Search This Blog

Monday, July 1, 2013

EXCLUSIVE: UKWELI KUHUSU SHOMARI KAPOMBE KUTAKIWA NA FC TWENTE HUU HAPA!


Kwa wiki kadhaa zilizopita kumekuwepo na taarifa nyingi zinazomuhusu beki wa kimataifa wa Tanzania na timu ya Simba, Shomari Kapombe kwamba  anatarajiwa kuondoka nchini hivi karibuni kwenda nchini Uholanzi kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya FC Twente.
Kapombe ambaye mwaka jana alishinda tuzo ya mwanasoka bora wa Tanzania amekuwa na mafanikio makubwa tangu alipojiunga na Simba akitokea Polisi Morogoro miaka mitatu iliyopita kwa kuisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Karibia vyombo vya habari vyote nchini vimekuwa vikikaririwa kwamba Shomari Kapombe anatarajiwa kwenda kufanya majaribio katika klabu ya FC Twente, ambayo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uholanzi katika msimu wa 2009-10, pia ilifanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu huo.
Kwa upande wa viongozi wa Simba mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Swed Nkwabi alikaririwa na gazeti la Mwananchi akisema kwamba,”timu atakayokwenda kufanya majaribio Kapombe huko nchini Uholanzi ni FC Twente, suala la ataondoka lini kwenda kufanya majaribio tutawaambia safari itakapokuwa tayari.”
Na kwa upande wa mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alikaririwa akizungumza kwenye kipindi cha michezo cha Spoti Leo cha Radio One akisema kwamba amekwishatoa kibali kwa Kapombe kuondoka nchini siku yoyote kuanzia sasa kwa ajili ya kufanya majaribio nchini Uholanzi.
Lakini baada ya kuwepo kwa taarifa hizi mtandao huu ulijaribu kufanya utafiti kidogo kuhusu suala la usajili wa mchezaji huyu kwenda FC Twente na kugundua vitu kadhaa vya utata kuhusu ukweli wa taarifa za Kapombe kutakiwa na klabu hiyo ya Uholanzi.
UKWELI
Mtandao feki
1: Kwanza kabisa chanzo kikuu cha taarifa za Kapombe kutakiwa na FC Twente zilizotolewa na mtandao wa www.fctwente.nu - ambao sio mtandao rasmi wa klabu ya FC Twente.  
Mtandao rasmi wa FC Twente
 Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa klabu ya FC Twente anuani yake ni hii (http://www.fctwente.nl/en/). Mtandao huu rasmi wa klabu hii haukuwa na taarifa zozote kumuhusu Shomari Kapombe au mchezaji mwingine wa Simba na Tanzania kiujumla.

2: Katika kupata uhakika zaidi mtandao huu ulijaribu kuwasiliana na afisa habari wa klabu ya FC Twente, Bwana Richard Peters kuhusu ukweli wa klabu yake kumtaka Shomari Kapombe kutoka Tanzania. Lakini afisa habari huyo alikanusha taarifa hizo na akisema kwamba klabu yake haina taarifa zozote kuhusiana na mchezaji huyu Kapombe. Akisisitiza kwamba mtandao ulioripoti taarifa za usajili wa Kapombe sio sahihi na zimetolewa na mtandao usio rasmi.
3: Mtandao huu haukuishia hapo, tulijaribu kumtafuta wakala anayeshughulikia kumtafutia Kapombe timu nje ya Tanzania, Bwana Denis Kadito ambaye alithibitisha ni ukweli kwamba alikuwa katika mpango wa kumpeleka Kapombe Uholanzi ili aanze kumtafutia timu ndani ya bara la ulaya, na alipoulizwa kuhusu taarifa za Kapombe kutakiwa na FC Twente, Dennis alisema hana taarifa zozote za Kapombe kutakiwa na FC Twente hivyo hawezi kutoa maoni yoyote kuhusu suala hilo.

11 comments:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. Mashabiki na wanachama wa Simba wameshazoea kudanganywa...
    Si hawa ndiyo hadi leo wanasubiri fedha za Okwi wakati watu walishalamba siku nyingi......!!!

