Siku kadhaa baada ya klabu yake ya Simba kutangaza kumtema mchezaji wa mkongwe Juma Kaseja, leo hii kocha wa timu wa timu ya taifa ya Tanzania Mdenmark Kim Poulsen ametangaza kikosi cha timu ya taifa na kumjumisha Kaseja ndani ya kikosi hicho.
Poulsen akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho kinachojiandaa na michuano ya CHAN na kiporo cha mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Gambia, alisema amekuwa akisoma na kusoma sana habari zinamhusu Kaseja na klabu yake kupitia kwenye vyombo vya habari, lakini yeye kwa upande wake amesema bado anamuamini Kaseja na ataendelea kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi chake: "Nimekuwa nikisikia taarifa nyingi zinamhusu nahodha wetu Juma Kaseja, ningependa kuweka suala hili wazi kwamba Kaseja bado ni mchezaji mzuri na anafanya kazi nzuri sana ndani ya timu ya taifa. Ni nahodha mzuri kwa sababu ni kiongozi mzuri kwa wenzie nje na ndani ya uwanja. Hivyo kwangu hali itaendelea kuwa vile vile na nategemea kesho kumuona akijiunga na kambi ya timu ya taifa, ataendelea kuwa nahodha na pia golikipa namba 1 wa kikosi changu. Kuhusu yeye na klabu yake nisingependa kuyaingilia, lakini kwangu Kaseja bado ni muhimu kwa sababu amekuwa akifanya nzuri kwenye timu ya taifa. Kuhusu hatma ya huko mbele, tusubiri muda utaongea," alisema Kim Poulsen.
Wachezaji wengine walioitwa kwenye timu ya Taifa ni kama ifuatavyo: Makipa - Juma Kaseja Ally Mustapha, Mwadini Ally, Aishi Mwanula.
Mabeki: Aggrey Morris, Kevin Yondani, Canavaro, Shoamari Kapombe, Erasto, Vicent, David Luhende
Viungo: Mcha Khamis, Kazimoto, Sure Boy, Domayo, Chanongo, Kiemba
Washambuliaji: Mrisho Ngassa, Simon Msuva, John Bocco, Juma
Shabiki na mkereketwa kweli kweli wa mnyama bado nimepigwa butwaa!! Naamini na wengine kama mimi wapo! Juu ya issue ya kaseja na kinachoendelea Simba! Kimewakumba nini enyi viongozi wetu! Tunawasubiri mje na maelezo kuwa mlijichanganya kwenye hili! Mturudishie kaseja.La 5-0 naziona kabisa zilee zikichomolewa, aaaaaaah!!!
ReplyDeleteUongozi wa Simba mmekosea kumuacha Kaseja, cz he still in good performances. I do wonder why happened this, pls all fans of Simba lets ask the menagement of Simba, otherwise next season we are in dengerous to qualify in V.P.L 2013-2014.
ReplyDeleteWenye viwango wanabembelezwa na vilabu wasiondoke (e.g. Rooney). ikiwa una kiwango na unaachwa kama una akili timamu unapaswa kujiuliza maswali mengi. Mpira kwa siku hizi ni kazi ya heshima sana, kama mchezaji mzuri lazima uwe na vitu muhimu vyote vya mchezaji mzuri.
ReplyDeleteIli mchezaji awe Profession wa ukweli anahitaji pamoja na kiwango cha uchezaji, awe msikivu na moyo wa kujifunza siku zote, ajitambue, ayasome mazingira na nyakati hii itamuwezesha kujua yuko wapi na anapaswa kufanya nini na achukue ulekeo gani, Mchezaji asiyajua hayo hata kama ni mchezaji mzuri an limited chance ya kufikia matarajio yake na wadau wa tasnia yake.
Zaidi ya hapo ni kupokea matokeo ili imsaidie kujifunza kwa makosa yake. kwa wachezaji wenzake nawashauri wawe werevu, kwa sababu wajinga wanajifunza kwa makosa yao lakini werevu wanajifunza kwa makosa ya wengine.
Chujı katemwa au umesahau kumuweka?
ReplyDelete