Search This Blog

Tuesday, July 2, 2013

MIAKA 10 YA ROMAN ABRAMOVICH BAADA YA KUNUNUA CHELSEA PART 1: HAWA NDIO WACHEZAJI WALIONG'ARA NA WALIOFELI DARAJANI CHINI YA UTAWALA WAKE

Wakati Roman Abramovich alipoinunua  Chelsea kutoka kwa Ken Bates miaka 10 iliyopita, hakuna aliyeweza kutabiri namna ambavyo mrusi huyu angeweza kuitingisha Premier League.

Huku akiwa ameona Manchester United ikitawala soka la kiingereza tangu kuanzishwa kwa premier league, The Blues ghafla wakawa moja ya timu zilizoanza kutishia utawala wa United baada ya utawala wa Abramovich kuanza kazi.

Katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, billionea huyu wa kirusi alitoa kiasi cha £150million za usajili - akiwaleta wachezaji kama Hernan Crespo, Claude Makelele na Juan Sebastian Veron Stamford Bridge.
Hernan Crespo
Hernan Crespo mmoja wa wachezaji wa kwanza kabisa kusajiliwa na Abramovich


Pamoja na kufungua sana waleti yake kila mara, awamu ya kwanza ya zama za Abramovich ilitoa ishara juu ya tabia yake ya kutokuwa mvumilivu baada ya kumtimua kocha Claudio Ranieri mapema mwishoni mwa msimu wa kwanza  baada ya kuinunua Chelsea. 

Makocha wamekuwa wanakuja na kuondoka kila mara ndani ya klabu hii tangu wakati huo, lakini muongo wa kwanza wa utawala wa Roman umeleta mafanikio ya makombe 3 ya premier league, manne ya FA Cup, mawili ya kombe la ligi na Champions League pamoja na uropa League.

Kiasi cha £874m kinakadiriwa kutumika kwenye usajili huku  £1.5billion zikitumika kwenye mishahara na kulipa fidia ya makocha wanaotimuliwa kabla ya kumaliza mikataba yao.

Katika kuadhimisha miaka 10 ya utawala wa Roman Abramovich kwenye Premier League - tunagalie usajili bora na mbovu zaidi aliowahi kufanya ndani ya miaka 10 hii baada ya kuinunua Chelsea.


TOP 5 YA USAJILI BORA

1) Jose Mourinho

OK, Special One hakusajiliwa kwa namna ya kawaida kama wachezaji na alimgharimu Roman kiasi kidogo tofauti na wachezaji wengi waliomfuatia kuja Stamford Bridge, lakini Chelsea isingekuwa hivi ilivyo bila Mourinho.
Jose Mourinho remains Chelsea's most successful manager
 
 
Akiwa ametoka kushinda ubingwa wa champions league na FC Porto kwenye msimu wake wa mwisho na klabu hiyo ya kwao Ureno, Mourinho alichukua nafasi ya Claudio Ranieri mwezi June 2004 na kushinda ubingwa ligi na Premier League  katika msimu wake wa kwanza ndani ya Stamford Brifge.
The Blues walifanikiwa kuutetea ubingwa wao msimu uliofuata na mreno huyo akaiongoza timu hiyo kushinda League Cup na FA Cup bkabla ya kuondoka September 2007 kwa makubaliano na Chelsea.

Mapema mwezi uliopita Jose Mourinho alirudi rasmi kuifundisha Chelsea akitokea Real Madrid.

2) Didier Drogba

Alisajiliwa na Chelsea July 2004 kwa ada ya uhamisho wa £24m, Drogba alichukua muda kidogo kuanza kufunga pamoja na kufunga goli lake la kwanza katika mechi ya 3 ya kimashindano kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace.
Mwanzoni, wachambuzi wa soka hasa wale wapenzi wa Chelsea hawakuwa wakimpa nafasi ya kufanya vizuri darajani, lakini Muafrika magharibi huyo baadae aliwaonyesha vitu vya hatari mpaka wakaanza kumtukuza kuliko baadhi ya wachezaji wengi wa timu hiyo. 

Mshambuliaji alithibitisha ukali wake kwa kuwa mmoja wa wachezaji wa kuogopwa hasa kwenye mechi kubwa. 
Akiwa ameshashinda makombe matatu ya Premier League, manne ya FA Cup, mawili yaLeague Cup ana ngao za hisani mbili, Drogba akajihakikishia nafasi katika historia ya Chelsea kwa kufunga bao la kusawazisha kwenye fainali ya UCL dhidi ya Bayern Munich kabla ya kufunga penati ya ushindi na kuipa ubingwa wa kwanza wa ulaya Chelsea. 
Didier Drogba ensured Chelsea became kings of Europe
 
 

3) Claude Makelele

Wakati Makelele alipowasili darajani  2003, Ranieri alisema: “Nina saa nzuri sana, inaendeshwa na batri nzuri mno na Claude ndio betri yangu mpya. Claude ni muhimu sana kwa Chelsea.”
Kwa wakati huo watu wengi walimcheka juu ya maoni yako hayo lakini Makelele akawathibitishia watu hao mneno ya Ranieri kuhusu yeye.
Mfaransa huyu aliifanya Chelsea kuwa na safu ya ulinzi imara kuliko - na akazidi kuimarika pale alipokuja Mourinho darajani.
Mpaka wakati anaondoka Chelsea kwenda Paris Saint-Germain mwaka 2008, Makelele alishashinda makombe mawili ya premier league, moja la FA CUP, mawili ya ligi na moja la ngao ya hisani.
Katika kuonyesha ni namna gani aliweza kuilinda safu ya ulinzi ya Chelsea na hakuwa mtu anayependa kuacha majukumu yake na kwenda kushambulia - Makelele aliweza kufunga mabao mawili tu mpaka anaondoka kwenye klabu hiyo.

Claude Makelele made Chelsea tick


4) Ashley Cole

Baada ya kuondoka kwa utata mkubwa kwenye klabu ya Arsenal in 2006, Cole alitukanwa mno na mashabiki wa Arsenal - njia pekee ya kuwajibu aliyoiona Cole ilikuwa ni kucheza mpira mkubwa na kushinda makombe. 
Alishatwaa makombe kadhaa akiwa na Arsenal, lakini akiwa na Chelsea, beki huyo wa kushoto wa England aliongeza makombe ligi, Champions League na Europa League. 

Pia alishinda ngao ya hisani pamoja FA Cup mara nne na akaongezea taji lingine la Premier league kwenye CV yake.

Ashley Cole lifted the Champions League trophy in 2012
 
 

5) Juan Mata

Wakati akiwa mmoja wa wachezaji wapya kuwasili darajani, mhispani huyu ndio anayetoa sura ya mbele ya klabu ya Chelsea.
Juan Mata aliwasili akitokea Valencia kwa ada ya uhamisho wa £23.5m  August 2011 na alipewa tuzo ya mchezaji wa mwaka wa klabu baada ya kuisadia timu ya Roberto Di Matteo iliyoshinda ubingwa wa FA Cup na Kombe la mabingwa wa ulaya.


Kijana huyu anatajwa kuwa Gianfranco Zola, msimu uliopita aliiongoza Chelsea kushinda ubingwa wao wa kwanza Europa League. Japokuwa anatajwa kuwa anaweza kuuzwa za Mourinho darajani.
Juan Mata
 
SEHEMU YA PILI ITAENDELEA....................................................

1 comment: