Klabu ya soka ya Uturuki, Fenerbahce, imepigwa
marufuku ya kushiriki katika michuano ya bara Ulaya msimu huu, baada ya
mahakama ya upatanishi ya michezo CAS, kuidhinisha uamuzi uliokuwa
umetolewa na shirikisho la UEFA kuwa klabu hiyo ilihusika na sakata ya
kupanga matokeo ya mechi.
Shirikisho la UEFA, liliipiga marufuku Fenerbahce mwezi Juni mwaka huu, baada ya kuwapata maafisa wa klabu hiyo na hatia ya kupanga matokeo ya mechi ili kushinda ligi kuu ya soka nchini Uturuki.
Kwa maana hiyo hata kama wangefanikiwa kuitoa Arsenal katika mechi ya kufuzu champions league isingekuwa na maana kwao kutokana kufungiwa huko.
Maneno ya mkosaji hayo!
ReplyDelete