Search This Blog

Thursday, July 4, 2013

ZDRAVKO MAMIC: 'JORGE MENDES' WA CROATIA ANAYEKULA ASILIMIA 20 YA MSHAHARA YA LUKA MODRIC - AGEUZA DINAMO ZAGREB KIBONDE KWA KUIPA UTAJIRI


Timu kubwa na yenye nguvu sana kwenye soka la Croatia haikufanya vizuri katika hatua ya makundi ya michuano miwili iliyopita ya Champions League. Kati ya michezo 12 waliyocheza, walipata pointi moja tu kati ya 36. Hwakufanya vizuri kabisa kwenye michuano hii, lakini kwao kucheza tu ilitosha sana.  Lakini Dinamo Zagreb imetoa vipaji vingi sana kwenye soka na tunavifurahia vipaji hivyo shukrani kwa mtu mmoja aitwaye  Zdravko Mamic.


Zdravko Mamic ni ni mkurugenzi wa michezo wa Dinamo. Amekuwa maarufu sana kwa tabia yake ya kuwatolea maneno machafu baadhi ya waandishi wa habari, akiwatishia kuwafanyia vurugu na kuwatukana wao na kazi yao. Pia amekuwa akihusishwa sana na sajili tata za wachezaji hasa wa nchi hiyo. Aliwahi kukamatwa baada ya kumtukana waziri wa michezo wa Croatia, lakini pamoja na vituko kocha huyu ana mazuri yake. Ni genius linapokuja suala la kufanya biashara ya wachezaji.

Katika kipindi cha miaka 10, tangu Zdravko Mamic ajiunge na Dinamo Zagreb, klabu hiyo imejipatia kiasi cha 160 million kutokana na mauzo ya wachezaji.

Dinamo Zagreb sio timu inayofanya biashara ya kuuza sana wachezaji barani ulaya kama ilivyo kwa Porto, lakini hawapo mbali kwenye. Benfica na Udinese pia nao wanafuatia, lakini inabidi vilabu hivi vyote vina misuli ya kifedha kuliko klabu hii ya Croatia.
Luka Modric mmoja ya wachezaji wanamuingizia fedha nyingi Mamic

Mamic anapata fedha nyingi kwa kukubali kuwauza wachezaji kwenda kwenye vilabu vikubwa. Mfano mzuri ni dili aliloingia na Luka Modric - walikubaliana na mchezaji huyo kupata asilimia 20 ya mshahara wake atakaokuwa akilipwa na klabu yake. Pia dili hilo limeendelea mpaka sasa mchezaji huyo akiwa na Real Madrid - kwa makataba wa miaka mitano na Madrid - Luka Modric atampatia kiasi kisichopungua 900 000 Euros Zdravko Mamic. 

Tangu awe mkurugenzi wa ufundi wa Dinamo mwaka 2003, ameshawabadilisha makocha 15 tofauti - waliokuwa wanatofautiana nae kwenye suala la kuuza wachezaji pale anapoona kuna maslahi yake yake binafsi.
 
BAADHI YA UHAMISHO WALIOWAHI KUFANYA DINAMO ZEGREB

Luka Modric to Tottenham , €21 million
Mateo Kovacic  to  Inter Milan , €15 million
Eduardo da Silva to Arsenal, , €15 million
Vedran Corluka to Manchester City, , €13 million
Dejan Lovren to Lion  , €9.5 million
Mario Mandzukic to Wolfsburg,  , €9 million 
Pia hivi sasa Mamic yupo katika mazungumzo na Tottenham katika kukamilisha baishara ya kuwauza wachezaji wawili Tin Jedvaj na Alen Halilovic ambaye anatajwa kuwa mrithi wa Luka Modric. Dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya paundi millioni 18 - na hapo Mamic ana kato lake pamoja na kuwa na mikataba binafsi na wachezaji hao wawili.

Taarifa nchini Croatia zinasema Mamic yupo katika matayarisho ya kuanzisha kampuni ya uwakala wa wachezaji, ili kufuata nyayo za wakala maarufu barani ulaya Jorge Mendes.

No comments:

Post a Comment