Kocha wa Manchester United David Moyes leo hii amethibitisha kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney hayupo sokoni na ataendelea kuicheza klabu hiyo kwa mingi ijayo.
Akizungumza kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na klabu hiyo akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson, Moyes alisema: "Nimeongea na Wayne Rooney. Wayne yupo nyuma ya mabao 40 kumfikia Sir Bobby na
Denis Law. Wayne hauzwi - ni mchezaji wa Manchester United - na ataendelea kubakia kuwa mchezaji wa Manchester United. Nimekuwa na mikutano nae kadhaa. Amerudi kwenye hali nzuri na anafanya vizuri mazoezini. Tunajaribu kufanya kila kitu kumrudisha Wayne Rooney kuwa kama alivyokuwa zamani - Wayne Rooney ambaye tunamjua.
"Vyovyote vilivyotokea kabla, tunafanya kazi pamoja sasa. Macho yake yanaonyesha ni mtu mwenye furaha, ni lazima niseme Wayne hauzwi. Kuliwahi kuwepo mkutano wa siri baina ya Rooney na Sir Alex. Mie naendelea mbele sasa, sijui nini kilizungumzwa kwenye mkutano huo. Ninachofikiria sasa ni kusonga mbele na kufanya kazi ya kumrudisha Wayne Rooney kwenye ubora wake. "
Alipoulizwa kuhusu Cristiano Ronaldo, Moyes alijibu: "Sitomzungumzia yeye moja kwa moja na wachezaji wengine wa vilabu vingine. Lakini hii klabu siku zote imekuwa ikivutiwa na wachezaji bora duniani."
Pia Moyes alithibitisha kwamba winga mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace - Wilfred Zaha ambaye amekuwa akiwindwa na vilabu vingi kujiunga navyo kwa mkopo - Moyes amesema mchezaji huyo ataungana na Manchester United kwenye tour ya pre-season, kama ilivyo kwa wachezaji wengine.
Wakati huo huo alipoulizwa kuhusu usajili wa wachezaji wapya, Moyes amesema angependa kusajili wachezaji mapema lakini mambo yamekuwa yakichelewa kutokana na makocha ambao ndio wanaothibitisha uuzwaji wa wachezaji wengi wamekuwa likizo au ndio wanaingia kwenye vilabu vyao vipya.
No comments:
Post a Comment