Search This Blog
Friday, July 19, 2013
NDOTO ZA KUREJEA UNITED ZAZIDI KUFUTIKA - CRISTIANO RONALDO AIWEKA SOKONI NYUMBA YAKE YA JIJINI MANCHESTER
Matumaini ya mashabiki wa Manchester United kuona kipenzi chao Cristiano Ronaldo akirejea kuitumikia klabu hiyo jana yalizidi kupotea baada ya mchezaji huyo kuiweka sokoni nyumba yake aliyokuwa akiishi wakati yupo nchini England kabla ya kujiunga na Real Madrid.
Ronaldo, 28 — aambaye alijiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa £80million mnamo mwaka 2009 — amekuwa akiuhusishwa sana kurejea Manchester United.
Lakini mreno huyo sasa ameiweka sokoni nyumba yake yenye vyumba vitano iliyopo kwenye eneo la Alderley Edge, Cheshire, kwa bei ya £3.75million.
Chanzo kimoja cha habari kilisema: “Mashabiki wa United mara zote walikuwa wanajua hatua ya Ronaldo kutokuiuza nyumba yake iliyopo jijini Manchester ilikuwa ni kwa sababu alikuwa na mpango wa kurejea mjini labda kujiunga na United, lakini baada ya mwenyewe jana kuiweka sokoni nyumba hiyo - inayoonyesha matumaini ya Ronaldo kurudi Old Trafford yanazidi kufutika.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment