Search This Blog

Thursday, July 18, 2013

WENGER: HATUJAKARIBIA KUMSAJILI MCHEZAJI YOYOTE MPAKA SASA - TUNAO UWEZO WA KULIPA MSHAHARA WA WAYNE ROONEY'

Wakati wa mashabiki wa klabu ya Arsenal wakiwa wanasubiri kwa hamu usajili wa wachezaji kwenye klabu yao - kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema kwamba klabu hiyo mpaka sasa haipo karibuni kumsajili mchezaji yoyote.

Kocha huyo wa kifaransa ambaye ndio kocha aliyedumu muda mrefu na timu kuliko kocha yoyote kwenye ligi kuu ya England, amepewa fedha nyingi za usajili msimu huu, na mpaka sasa amemsajili mchezaji mmoja tu - mshambuliaji wa timu ya Ufaransa chini ya miaka 20 Yaya Sanago kwa uhamisho wa bure kutoka  Auxerre.

Wakati mashabiki wakiwa na tumaini la kusajiliwa kwa mchezaji mkubwa, kocha huyo mwenye miaka 63 ameonya kwamba mpaka sasa hawajakaribia kumsaini mchezaji yoyote.

“Ushindani barani ulaya ni mkubwa kwa sasa. Kuna fedha nyingi lakini hakuna wachezaji wengi wa kuwasajili. Tunajitahidi sana kufanikisha usajili lakini mpaka sasa hatupo karibu kusajili mchezaji yoyote.

Wenger pia alimzungumzia mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney ambaye amekaririwa akisema yupo tayari kumsajili mchezaji huyo kwenye timu yake ya Arsenal.

"Ilitokea kwetu msimu uliopita na inaweza ikawatokea wao United msimu huu. Rooney yupo kwenye mkataba wa miaka mwili na United, hivyo sasa kilichobaki ni maamuzi ya United. Lakini sisi kama Arsenal tuna uwezo wa kumsajili na kumlipa mshahara wake mkubwa Wayne Rooney."

No comments:

Post a Comment