Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya TP Mazembe ameendelea kung'ara kwenye timu hiyo baada ya juzi kuifungia bao muhimu la ugenini klabu yake ilipokuwa ikicheza na klabu ya ES Setif ya Algeria katika mchezo wa kombe la CAF.
Samatta alifunga bao hilo kutoka na mpira wa faulo uliotemwa na kipa wa Setif na yeye akaumalizia bila kupoteza nafasi katika dakika ya 81. Dakika moja baadae Setif wakiwa na sapoti kubwa ya mashabiki wao walirudisha bao hilo kupitia mchezaji M. Delhoum. Kutokana na matokeo hayo timu zote za kundi B zinabaki pointi moja moja, baada ya CA Bezertin ya Tunisia kutoka sare na FUS Rabat ya Morroco.
Team | Pld | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
CA Bizertin | 1 | 0 | 1 | 0 | 1 | 1 | 0 | 1 |
TP Mazembe | 1 | 0 | 1 | 0 | 1 | 1 | 0 | 1 |
ES Sétif | 1 | 0 | 1 | 0 | 1 | 1 | 0 | 1 |
FUS Rabat | 1 | 0 | 1 | 0 | 1 | 1 | 0 | 1 |
Safi sana kijana (Mbwana Samatta)...najivunia kuwa Mtanzania kupitia wewe. Ongeza juhudi uvuke hatua uliyopo sasa na Mwenyezi Mungu atakusaidia.
ReplyDeleteSafi sana kijana Mbwana Samatta...Wakati mwingine nimekuwa nikijivunia kuwa Mtanzania kwasababu yako maana umekuwa ukiipeperusha vyema bendera ya nchi yetu huko ulipo. Ongeza juhudi uvuke hatua hiyo ili hatimaye mwisho wa siku inshallah tukuone ukicheza ile ligi ya mabingwa barani Ulaya.
ReplyDeletesafi xana kaka,
ReplyDeletejitahd utafka mbal
Nzuri tubebe wabongo
ReplyDeleteSafi tutangaze wabongo tujulikane
ReplyDeleteNzuri tubebe wabongo
ReplyDelete