Mshambualiaji wa Liverpool Luis Suarez amepewa amri ya kufanya mazoezi peke yake na kocha Brendan Rodgers, ambaye amesema hatua hiyo inakuja baada ya mshambuliaji huyo kuikosea heshima klabu hiyo.
Rodgers pia amekataa taarifa alizotoa Suarez kwamba klabu ilimhaidi kwamba ikiwa Liverpool watafeli kufuzu kucheza Champions League.
Suarez, 26, anajipanga kuwasilisha ombi rasmi la kuuzwa wiki hii ikiwa uhamisho wake utazuiwa.
"Hakujawahi kuwa ahadi yoyote ya namna hiyo baina yetu - kwa kifupi ahadi yoyote, na kwa maana hiyo hakuna ahadi iliyovunjwa," alisisitiza Rodgers.
"Klabu na wawakilishi wake walikuwa na mazungumoz kadhaa na alijua kila kitu kilivyokuwa kinaendelea .
"Ameikosea sana heshima klabu - lakini klabu hii ilimpa na kumfanyia kila kitu.
"Maneno yake niliyoyasoma kwenye vyombo vya habari yamenisikitikisha sana - lakini kazi yangu ni kubwa zaidi ya hili suala. "
Vyanzo vya karibu na Liverpool vinasisitiza uamuzi wa kumlazmisha Suarez afanye mazoezi kimpango wake ulifanywa kabla hata mchezaji huyo hajaongea jana na vyombo vya habari, hivyo uamuzi huo umetokana na kucheza kwake chini ya kiwango kwenye mechi za kirafiki.
Rodgers aliongeza: "Nitachukua maamuzi magumu juu ya suala hili. Nadhani Luis anajua sapoti aliyokuwa akipata kwenye klabu hii na hilo limekuwa jambo la siku zote.
"Kazi yangu ni kupigana na kuilinda klabu hii. Mazungumzo niliyokuwa nayo na yeye, anajua yalikuwa na yataendelea kuwa binafsi kati yangu na yeye."
hizi club anazozililia sasahivi hazikumuona wakati yupo Ajax? lazima awe na shukrani kwa liverpool kwani ndiyo imemuweka kwenye kiwango hicho cha kufanya hizo timu zimfuate sasahivi......Nico
ReplyDeleteAcha maneno mbofu mbofu kaka,hata hao wachezaji wengine wa Liverpool wamesajiliwa kutoka kwenye timu,mwacheni Suarez aondoke mbona arsenal wenzenu hawalazimishi mchezaji akitaka kuondoka?huko ni kukosa kujiamini
DeleteAcha kuleta maneno yako mbofu mbofu mwenyewe kila timu ina mipango yake kisoka. Suarez alikuwa kwny mipango ya liver msimu huu na co rahisi kupata mbadala wake kwa sasa so asubiri watu wajipange ataondoka tu
DeleteLiverpool kwa sasa hawana mchezaji mbadala wa Suarez ndio maana ni vigumu kwao kumruhusu kuondoka bila matarajio kumnasa striker mwingine.
ReplyDeleteHuyo Suarez ni msumbufu hapo adai kucheza Uefa na Akija Arsenal atadai Vikombe,Huyo ni msumbufu hafai,Hana nidhamu.
ReplyDelete