    ReplyDelete
  3. Haa haaa.. Kwanza mtu anapokuwa kwenye Trial huwa haandikwi kwenye official website ya timu na wala ha-exist katika database ya klabu kwa kuwa si mchezaji rasmi wa timu kwa hiyo huyo kiongozi amejibu sahihi kabisa.

    Pili hakuna habari iliyokuwa inasema kuwa Kapombe anatakiwa FC Twente bali anakwenda kufanya majaribio

    Tatu hiyo website ya www.fctwente.nu ni website maalum kwa ajili ya mashabiki wa fc twente ambayo huwapa habari mbalimbali kuhusu klabu na tetesi za usajili na si website FEKI kama ulivyosema.

    Nne hizi ni baadhi ya website za mashabiki wa fc twente ambazo zimetoa taarifa ya " Shomari Kapombe on trial at FC Twente"
    1. http://www.twentefans.nl/nieuws/10192/-tanzaniaanse-linksback-kapombe-op-proef-.html

    2. http://www.fctwente.nu/fotos/fc-twente-nieuws/tanzaniaans-international-shomari-kapombe-op-proef-bij-fc-twente.html

    Mwisho
    Acha roho mbaya wewe,kumbuka kuwa viongozi wa timu za wenzetu ulaya huwa hawaongelei mchezaji ambaye si mchezaji rasmi wa timu yake..

    Mwacheni dogo akafanye majaribio akishindwa ashindwe mwenyewe acheni roho mbaya,fitina na majungu ya uyanga na simba.

    Mara Kiemba asaini Yanga,Mara Simba imekosea kumuacha Kaseja,kote huko umeshindwa na sasa umegeukia kwa Kapombe..3K..Ciao

    Daudi wa Kota

    ReplyDelete
  4. Wanachama wa Simba ndio wakome kila kudanganywa tu sasa wanataka kutuliza wanachama kwa kuuzwa kapombe kumbe fix Mara wadai wamemnunua Twite kumbe fix Mara Yondani hatochezea yanga kumbe fix na wala pesa yake hakupewa Mara kaseja anaachwa kama mbuzi wa kafara kuficha dhaifu wa viongozi ambao wameshindwa kazi wana Simba tuungane tuwatoe hawa viongozi kwenye mkutano Mkuu jamani

    ReplyDelete
  5. hakuna shida lisemwalo lipo kama halipo bac liko njiani linakuja

    ReplyDelete
  6. Wanajifanya wao ndiyo mabingwa wa kuuza wachezaji nje,watasababisha wachezaji wao wakauze matunda!
    Mr,Bm DOM

    ReplyDelete
  7. Acha roho mbaya we dauda unaandika kishabiki ili iweje?? Nlikua cjajua kwann tff hawakuitaji, kwa muonekano unaonekana una hakili kumbe umebeba boga tu juu ya mabega,mbna we unashndwa kuandka makala zenye maana kutwa unashnda kwenye internet kupakua za wenzio..nnamashka na elimu yako huu uandishi wa. dzain hii haukuz soka bali kududimiza..potia kwa mzee akilimali akulipe ukijira wako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. we unajua kaka ila wabongo tunapenda kudanganywa kuliko kupewa ukweli habari ndo hiyo, kaza uzi dauda ili uendelee kuwaumbua wanafiki wa soka

      Delete
  8. Mmmmmmmmh! Hili suala ni kusubiri muda jamani, why too emotional? Km Kapombe kaitwa kwenda kwenye majaribio muda utafika atakwenda na km c kweli basi tutamweka kapuni km ujenzi wa uwanja kwenye eneo hewa kule Bunju.
    Hatutakiwi kutukana wala kutumia lugha za kashfa, mafaniko ya Kapombe ni ya taifa pia, mkweli atajulikana iwapo na iwapo tu alichokisema kitadhihirika!

    ReplyDelete
  9. yawezekana shffih uko kweli lakini wewe na SUPERSPORT nani wanatoa habaari za ukweli?

    ReplyDelete