Search This Blog

Monday, July 22, 2013

DAVID MOYES: "NI KWELI TUMETUMA OFA YA PILI KWA AJILI YA FABREGAS - TUNAAMINI TUTAFANIKIWA"


David Moyes amethibitisha kwamba Manchester United wametuma ofa ya pili kwa FC Barcelona kwa ajili ya kumsaini Cesc Fabregas na ameonya kwamba hayupo tayari kukata tamaa ya kumsaini nyota huyo wa kihispania
Akiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Nissan alisema kwamba CEO wa United Ed Woodward bado yupo kwenye mazungumzo na Barcelona baada ya kutuma ofa ya pili ambayo inatajwa kufikia kiasi cha paundi millioni 30.

Alisema: 'Uelewa wangu ni kwamba Ed alijibiwa na Barcelona na tukatuma ofa ya pili. Lakini Ed bado anaendelea kushughulikia suala hilo, na sio mimi binafsi.'
Alipoulizwa kama watafikia ya kusajili mbadala wa Fabregas ikiwa waashindwana na Barca alikiri, "Nadhani hatua hiyo hufikiwa wakati unapokuwa umekata tamaa ya kumsajili mchezaji unayemtaka, lakini unapokuwa unamtaka mchezaji mzuri unakuwa unataka kutumia kila nafasi kuhakikisha dili linafanikiwa. Na nina matumaini nitafanikisha hilo. Ninatumaini mambo yataendelea mbele vizuri. Kwa muda huu ninachoweza kuwaambia ni kwamba Ed Woodward anafanya kazi kwa bidii kuhakikisha dili zote za usajili zinafanikiwa na tuna matumaini baadhi ya sajili hizo zitafanikiwa hivi karibuni.'
Je manahodha wawili wa zamani wa Arsenal wataungana Old Trafford msimu ujao

Pia aliongeza kwamba anaelewa namna mashabiki wa United wanavyosubiri kwa hamu usajili wake wa kwanza mkubwa tangu kuanza kwa utawala wake. Mpaka sasa United imefanya usajili wa mchezaji mmoja tu kinda Guillermo Varela.

'Naelewa sana hamu yao, lakini kwa sasa hakuna ninachoweza kusema zaidi.'

No comments:

Post a Comment