Kwa miaka mingi zimekuwepo tetesi zimekuwepo juu ya malalamiko kwamba vilabu vikubwa vya Spain vimekuwa vikipata msaada wa kifedha kutoka kwenye mabenki, kupitia serikali yao.
Tuhuma hizi zimezidi kuwa kubwa hivi karibuni kutokana na madeni waliyonayo vilabu hivi, lakini bado wamekuwa fedha nyingi kufanya usajili na kulipa mishahara mikubwa sana kwa wachezaji. Watu wengi nchini Spain wanasema kwamba sio jambo zuri kwa vilabu kupokea msaada wa kifedha na kutumia vibaya katika nchi ambayo uchumi wake wake umeyumba sana. Hali ya uchumi wa Spain imekuwa mbaya mpaka sasa asilimia 52 ya vijana wa nchi hiyo hawana kazi za kuwaingizia vipato.
Real Madrid na Barcelona zote zimekanusha madai ya kupokea msaada kutoka kwenye mabenki kupitia serikali.
Raisi wa Bayern Munich ya Ujerumani, Uli Hoeness, alilamika wakati taarifa za madeni ya klabu hizi mbili zilipotoka hadharani. Alisema: "Mataifa mengine yanatoa mabilioni ya fedha kusaidia uchumi wa Spain, lakini serikali ya nchi hiyo imekuwa ikiviacha vilabu hivi kutolipa madeni yao ya bank na kodi pia."

Professor José María Gay de Liébana, wa chuo kikuu cha Barcelona, anakubaliana na hoja akisema:
''Hoeness yupo sahihi. Ikiwa mie sitolipa kodi yangu, then mamlaka za kiserikali lazima zinikamate. Lakini hilo halifanyiki kwa kwa vilabu hasa hivi vikubwa ambavyo vinapendelewa tofauti na ilivyo kwa kampuni nyingine."
Kwa mujibu wa scisports.net, jumla ya deni la Barcelona ni €359,796,000 ($461,654,247 USD), wakati Real Madrid wanadaiwa kiasi cha €473,943,000 ($608,116,263 USD). Lakini bado vilabu hivyo vinatumia fedha nyingi sana kununua wachezaji wapya na kuhakikisha mastaa wao wanalipwa fedha nyingi. Lakini ni vipi klabu hizo mbili zinaweza kufanya kazi zake vizuri na kupokea msaada mkubwa kutoka serikalini wakati nchi yao ipo katika mtikisiko mkubwa wa uchumi?
Vilabu vingine vya Spain vikiwemo Valencia, Deportivo La Coruna, Racing Santander, Atletico Madrid na vingine vingi vina deni la jumla linalofikia kiasi cha €2.19bn. Jumla ya €690m ni za kodi ya serikali.

Michezo, hasa soka ni kitu muhimu sana kwa Spain. Wamefanikiwa sana kupitia soka na labda kama ingekuwa sio kwa kuvisaidia vilabu hivi - tatizo la uchumi lingekuwa kubwa zaidi kwenye nchi yao. Viwanda vya nchi hiyo vimekumbwa na anguko, Catalonia inataka uhuru wao; maandamano yapo Spain nzima. Nchi hii ipo kwenye dimbwi kubwa la matatizo ya kiuchumi, lakini vilabu vyao vikubwa vinatumia fedha kama fedha hizo zinaanguka kutoka mtini pamoja na kuwa na madeni makubwa ya kodi ambazo zingeweza kusaidia matatizo mengine yanayoikumbuka nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment