ili tufanye vizuri,” alisema.
Duni ameomba na mashirika mengine pamoja na makampuni mbalimbali nayo kuiga mfano wa NSSF katika kuzisaidia timu za madaraja ya chini ili nazo zifanye vizuri.
Ndo mujitahd ili mufke premier league, cyo porojo nyng tu!
ReplyDeleteNa nyinyi ndo mujtahd ili mufke premier league, cyo porojo nying tu
ReplyDeleteSafi sn nssf ila viongozi wa boom fc mjipange jinsi ya kuzitumia vzr izo pesa sio mnaanza kugawana mara azionekani Slasher jr
ReplyDelete