Shabiki wa Manchester United Bwana Peter Bolton inawezekana ndiye mshabiki namba moja wa timu hiyo.
Bolton mwenye miaka 56 ambaye anatarajiwa kukwea pipa kuifuata United kwenye ziara ya pre-season tour barani Asia na Australia, hajawahi kukosa mchezo hata mmoja wa United ndani ya Old Trafford tangu mwaka 1974 na Bolton aliwahi hata kuamua kukosa harusi ya kaka kwa ajili ya mechi ya United.
‘Nilipokutana na mke wangu mwaka 1976 kwenye ukumbi wa disco, aliniuliza kama ningeenda tena wiki ijayo. Nilimjibu “Hapana, nitaenda kuangalia mechi dhidi ya Spurs White Hart Lane, tangu siku hiyo aligundua maisha yangu yanazungukwa na soka. Mwaka 1979, tulikuwa tumepanga kufunga ndoa na ilibidi nichague mwezi wa sita - kwa sababu nilijua hakuna soka mwezi huo!’
‘Wakati kaka yangu alipokuwa anaoa, alipanga tarehe ambayo iliangukia wikiendi katikati ya msimu. Nilibaki njia panda kwa sababu kulikuwa kuna mechi ya United ikicheza.... baadae niliamua kwenda kuangalia mechi Old Trafford na usiku nikaenda kwenye party ya harusi. Kaka yangu hakukasirika, alifahamu namna ninavyopenda kuiona United ikicheza.’
Wiki hii, Bolton anakwea pipa kwenda Sydney kwa ajili ya kuiangalia timu yake aipendayo ikijiandaa na msimu mpya - hakuenda Bangkok lakini sasa atakuwa na wiki tatu zenye mihangaiko kuliko akisafiri maili 30,000 na kutumia masaa zaidi ya 50 hewani kuifuata timu ya David Moyes kwenye pre season.
Bolton, ambaye anaishi maili kadhaa kutoka Old Trafford huko Timperley, anasema: ‘Nina mashaka kama nitabakiza chochote katika hizi £5,000 ndani ya kipindi cha wiki 3 zijazo. Ni vigumu kusema, kwa sababu huwezi kutabiri matumizi ya fedha lakini sina cha kujutia kwa sababu naenda kuiangalia timu yangu.
'Nina fahamu namna safari yangu itakavyokuwa, nitasafiri kwa umbali wa maili 30,000 na masaa kama 55 hewani. Tatizo ni kwamba hakuna hata ndege moja itakayokuwa ikienda moja kwa moja.
Gary Neville akisimama na bendera ya bwana Bolton yenye maandishi ya 'One Love'
‘Nitatoka Manchester mpaka Sydney kupitia Dubai. Then Sydney mpaka Yokohama kupitia South Korea. Halafu nitachukua treni mpaka Osaka kabla ya kuelekea Hong Kong kupitia Shanghai. Halafu nitakuwa narudi nyumbani Manchester kupitia Dubai na baada ya hapo safari itakuwa inaelekea Stockholm Sweden. Lakini hata kutokea kurudi nyumbani itabidi nipitie Oslo!'
Bolton, ambaye ameshahudhuria mechi za United za nyumbani zaidi ya 1,000 mfululizo na amekuwa akishabikiwa United tangu mwaka 1962, pia amekuwa akifuatilia mechi za timu ya vijana ya United pale Old Trafford.
‘Niliangalia michezo 120 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Ikiwa timu ya wakubwa haichezi, najaribu kufuatila timu ya vijana na timu ya reserve pia nyumbani na ugenini. Mwaka uliopita nilienda kuangalia wakicheza na Swansea na Southampton ugenini nikiisapoti timu ya vijana.
‘Mke wangu anajua ninavyopenda soka na kuna siku nyingi ndani ya mwaka ambazo ninatumia kuwa nae na familia kiujumla. Kwangu mimi soka ni kama kilevi changu, kwangu mimi ni familia na soka ndio vitu muhimu.'
Bolton na bendera yake ya akiishangilia United. Amesema kwamba mashabiki wa Atletico Bilbao ndio wastaarabu kuliko wote ambao amewahi kukutana nao.
kweliiiiiii
ReplyDeleteMU ya Fagie sawa, ngoja 2subili na ya Moyes km ataenda kushuka nayo daraja
ReplyDelete