Search This Blog

Sunday, July 21, 2013

EXCLUSIVE: RAGE - KIGGY MAKASSY ATATIBIWA INDIA - SERIKALI WALITUMIA MIAKA 50 KUJENGA UWANJA WA KISASA, MIE RAGE NITAWEZA WAPI NDANIYA MIAKA MIWILI"

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amezungumza na kusema kwamba klabu hiyo itamtibia kiungo mshambuliaji wake Kiggy Makassy ambaye ni majeuhi wa goti kwa kumpeleka nchini India.

Akizungumza na wanahabari wakati akiondoka kwenye mkutano mkuu wa Simba uliofanyika jana, Rage alisema kwamba wameshafanya matayarisho ya kumpeleka Kiggy India kutibiwa na sasa kinachongojewa ni taratibu kukamilika ili mchezaji huyo wa Simba aende kushughulikiwa na madaktari bingwa wa tatizo lake.
"Kiggy atatibiwa, sababu za kumtibu tunazo kwasababu aliumia akiwa anaitumikia klabu yake ya Simba na pia fedha za kumtibia zimepatikana. Hii ndio Simba inayojali wachezaji wake." Alisema Rage kwa majigambo.

Pia Rage ambaye ni mbunge wa Tabora mjini amefunguka rasmi kuhusu suala la uwanja wa Simba, ambao tayari alishatoa ramani namna uwanja huo utakavyokuwa pamoja kusaini mkataba na mkandarasi kampuni ya Gidas ya nchini Uturuki. Akizungumza baada ya kuulizwa swali kuhusu suala hilo Rage alisema: "Kwenye suala la uwanja tayari tumeshalipia eneo na tunasubiri hati yetu. Unajua wakati mwingine inabidi niwe muwazi. Serikali yangu ya chama cha Mapinduzi imewachukua zaidi ya miaka 50 kuweza kujenga uwanja wa kisasa ule wa taifa wa sasa, sasa mimi Rage na kamati yangu tutajenga uwanja wa kisasa ndani ya miaka miwili uwezo huo tunautolea wapi? Ule uwanja wa Shamba la Bibi tangu uhuru ndio unakarabtiwa sasa. Tunachoomba watu wawe tu wavumilivu, tunaenda pole pole lakini kwa uhakika."

Kuhusu suala la mkakati wa kimaendeleo Rage amesema wamewatumiwa watalaamu kutoka chuo kikuu kuandaa mpango huo ambao ndio utafuatwa na Simba katika kujiendeleza. Pia ameahidi kuwa kutafanyika mkutano mwingine mkuu wa Simba mnamo mwezi wa 11 mwaka huu.

3 comments:

  1. rage na genge lake waache kuwafanya wanachama wapenzi wa simba pamoja wapenda soka kama wajinga serekali haikuwa na mpango wa uwanja na asidanganye serekali imejenga uwanja kwa miaka khamsini aache unafiki wake na ramadhani yake ya uongo aliofunga huku anaongopa serekali baada ya kuwa na uwanja wake wa uhuru haikushughulikia swala la uwanja wa kisasa ilijikita katika mambo mengine ya kimaendeleo uwanja huu mkubwa ni ahadi ya mheshimiwa mkapa kuwa hatatoka madarakani ila atawapa zawadi wana michezo ya uwanja na sio kusema serekali imejenga uwanja kwa miaka khamsini anaongopa mchana wa ramadhan haogopi hata funga yake.namkumbusha kama kasahau kama serekali imejenga uwanja kwa miaka 50ccm iliwezaje kuwa na biwanja kama kirumba mkwakwani sokoine na kwengineko asisahau wakati kunajengwa viawanja hivyo ilikuwa serekali ya chama kimoja cha ccm vipi ccm ilimudu kujenga viwanja vingi eerekali ijenge uwanja mmoja kwa miaka hamsini?amkumbuke mjeshimiwa gama na uwanja wa majimaji na huyohuyo ndie alihamasisha uwanja wa aliy hassan mwinyi tabora kwao rage na haikuwa miakaa hamsini majibu na kauli zake ni wazi kuwa hakuna kinachoendelea wala hakuna uwanja simba yumepotea na tumepoteza mwelekeo

    ReplyDelete
  2. Wana simba acheni uzumbukuku. rage atatoa wapi pesa ya kuwajengea simba uwanja. halafu mtamlipa nini? Timu haina kitu. mko juu ya mawe. hakuna kitega uchumi au lile jengo la msimbazi litajenga uwanja

    ReplyDelete
  3. Rage toka awe mbunge kawa mjinga vituvingi anaropoka tu.... kwan Azam wametumia miaka mingapi? Kwa kuwa mbunge ameshaona ndo kamaliza kila kitu(Ubabe 100%) Frankly speaking naumia sana Rage anavyoiongoza Simba, nilikuwa na matumaina nae sana. NADHANI MTU UKISHAKUWA MBUNGE WA CCM AKILI YAKE INAFIKIRI KIJINGA KABISA.(Sorry kutoa kauli za kisiasa hapa)lakin huu ndio ukweli.Lakin wana Simba tusife Moyo tutakuja kukaa sawa tu.

    ReplyDelete