Search This Blog

Thursday, July 25, 2013

OFFICIAL: YANGA YAMALIZANA RASMI NA HAMIS KIIZA

Sakata la usajili la mshambuliaji Uganda anayekipiga kwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Dar Young African Hamisi Kiiza limefikia tamati rasmi baada ya Yanga na Kiiza kukubaliana kimsingi kuongeza mkataba mpya wa mshambuliaji huyo.

Kwa mujibu wa Hamis Kiiza ambaye nimekutana nae mapema leo ni kwamba anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili kabla hajaondoka kwenda kwao Uganda.
"Tumefikiana na klabu yangu - sasa nitaongeza mkataba na kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga msimu ujao. Baada ya kumaliza taratibu zote za kusaini mkataba mpya nitarudi nyumbani Uganda mara moja kabla ya kurudi kuja kujiunga rasmi na wenzangu kwenye pre-season," Kiiza alisema. 

9 comments:

  1. Yanga Afrika wameshindwa kutafuta strike wa ukweli mpaka wanaamua kumsainisha KIIZA.Kwa usajili huu wa Yanga hawavuki round ya kwanza ya klabu bingwa.Hawana striker wa ukweli,kwani wote waliopo pale ni viungo tu.Ukiangalia anavyocheza TEGETA ni ajabu ajabu tu(KIMAGUMASHI),kidogo KAVUMBAGU anaafadhali sababu anaweza kupiga hata vichwa.KIIZA ni type ya kina TEGETE ingawa yeye kidogo amemzidi TEGETE.So klabu bingwa imekaa vibaya kwa Jangwani,wapende wasipende.

    ReplyDelete
  2. Timu yangu YoungAfrikans tunaua sana vipaji vya wachezaji,kwani mpaka sasa tumesajili washambuliaji 9 sijui nani atakaa benchi na nani atacheza kati yao.Mimi nashauri wengine watolewe kwa mkopo huko Rhino,Mbeya City,Ashanti etc.Mfano Teget atolewe mkopo maana hamna anachofanya,Bahanuzi naye atolewe mkopo,Nizar mkopo ili angalau waliobaki nao wawe wanapata nafasi ya kucheza.Mimi nilikuwa sioni umuhimu wa kumsajili KIIZA wakati JAVU anakuja Yanga(ameshaanza zoezi).Mnapoteza pesa bure tu.Timu moja ina ngasa,kavumbagu,bahanuzi,kiiza,javu,kondo,lusajo,msuva,nizar etc.Toa wengine kwa mkopo angalau nao wawe wanacheza huko waendako then ubaki na strikers wa4 au wa5 tu.Huu ni ushauri tu,maana tunaonekana sasa Yanga tuna-tamaa hatujui tutendalo.CHEPEEEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sidhani kama ni sahihi kuwatoa wachezaji kwa mkopo ilhali viwango vyao ni vzr tu. Ktk mashindano ya kimataifa hii ndio safi, bandika bandua.
      Labda kwa upande wa Yanga, TEGETE aodoke tu coz anua vipaji na viwango vya wenzie, anawatia sana misumari. Angeachwa tu. Kika foward akija basi si lolote.

      Delete
  3. Yanga yangu nimeshangzwa sana na kumpa kiiza mkataba mi kwa mtazamo wangu kiiza tegete na bahanuz..wakae pembeni..huruma inatosha wapishe wengine...watolewe kwa mkopo kabisa mchango wao kawaida sana kina javu msuva madogo wanajua wanozea bench kabisa..think about this tusisajili ili kuzuia timu pinzani wasisajili..mimi kma shabiki wa kutupwa wa yanga yangu ndo hayo...ikumbukwe tunaenda club bingwa.

    ReplyDelete
  4. Vizuri sana Uongozi wa YANGA,, kuna wachezaji ambao ni wapambanaji....mmojawapo ni kiiza,, si kwamba ana kipaji kikubwa but hucheza kwa kujitoa kwa ajili ya timu...hii ni tofauti na wachezaji wengi hasa wa tz ambao hutumia asimilia 60 ya uwezo wao tu uwanjani.. Mtofautishe kiiza na Niyonzima......NIYONZIMA ana kipaji sana but masihara mengi sana,, ucheza na jukwaa,,, mtofautishe na tegete ambaye hukata tamaa akiwa uwanjani.....Nadhani hii ni sprit ya Waganda.. Tz yaweza kuwa na vipaji kuliko UG, but wangana wanatuzid commitment. Hivi huyo oloya wanayemgombania siri yake kubwa ni hardworking,, nilimuona CECAFA hapa dar alivyokuwa anawatesa mabeki wetu wavivu.

    Back to the point,, kiiza ni mchezaji ambaye kila mwalimu mpira (Walimu wanao abudu kujituma) angepaswa kuwa naye kikosini. Ndo maana kwenye mechi ngumu anang'ara kasoro mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi dhidi ya simba last season. Ni mtu ambaye utafikiri ni shabiki wa timu anayoichezea ya YANGA,..Mnamkumbuka mechi dhidi ya ZAMALEKI? MECHI YA MTIBWA mzungo wa pili wa ligi?

    Kiiza ni tofauti na wachezaji wengi wa YANGA.... NAMSHABIKIA SANA, si kipaji chake bali jitihada zake, hana masihara...Mi nimecheza mpira hapo mbagala kuu na Hamis Thabit(Kiungo mpya wa yanga) ana kipaji kumzidi kiiza lakini nina doubt na kujitambua na commitment yake awapo kazini.. huu ni ugonjwa wa watanzania wengi hata maofisini ni uvivu na kulalamikia tu..(ni madhara ya Ujamaa)

    ASANTE SANA JANGWANI KWA KUMPA MKATABA MFANYAKAZI BORA WENU( HAMIS KIIZA),,, TENA HAKUSTAHILI MKATABA WAKE UISHE NANYI PASIPO KUMPA MKATABA MPYA..


    ReplyDelete
  5. Yanga kwa kifupi akili hamna.

    ReplyDelete
  6. Kiukweli sikuona sababu yoyote ya kumhangaikia saaana. Kiiza Nilitegemea viongozi wangetafuta mastraika wawili wa ukweli kwa kuwa klabu itashiriki mashindano makubwa mwakani, naomba viongozi viongozi ease makini Kiukweli.

    ReplyDelete
  7. yanga kwa usajili huu mliofanya ni dhahiri kwamba umejiandaa na ligi kuu ya tanzania bara na si klabu bingwa afrika , kwa akili yenu mnavyo jidanganya mtamfunga nani ? Katika afrika na timu yenu hiyo ? Yanga badilikeni kila mwaka akili ni zile zile ?

    ReplyDelete
  8. mmmh, hii hatari, ukijumlisha javu inakuaje?

    ReplyDelete