Search This Blog

Friday, July 5, 2013

CAMEROON YAFUNGIWA NA FIFA BAADA SERIKALI KUINGILIA MASUALA YA SOKA


Cameroon imefungiwa kwa muda na FIFA kufuatia serikali ya nchi hiyo kujiingiza katika masuala ya chama cha soka nchini humo.

Tangazo la FIFA limesema kwamba kamati ya dharura ya shirikisho hilo la soka duniani imeamua kusimamisha kwa muda chama cha soka cha Cameroon FECAFOOT na uamuzi huo umeanza kutekelezwa mara moja kwa sababu serikali inaingilia masuala ya chama cha soka

Taarifa hizi zimekuja saa moja baada ya Cameroon kuzawadiwa pointi 3, kuwarudisha kwenye uongozi wa kundi I, baada ya Togo kuadhibiwa kwa kumchezesha mchezaji Jacques Alexys Romao, ambaye hakupaswa kucheza wa mwezi uliopita baina ya timu hizo mbili.

Hatua hii ya FIFA inawazuia Indomitable Lions kucheza mchezo wao muhimu wa kufuzu dhidi ya Libya September 6.

Taarifa rasmi ya FIFA ilisema: “"kamati ya dharula ya FIFA imeamua kufungia chama cha soka cha soka cha Cameroon kutokana na serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka ya chama hicho.

“Wakati wa kipindi cha kifungo hichi, Fecafoot inaweza isiwakilishwe katika michuano yoyote ya inayosimamiwa na FIFA na CAF, kuanzia ngazi ya taifa kwenye vilabu kwenye mechi za mashindano mpaka kirafiki."

No comments:

Post a Comment