Search This Blog

Wednesday, July 3, 2013

SABABU KWANINI WAYNE ROONEY HAKUWEZA KUWA KAMA CRISTIANO RONALDO

WAYNE Rooney hakuwahi na hatoweza kuja kuwa kama mchezaji mwenzie wa zamani wa Man United Cristiano Ronaldo kwa sababu hapendelei kujituma kufanya mazoezi gym, kocha wa zamani wa klabu hiyo amesema. 

Wazza — ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akisumbuliwa na suala uzito wa mwili linalomletea matatizo kwenye uimara wa mwili - lakini pamoja na kuwa na tatizo hili - Wayne Rooney hapendi kufanya mazoezi ya viungo kwenye gym
Kocha wa zamani wa viungo wa klabu hiyo Mick Clegg amefichua: “Wayne hakuwa anaona umuhimu wa kwenda gym. Alikuwa akisema, 'Nipo hapa kucheza soka na sio kwenda gym'. Siku zote nilitamani aondokane na fikra hizo na kujituma zaidi kwenye mazoezi ya viungo.
Rooney na Ronaldo, 28, walicheza kwa pamoja Old Trafford kwa miaka mitano mpaka pale mreno huyo alipouzwa kwenda Real Madrid mwaka 2009.
Mick aliendelea: “Wayne siku zote amekuwa na mwili mkubwa na alikuwa akiogopa kuzidi kuwa mkubwa ikiwa angetumia muda mwingi gym kujifua.
Hilo ndilo lilomtofautisha na Cristiano Ronaldo. Ronnie alikuwa tayari kufanya chochote nilichomuelekeza na vingine zaidi.
Aliishi na kupumua soka 24/7 na kujituma kwake kwenye mazoezi hakuelezeki.
“Wayne angeweza kuwa vizuri kama alivyo Cristiano ikiwa angefuata hali ya kujituma gym kama ilivyokuwa kwa Ronaldo.
Rooney, 27, amekuwa akisumbuliwa na unene - jambo ambalo limekuwa likimsumbua kiasi cha kuathiri kiwango chake.

No comments:

Post a Comment