Kama ilivyoripotiwa na na The Daily Telegraph huko nyuma mwezi June, kiungo huyo alilazimika kukanusha taarifa kwamba ni mtu ambaye yupo tu - yaani wa zaida ndani ya kikosi cha Mourinho.
Mourinho ilibidi azikanushe kwa nguvu taarifa za namna hiyo kabla hata hazijaanza kupata nguvu. Wakati Chelsea wakiwa wametuma ofa rasmi ya millioni 25, na ttarifa za Mata kuongezwa kwenye dili - hatimaye boss huyo wa zamani wa Real Madrid akaongea na kukanusha taarifa hizo.
Huku mwandishi mwandamizi wa The Daily Mail's David Kent akiripoti kwamba Mata ni mtu anayetakiwa na na Arsenal, sasa ni muda muafaka wa Mourinho kumhakikishia mchezaji wake umuhimu wake na namna alivyo na thamani ndani ya klabu hiyo.
Uwekezaji wa Chelsea wa wachezaji vijana uliofanywa hivi karibuni kwa kuongezwa kwa wachezaji kama Andre Schurrle na Marco van Ginkel unathibitisha kwamba huu ni msimu wa kuelekea kwenye mabadiliko. Ni wakati wa kiangazi ambao Mourinho anajenga msingi kwa ajili ya mafanikio ya baadae kwa kujenga kikosi akitakacho.
Mata inabidi katikati ya moyo wa kundi hili. Tangu ajiunge na Chelsea mnamo mwaka 2011, kiungo huyu mbunifu ameendelea kuwa mchezaji muhimu sana katika timu. Msimu uliopita tuliona umuhimu wake kwa Chelsea, alikuwa ndio moyo wa timu iliyoongozwa na Roberto Di Matteo na Rafa Benitez. Ndio daraja la zama mbili za Chelsea; mtu ambaye ataunganisha kikosi cha wachezaji wa zamani na wapya na kuunda kikosi cha mfanikio cha Jose Mourinho.
Kama ilivyooneshwa na Whoscored.com, alikuwa kiungo muhimu wa Chelsea katika mashindano yote msimu uliopita. Mata alifunga mabao 12 na kutoa assists 12 wakati klabu hiyo ikigombania nafasi ya 3 katika premier league. Mabao muhimu kwenye mechi kubwa dhidi ya Tottenham Hotspur, Arsenal, Manchester United na Everton yaliwasaidia Chelsea kukusanya pointi muhimu msimu uliopita.
Pia goli moja la Mata na assits tano alizotoa kwenye mechi nane za Europa League ziliisakisaida kikosi cha Roman Abramovich kushinda ubingwa wake wa kwanza wa Europa League mara baada ya kushinda champions league msimu uliopita. Goli lake na assits mbili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Steaua Bucharesti uliisadia The Blues kuingia robo fainali kwa ushindi wa jumala wa mabao 3-2. Assist yake kwenye mchezo wa robo fainali pia ukaivusha Chelsea dhidi ya Rubin Kazan lakini kama haikutosha Mata aliifadhi balaa kwenye mchezo uliofuatia.
Mchezaji huyo wa zamani wa Valencia alitoa pas mbili za mwisho katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Benfica katika fainali ya kombe la Europa.
Namna klabu inavyoendelea, umuhimu wake utaendelea kukua. Sio tu kwamba Mata ni muhimu kwenye mapngo wa maendeleo wa klabu bali pia ni mfuasi wa mpango huo, na pia bado hajafikia kiwango chake cha juu kabisa. Mourinho inabidi ampe msingi wa kukiboresha kiwango chake zaidi kwa faida ya timu, akikijenga kikosi chake cha mbele kwa kumzunguka Mhispania huyo.
Wachezaji wengi wanakuja na kupita katika milango ya Stamford Bridge, lakini huku Mourinho akiwa anaingia katika zama zake za pili kama kocha wa Chelsea, ni muhimu kwamba maendeleo ya Mata yawe moja ya vipaumbele vyake vikubwa. Klabu hiyo ya kiingereza ina gwiji wa baadae mikononi mwake.
No comments:
Post a Comment