Timu ya Taifa (Taifa Stars) imewasili Uganda jioni hii
Jumatano tayari kuikabili Uganda Cranes kwa mechi ya marudiano kutafuta tiketi
ya kucheza katika mashindano ya CHAN.
Kikosi hicho chichi nye wachezaji 20, kiliwasili muda mfupi
baada ya saa kumi alasiri huku wachezaji na benchi la ufundi wakiwa na
matumaini makubwa.
Akiongea mara baada ya kuwasili Kocha wa Timu ya Taifa Kim
Poulsen alisema wamejiandaa vizuri wakiwa Mwanza na ana imanikikosi hiki
kitabadili matokeo ya awali ambapo Stars ilifungwa 1-0 na Cranes Jijini Dar es
Salaam.
Alisema licha ya kuwakosa wachezaji Shomari kapombe na
Mwinyi Kazimoto, ana imani na kikosi chake hiki kuwa kitafanya makubwa Kampala.
“Tumekuja kubadilisha mahesabu kwani tumejiandaa vizuri
kabisa,” alisema Poulsen.
Wadhamini wa Stars, Kilimanjaro Premium Lager wamewaomba
watanzania wasikate tama kwani Stars bado ina nafasi kubwa ya kupindua meza.
“Sisi kama wadhamini bado tuna imani na Stars na tunajua
watatuwakilisha vizuri ni vyema watanzania wawe na imani na kuiombea dua timu
iibuke na ushindi mnono katika mechi hii ya marudiano,” alisema Meneja wa Bia
ya Kilimanjaro Premium Lager, george Kavishe.
Mechi hii ni gumzo kubwa Jijini Kampala kwani baadhi ya
waganda wana hofu kuwa henda wakafungwa nyumbani kwao.
Mechi hii itapigwa katika Uwanja wa Nambole Jijini Kampala
JUmamosi hii saa kumi jioni.
Mashindano ya CHAN yanatarajiwa kufanyika Januari mwakani
nchini Afrika Kusini.
hiv hii mechi itarushwa chanel ipi???
ReplyDelete