Search This Blog

Saturday, July 20, 2013

TIMU ZA AFRIKA MAGHARIBI ZIZIDI KUKATWA POINTI MICHUANO YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014 - GUINEA NAYO YAKATWA POINTI 3 KWA KUCHEZESHA MCHEZAJI ASIYERUHUSIWA KISHERIA

Kiungo wa Equatorial Guinea Emilio Nsue, mfungaji wa hat trick katika ushindi wa mabao 4-3 katika mechi ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Cape Verde, alikuwa haruhusiwi kucheza mchezo huo na hivyo timu yake ya Guinea imepokonywa ushindi wa mechi hiyo, Fifa imesema leo Ijumaa.
Cape Verde wamepewa ushindi wa mabao 3-0 wa mchezo huo uliochezwa March 24, hivyo wameongeza matumaini ya kuwang'oa Tunisia kwenye kilele cha kundi B

Pia FIFA imewapa pointi ushindi wa mabao 3 Cape Verde wa mchezo wa marudiano, uliochezwa mwezi uliopita, baada ya mchezaji wa Guinea anayekipiga - Nsue ambaye alicheza katika mchezo huo na akiwa haruhusiwi kisheria. Cape Verde walishinda mchezo huo kwa mabao 2-1. 

MSIMAMO WA KUNDI ULIVYO SASA:
  Team P W D L GF GA GD Pts
1 Tunisia 5 3 2 0 10 6 4 11
2 Cape Verde 5 3 0 2 9 4 5 9
3 Sierra Leone 5 1 2 2 7 8 -1 5
4 Equatorial Guinea 5 0 2 3 4 12 -8 2

1 comment:

  1. hizi nchi hufuatilia zenyewe kwa mchezaji wenye mashaka nae au fifa tanzania vp wapinzani wao walikuwa safi kucheza angetile amkaaaaa baba

    ReplyDelete