Search This Blog

Wednesday, July 17, 2013

EXCLUSIVE: HUMUD - "LONGOLONGO ZA AZAM ZINANIFANYA NIKOSE NAFASI YA KWENDA KUCHEZA JOMO COSMOS YA SOUTH AFRICA'


Miezi mitatu baada ya kuripotiwa kufuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika timu ya Jomo Cosmos FC ya Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini, ndoto za kiungo wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC Abdulhalim Humud kucheza kwenye klabu hiyo inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Afrika ya kusini zimeanza kufifia baada ya kushindwa kujiunga na timu hiyo baada ya taratibu za usajili wake kukwamisha na Azam FC.


Kwa mujibu wa Humud ambaye amewahi kuvitumikia vilabu vya Mtibwa Sugar ya Morogoro na Simba, anasema yeye binafsi alikamisha kila kitu katika kuhakikisha dili lake la kwenda Cosmo linafanikiwa na hata alishakubaliana maslahi binafsi na timu hiyo inayomilikiwa na kufundishwa mwanasoka wa zamani wa nchi hiyo 
Jomo Sono.

"Mie nilikamilisha majaribio yangu na nikafuzu na siku tano kabla sijaondoka kule tayari nilishakubaliana kila kitu na klabu ya Jomo Cosmos. Niliporudi huku nyumbani Azam wakaniambia kila kitu kitakuwa sawa, pia walinipa barua ya kunijulisha kwamba sitokuwepo kwenye usajili wa Azam FC msimu ujao kwa kuwa nitauzwa kwenda Jomo.

"Niliwaachia Azam kila kitu katika kukamilisha taratibu za usajili kwa sababu ndio walikuwa wanasimamia hivyo vitu, lakini mpaka jana siku ya mwisho kukamilisha usajili hakukuwa na lolote lilofanyika. Tarehe ya mwanzo ya kukamilisha usajili na kwenda South ilipita ikabidi niende ofisini kuulizia na wakaniambia kila kitu kinaenda sawa na jana tarehe 15 ilikuwa ndio niondoke, lakini bado kimya.

"Kiukweli hili linakatisha tamaa, ukizingatia hata nauli ya kwenda kwenye majaribio nilijitolea mwenyewe, sio klabu wala mtu yoyote ambaye alinitolea, ilinitoka dola 800 kutoka kwenye mshahara wangu. Kiukweli napata machungu sana kuhusu suala hili. Muda mwingine tunaonekana wachezaji ndio tuna matatizo lakini ni hawa viongozi wa vilabu.,' alisema Humud


UNAWEZA KUSIKILIZA INTERVIEW YA HUMUD KUHUSU SAKATA LAKE LA USAJILI HAPO CHINI

Aidha katika barua rasmi aliyoandikiwa na Azam FC kuhusu uhamisho wake wa kwenda Jomo Cosmos, (mtandao huu unayo nakala) klabu ilimthibitishia Humud kwamba ameuzwa kwenda Jomo na kutokana na hilo imemuondoa kwenye usajili wa msimu ujao, lakini pia endapo tu ingeshindikana kukamilika kwa usajili wake basi angerudi Azam FC. Hata hivyo kwa sasa tayari Azam imeshamtema mchezaji huyo na pia uhamisho wake wa kwenda Jomo unaelekea kushindikana na kumuacha mchezaji huyo asijue nini atafanya msimu ujao wa ligi.

Tetesi za chini kutoka vyanzo vilivyo karibu na klabu ya Azam ni kwamba - Humud alikuwa hapatani na kocha Stewart Hall na hivyo alikuwa akitafutiwa namna ya kuondolewa kwenye timu hiyo.

1 comment:

  1. Pole jembe! Wanataka kukufanya kapeto ujue! yaani wa hapa hapa.komaa nao!

    ReplyDelete