Search This Blog

Sunday, July 14, 2013

BAADA YA KUTEMWA YANGA: NURDIN BAKARY AFUNGUKA - 'TWITE ALISAJILIWA ILI KUMMALIZA NSAJIGWA, KIIZA ALIPWE ANACHOSTAHILI - KASEJA ANASTAHILI KUENDELEA KUWA NAMBA 1 SIMBA'

KIRAKA Nurdin Bakari aliyeachwa na Yanga baada ya mkataba wake kumalizika amefichua siri baada ya kutamka kwamba Mbuyu Twite alisajiliwa na viongozi wa Yanga ili aje kumaliza kipaji cha Shadrack Nsajigwa.
Twite alisajiliwa na Yanga akiwa njiani kutua Simba ambapo mchezaji huyo amekuwa akipendelea sana kucheza beki ya kati lakini imemilikiwa na Kelvin Yondani na Nadir Cannavaro.
Twite alikabidhiwa namba ya Nsajigwa ambaye Yanga imemuonyesha mkono wa kwaheri kwa madai kwamba ameshuka kiwango na tayari Lipuli ya Iringa imemsajili kama kocha.
Nurdin alisema; “Hivi unajua Mbuyu (Twite) ni viongozi waliamua tu kumsajili bila kulishirikisha benchi la ufundi. Ndiyo maana unamwona anachezeshwa beki wa kulia badala ya beki wa kati,”alisema Nurdin aliyewahi kuichezea Simba na AFC ya Arusha.
Lakini viongozi wa Kamati ya Usajili wa Yanga wamesisitiza kwamba mchezaji huyo alikuwa chaguo la kocha Ernest Brandts ambaye amewahi kufanya naye kazi akiwa APR ya Rwanda.
Nurdin alisema baada ya Nsajigwa kutakiwa na Simba msimu wa 2011 na baadaye dili ikashindika alianza kuwekewa mizengwe: “Baada ya Nsajigwa kumalizana na viongozi wa Yanga, tulidhani yameisha. Fitna zilianza na kumletea mabeki wengi kwa lengo la kumshinikiza kocha awe anamweka benchi,” alisema Nurdin na kuongeza kuwa beki wa kwanza aliyesajili kwa nia ya kumpoteza Nsajigwa alikuwa Taita (Godfrey) kutoka Kagera Sugar.
“Lakini alishindwa kumweka benchi, baada ya kuona malengo yao hayajatimia walimletea tena beki mwingine Juma (Abdul) kutoka Mtibwa Sugar na baadaye akaja Mbuyu lengo lao likatimia.”
Nurdin pia amepinga vikali kutemwa kwa straika Hamis Kiiza na kipa Juma Kaseja.

Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Tabata, Nurdin alisema: “Unajua hawa viongozi wa Simba na Yanga wana chuki zao tu binafsi, mimi bado naamini Kaseja (Juma) ndiye kipa bora kwa Tanzania. Pia, ana nafasi ya kuendelea kuichezea Simba na kwa mafanikio makubwa.”
“Kama unataka kuchukiwa na viongozi wa timu hizi mbili dai chako, kwa jinsi namfahamu Kaseja ni mtu ambaye hataki kuburuzwa. Ni mtu ambaye yupo mstari wa mbele kudai haki yake. Nafikiri ndiyo yaliyomkuta kama ilivyo kwangu.”
“Kaseja bado atabaki kuwa kipa bora na hakuna anaweza kupinga hilo. Sidhani kama atakosa timu ya kuichezea. Ni mtu anayelijenga vizuri jina lake kisoka. Kwa upande wa Kiiza, nafikiri anastahili kudai kuongezwa mshahara na dau la kusaini mkataba mpya anafanya kazi na inayoonekana. Kwanini wanashindwa kuthamini mchango wake na kumpa kile anachostahili,” alihoji.
“Mbona Haruna (Niyonzima) alitaka na kuboreshewa masilahi yake, iweje inashindikana kwa Kiiza mpiganaji, kuna tatizo?  Viongozi wa timu hizi mbili wanachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu maendeleo ya soka katika klabu hizi mbili kubwa. Hawana malengo endelevu,”alisisitiza mchezaji huyo mwenye rasta.

CHANZO: MWANASPOTI

8 comments:

  1. Huyu ni mpuuzi kweli, kama Nsajigwa ni mzuri nini kashindwa kupambana na kubaki kwenye timu? Hivi Twite ni mchezaji wa kwanza kuhamishwa namba hapa duniani? Hivi hajui Mohamed Salim alikuwa beki mzuri saana costal union, alibadirishwa na kuwa namba 9 mzuri saana. Ahmed Amasha, alikuwa namba 6 mzuri saana, akabadilishwa kucheza beki 3. Huyu jamaa ni kiazi kabisa

    ReplyDelete
  2. Haya sasa, Naushauri uongozi wa simba kumrudisha Nurdin Bakari Simba na Hamis Kiiza kwani wachezaji hawa bado wana uwezo wa kucheza mpira. By Mkinga

    ReplyDelete
  3. Nurdiiiiin acha uongo na kujaribu kupofusha watu.kila mpenzi wa soka anajua jembe shadrack limechoka na yanga walitumia busara saaaana kumuongezea mwaka mmoja wenye maana ya yy kujipanga na binafsi nampongeza saaana shadrack kwa kutambua hilo kiasi cha kumfanya ajisomee kozi mbalimbali za soka na hivi sasa ni kocha tunayemuombea mafanikio.umeeleza mengi lkn mm nakuuliza swali moja tu.je ww waliposajiliwa kina Niyonzima na Frank Domayo lengo likuwa kuuwa kipaji chako? Acha ubabaishaji wa kibongo pambana na changamoto.

    ReplyDelete
  4. Wachezaji wa kitanzania huwa hawakosi sababu mkataba ukiisha co lazma usajiliwe upya na timu ile ile mbona wenzetu ulaya mchezaji akimaliza mkataba malalamiko ya kutobaki kwenye klabu huwa hakuna zaidi ya kuishukuru timu? Mfano Erick Abidal, Didier Drogba na wengne wengi mbona hawakulalamika na kueleza siri za timu zao? Badiliken vinginevyo mtabaki kulalamika tu bila maendeleo yoyote! Mchango wa Nsajigwa na Nurdin tunautambua lakini klabu haina uwezo wa kuwa na idadi zaidi ya wale wanaotakiwa kaka tafuta timu nyingne ligi kuu tz au katafute nchi nyingine

    ReplyDelete
  5. Mfa maji huyo,ooh eti viongozi wa Yanga na Simba hawataki kuona unadai chako.Je wewe unaidai Yanga??????????? na kiasi gani???????? Jipange upya nenda kapige soka huko Mwenge Vinyago huku kumeshakutupa mkono baba.

    ReplyDelete
  6. Huyu jamaa bana, anaongea km sio mwanasoka, yanga walitaka kuleta ushindani kitu ambacho ni muhimu ktk soka na si kuua kipaji cha nsajigwa

    ReplyDelete